Ushauri: Ndugu wamemgeuza mama yangu kama mgodi

Ushauri: Ndugu wamemgeuza mama yangu kama mgodi

Status
Not open for further replies.

mysara2011

Member
Joined
Sep 28, 2017
Posts
69
Reaction score
84
Inshort na mama yangu ambaye kwa bahati mbaya ulitokea mtafaruku wakatengana na baba miezi mitatu iliyopita .

Shida sasa niliyonayo mama yangu wakati anaishi na baba alikuwa amefanikiwa kujenga kibanda chake cha kuishi maeneo ya mbagala lakini kwa vile tulikuwa na nyumba yetu ilibidi mama amkabidhi mama yetu mdogo ile nyumba aishi na kwa sasa ni karibu miaka kumi na nne tangu aanze kukaa huko lakini tangu ameanza kukaa huko hawajawahi kumshukuru hata senti .

Sasa kutokana na utengano nyumbani mama ilibidi aondoke nyumbani akaenda kujihifadhi kwa ndugu yetu ili atafute namna ya kuishi lakini cha ajabu hawa ndugu zangu wala hawastuki kuwa mwenye nyumba now ana matatizo tumrudishie nyumba yake au tumpe hata chumba kimoja aishi wao kwao hilo ni no.

Na mamangu alikuwa anataka akapange na ni mtu ambaye yupo age ya 50's. Sasa kubwa zaidi hii juzijuzi mama alinunua usafiri wake lakini cha ajabu kuna uncle wetu kajimilikisha basi hilo si shida sana but anachonikwaza ni daily anataka mafuta ya gari karibu elfu thelathini

Kiukweli nawapenda sana ndugu zangu but kwa hili naona linataka kunipa shinda cause wamemgeuza mama yangu kama mgodi na shida alonayo mamangu ni mpole mno cause majukumu ya kumlea bibi yetu ndugu zake wamembwagia na kuna ndugu zangu watatu wazazi wao walishafariki wote wamemuachia mama lakini hawa si tatizo cause ni yatima

Nahitaji msaada how can I deal na hawa wengine kiukweli nahisi uchungu mno moyoni na kuwaambia nashindwa.
 
huna kaka yako awaambie... wanawake waoga sana kiukweli ndio maana hata mkiachiwa kampuni mume wenu akifariki.. na kampuni zinakufa
 
huna kaka yako awaambie... wanawake waoga sana kiukweli ndio maana hata mkiachiwa kampuni mume wenu akifariki.. na kampuni zinakufa
Kaka tunaye lakini ni mdogo mno ndo kwanza yupo standard 5.
 
Kaka tunaye lakini ni mdogo mno ndo kwanza yupo standard 5.

kuhusu kukaa na ndugu zake sio ishu.. ila huyo anaeendesha gari na kutaka apewe mafuta elfu 30 kila siku.. ni trip za wapi.. na je anamwendesha mama akiwa na mizunguko yake au anajiendesha mwenyewe...
 
"Ndugu lawama wamejaa daresalamaa" hii nyimbo waliimba twangapepeta ee!? Ickilize huenda ikakusaidia pia..

Mpambano mwema maana hapo unaeza hata kulogwa waz waz
 
Kuwa jasir uwaeleze kuwa yule ni ndugu yao ila wanavyofanya sio vzr kwani bimkubwa hvyo vtu anataka vimsaidie
 
Unashindwa kutetea mali za mama yako kisa nini? Au mnataka msionekane wabaya kwa ndugu zenu!? Kwanini uogope kupigania jasho la mzazi wako!?

Amka, tetea mali za mama yako! Upole wa mama yako jumlisha na wewe ndio utakua umaskini wenu..
 
Kuhusu kuwa nazo zangu ninazo na hata ndugu zangu wanatambua hilo kuwa simtegemei mama yangu kwa chochote .
Sasa huo mbanano mama akakae mara kwenye single room kwanini usimchukue ukae nae kwako?
 
Kama mama yako kashindwa be strong for her acheni upole ulioptiliza uo ni uboya usiogope eti mkiwachana watawasema binadam hawana jema tena ukute mnavyowakalia kimya ndo wanawasema zaid bora lawama kuliko fedheha usiogope kusemwa be strong watawaheshim
 
Simama kama binti shupavu,hao ndugu waliokaa miaka yote hiyo bure waambie imetosha, mama amewasaidia kwa kiasi kikubwa sana, wakichukia ni ukosefu wa shukrani, kwa huyo anko wako mwehu, chukua funguo na umwambie chombo kipo katika usimamizi wako,atafute shughuri ya kufanya....
 
Umenikumbusha....kuna jamaa aliomba awe mlinzi wa kibanda changu ( awe anakaa humo bure)..nikamruhusu alikaa miaka takribani saba,niliporaka kuhamia nilimpa miezi mitatu ya kujiandaa!..miezi hiyo ikaisha eti hajapata chumba nimuongezee muda wa kutafuta....pumbavu nilimtimua fasta....
 
Simama kama binti shupavu,hao ndugu waliokaa miaka yote hiyo bure waambie imetosha, mama amewasaidia kwa kiasi kikubwa sana, wakichukia ni ukosefu wa shukrani, kwa huyo anko wako mwehu, chukua funguo na umwambie chombo kipo katika usimamizi wako,atafute shughuri ya kufanya....
Ahsante kwa ushauri wako nitajaribu kufanya hili ili nimuokoe mama yangu katika adha hii
 
Amuambie anahitaji gari alitumie,wema usizidi uwezo.Awaambie ametengana na babaako anahitaji nyumba yake period.
 
Yaani kwa jinsi aya maisha yalivyo kivuruge ningekuwa nishawaambia siwezi kuweka vitu moyoni hata kidogo....nakuambia tu ukimaind fresh nakupunguza kimyakimya.......kuna vitu ukivitoa/ukivipunguza moyoni hata Mungu anakubariki.....
Kweli mkuu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom