Ushauri: Nifanye nini niweze kuthibiti pesa?

Shomary47

JF-Expert Member
Feb 12, 2021
224
348
Habari wana JF

Naomba Ushauri, Mimi ni Muhanga wa Kutokukaa na Pesa,ama nikipata pesa zinaisha bila kufanya kitu cha maana au kitu cha kuonekana.

Nimejitahidi saana Kuweka bajeti ya Mwezi nakuifata lakini nashindwa, najitahidi kuweka kumbukumbu ya matumizi yote ya siku ila nafanya kwa siku 2 siku ya 3 nasahu.

Kwa Mwezi kwenye mihangaiko yangu naweza pata faida mpaka ya 1,300,000 kwa mujibu wa daftari langu ka mauzo, Lakini mwisho wa mwezi ukiniuliza hiyo pesa iko wapi naweza nisiwe nayo, ama inakua imebaki kodogo saaana.

Naomba Ushauri, Nifanye nini ili pesa ninazopata kwenye mihangaiko yangu mwisho wa mwezi niione Yote mezani. Natanguliza Shukrani.

PXL_20220515_164932217.jpg
 
Jifunze kusema hapana. Jifunze kusema hapana. Jifunze kusema hapana.

Hii itakusaidia kupunguza mambo usipenda kufanya ila unafanya kwa ajili ya fulani au kuonekana na wewe umefanya kwenye jamii. Maana msingi wa matumizi huko hapa

Wekeza pesa zalisha pesa.
 
Habari wana JF
Naomba Ushauri, Mimi ni Muhanga wa Kutokukaa na Pesa,ama nikipata pesa zinaisha bila kufanya kitu cha maana au kitu cha kuonekana.

Nimejitahidi saana Kuweka bajeti ya Mwezi nakuifata lakini nashindwa, najitahidi kuweka kumbukumbu ya matumizi yote
Mimi chuma ulete ya pesa yangu ni ndugu na jamaa. Nadhan 80% ya mapato yangu huishia kwao. Kila mara uwa nasema ntaanza komaa lakini nashindwa. Mwaka huu nimejiwekea ultimatum kuwa mwisho kabisa ni september 🤣
 
Jifunze kusema hapana. Jifunze kusema hapana. Jifunze kusema hapana.

Hii itakusaidia kupunguza mambo usipenda kufanya ila unafanya kwa ajili ya fulani au kuonekana na wewe umefanya kwenye jamii. Maana msingi wa matumizi huko hapa

Wekeza pesa zalisha pesa.
Aanze kwanza na kusave hela. Ajifunze kuweka akiba. Ukikimbilia biashara wakati hata akiba hujajifunza kuweka, utaambulia patupu. Ndio msingi wa biashara since time imemmorial! Biashara zilianza baada ya binadamu kuweka akiba hadi kuwa na ziada.

Hata katika monetary economy, uwe na 1. akiba kwanza 2. Anza biashara 3. Kopa kukuza mtaji 4. Hapa kazi tu na kazi iendelee ya biashara zitamalaki.

Maisha ni sayansi. Lazima uishi kwa kanuni ile waswahili huita kuishi kwa mahesabu.
 
Mimi ndiyo nadondosha sijui ila nimeshafanyia tafiti nikiwa nina hela kuanzia laki ni lazima nidondeshe 30000 au 20000 au hata 10000 yani kuna some missing money gone without noticing mpaka nikae sana nijuulize nilikua na pesa hii mbona sioniii hivyo yani
 
Rekodi matumizi yako

Punguza matumizi ya siyo ya lazima

Acha kuishi maisha ya kufake yaani kujifanyankama unazo

Jichanganye na watu maskini kama Mimi ili ujifunze kutumia pesa kiubahili

Kwa maelezo zaidi njoo pm
Huwezi kujifanya unazo na ukazitumia,, huyu jamaa hafake kwani pesa ipo

Hapa aachane na matumizi yasiyo lazima
 
Mimi chuma ulete ya pesa yangu ni ndugu na jamaa. Nadhan 80% ya mapato yangu huishia kwao. Kila mara uwa nasema ntaanza komaa lakini nashindwa. Mwaka huu nimejiwekea ultimatum kuwa mwisho kabisa ni september
Kumbe hili ni gonjwa la wengi,pole sana mkuu,halafu wakishajua wewe ni mtoaji wanapeana taarifa tu nenda kwa fulani atakupa.
 
Back
Top Bottom