Ushauri: Nimekuwa na tabia ya kuogopa kuoa

Kiti Chema

JF-Expert Member
Oct 18, 2017
1,791
1,940
Nawasabahi ndugu zangu mlio wazima na wale wenye shida kidogo Mungu atatia wepesi.

Niende kwenye kusudi maalumu, mimi ni kijana ambaye nikitazama idadi ya namba ya miaka yangu naona inakimbia.

Leo linalonifanya niandike uzi huu ni hii hofu ya kuoa niliyo nayo. Nimekuwa na tabia ya kuogopa kuoa na kujihi kuwa kama nikioa nahisi ndo nitajiongezea mizigo zaidi, maana kuna muda huwa najitathimini na kuwaza kwa sauti ikiwa marafiki zangu waliooa huwa wananisimulia changamoto wanazokumbana nazo katika ndoa au familia.

Je mimi nitaziweza hapo tu ndo swala la kuoa hukata na hamu inaniishia tena yapo mambo mengi huwa nawazaga.

Kwa wanasaikolojia hii hali inatokana na nini ikiwa kama ni habari ya uzinzi mimi huko siko maana nimelelewa katika misingi ya dini na ninaye mchumba mmoja tu ingawa nimepitia changamoto mbali mbali kupitia huyo binti lakini sikutaka kuwa leo nipo na huyu na kesho nipo na huyu.

Nitashukuru kwa mawazo yenu.
 
Una miaka mingapi?.
Una shughuli yoyote ya kukuingizia kipato?.
Ushapata mwanamke wa kumuoa?,maana huyo mchumba wako umesema kakusotesha sana
 
Maisha ya kusimuliwa siyo maisha yako ni maisha ya huyo msimulizi.
Ninawezaje kuikataa biashara fulani kwa kuwa nimesimuliwa changamoto zake na huyo msimuliaji bado yumo kwenye hiyo biashara!

Unataka kusema hakuna sehemu ya furaha katika ndoa?
Anyway maamuzi ni ya kwako unaweza ukabakia single milele ama ukaoa chaguo la moyo wako.
 
Kila ndoa inachangamoto zake, changamoto za rafiki zako ndio zisikufanye uoe sema tu haujajipanga kuwa na familia sio uwoga
 
Sasa unasema unaogopa kuoa wakati huo huo unadai una mchumba sasa huo ni uchumba gani au hujui kuna mpenzi, mchumba na Mke?

Sijaelewa shida yako.
 
... ninaye mchumba mmoja tu ingawa nimepitia changamoto mbali mbali kupitia huyo binti lakini sikutaka kuwa leo nipo na huyu na kesho nipo na huyu.

Nitashukuru kwa mawazo yenu.
Dah....acha ujinga Dogo....... mbona umeisha oa tayari...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom