Ushauri: Nilibadili kozi chuoni bila kumtaarifu mwajiri wangu

sir ronga

Member
Nov 25, 2016
90
150
Salaam wana JF,

Kama mada inavyodokeza, mimi niliwahi kuajiriwa serikalini kama mwalimu wa secondary kwa muda wa miaka minne. Baada ya hapo niliomba ruhusa ya kwenda masomoni kujiendeleza. Mara baada ya kufika chuoni, niliamua kubadili kozi na kusoma fani niliyokuwa naipenda hapo awali kwani nilishindwa kuisoma kutokana na changamoto za maisha ikiwemo kukosa ada. Kozi yenyewe ni ya miaka minne.

Mwaka mmoja baadae, nilitakiwa kuwasilisha ripoti kazini ila sikufanya hivyo kwani sikuwa nasomea education. Kila likizo nilikwepa kurudi kituoni kwa sababu mbalimbali. Nikiwa chuo mwaka wa mwisho(wa nne), likapita fagio la Magufuli mshahara ukasimama. Nilihesabika kama mtoro kazini.

Kwasasa nakaribia kuhitimu elimu yangu, na nipo katika mchakato wa kujiajiri na changamoto ni lukuki. Nikakumbuka nilipokuwa kazini nilikuwa mwanachama wa mifuko kadhaa ikiwepo PSPF na CWT na nilikuwa nachangia wastani wa 25,000 kwa mwezi kila mfuko kipindi nasitishiwa mshahara.

Naombeni ushauri katika haya na mengineyo:
1.Naweza kupata stahiki zangu kwa kipindi nilichodumu kazini?
2.Nawezarudi kazini ili hali sikusomea nilichoombea ruhusa?
3.Ikitokea nafasi nyingine ya kuajiriwa serikalini naweza kupitia hii kozi mpya bila tatizo?
4. Ushauri wa ziada wa nini nifanye kuhusu hili.

Ahsanteni.
 

kifinga

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
3,671
2,000
Mkuu hapo wafwaaa Lawson system wakiingiza jina lako utaonekana uliisha ajiriwa so watashindwa kukuingiza tena kwenye system we sasa focus secta binafsi
 

Yuda Iscariot

Member
Mar 2, 2017
72
150
Kajaribu kuongea na HR mmojawapo mnaefahamiana hapo job. Anaweza kukupa mwanga. By the way, kwa nini usingetafuta sababu yoyote ili kazini kwako uonekane umeextend mwaka?
 

JMF

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
918
1,000
Ulidhani JK angeendelea kuwa rais au? Chamsingi hapo kalime matikiti. Fuatilia fedha za mifuko nadhani unawezakupata kwani kama ulitumikia miaka minne, ilikuwa ni jasho lako. Ila hiyo mifuko sijui kama watakupa bila barua kutoka kwa mwajiri wako. Na waajiri sasahivi wamebanwa wanaweza wasikupe. Ngoja waje wajuzi wa haya mambo.
 

samsonsheshe

Member
Oct 30, 2015
5
45
Unatakiwa urudi kazin ukaongee na mwajir wako kama ni taarifa akubadilishie urudi kazin...huku nilipo pia kunamtu yuko na insue ka yako bt now kesharudi na pia kawekwa ofisi za ugavi harimashauri..ko wew mkuu komaa na mkurugenzi wako tu
 

zincate

Member
Mar 28, 2017
6
45
kwanza umetenda kosa
1:stahiki hutopata kwan umefukuzwa kaz kwa utoro
2:kwa mfumo wa ss ukiondolewa huwez ajiriwa tena kwan jina lako lpo kwenye data base
3:kwa kuwa uliamua kusoma ulichokupenda hopely utajiajir kupitia hyo fan,nikutakie mafanikio mema
 

Goodhearted

JF-Expert Member
Feb 15, 2015
562
500
Mimi mwenyewe niltaka nkasome kitu kingne kabisa apart from hii profesioal yangu lakini nikimfkiria huyu mdudu lawson najikuta nakuwa mpole ghafla
 

Handsome man

JF-Expert Member
May 6, 2017
899
1,000
Maamuzi uliyoyachagua nadhani ndo mda wa kuyatumia hapo jiajiri tu mkuu, huku kwingine umeshauza mech tayar
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom