Ushauri: Ndugu wamemgeuza mama yangu kama mgodi

Ushauri: Ndugu wamemgeuza mama yangu kama mgodi

Status
Not open for further replies.
kuhusu kukaa na ndugu zake sio ishu.. ila huyo anaeendesha gari na kutaka apewe mafuta elfu 30 kila siku.. ni trip za wapi.. na je anamwendesha mama akiwa na mizunguko yake au anajiendesha mwenyewe...
Atleast angekuwa anamuendesha mama ingekuwa sawa mda mwingi yupo nalo kwenye mizunguko yake
 
Kuhusu kuwa nazo zangu ninazo na hata ndugu zangu wanatambua hilo kuwa simtegemei mama yangu kwa chochote .
Mpotezee hawakosekanagi hawa viwavi jeshi wenye kejeli i can feel ur self pain nimegundua unahofia kutengwa na ndugu endapo ukiwaambia hali halisi but u must wear the strong heart and go to fight nothing comes without a battle
 
Ahsante ndugu yangu
 
Dah pole sn...Nmewaza apo ningekua Mimi...Nyumba ile ningeenda kuwapa ujumbe tu kua kufikia mwakan kila mtu awe ameshahama...na uyo anayedandia magari nadhan angekua ameshanichukia.....hii ishu imefanya sn nigombane na ndugu...mm sinaga cha kuremba
 
Dah majanga ila komaa vaa sura ya fisi wachane tu. Angalia lakini kama ndugu zenu wana asili ya kupenda shirki utakuwa umeamsha vita kubwa sana itayoweza kusababisha madhara ya visasi.
Kama ukoo wenu ni wa watu smart then ongea tu kila mtu apambane na hali yake. Unayoyaona huyafurahii yaseme tu msaidie bi.mkubwa!
 
Unawezaje kuleta Uzi huu kwenye kundi kubwa LA watu ushindwe kuwaambia ndugu wachache wanaoweza kumsababishia mama presha jitathimin unao uwezo wa kuwaambia na wakakuelewa
 
Mwambie mama awaite mbele yako na awaeleze ukweli kwamba sasa hivi hana mume hivyo anahitaji nyumba yake, hadi January wawe wamemwachia nyumba, pia gari irudi nyumbani kwa vile hana pesa tena ya kila siku ya mafuta, nakuhakikishia wa gari ataliacha, na nyumba kwa hasira hawafiki January watahama Ila watanuna kidogo baada ya muda wataanza kujisogeza kwa mama mmoja baada ya mwingine, sio apewe chumba waondoke kabisa maana wataanza kumkera kwenye nyumba yake
 
Imeandikwa Mali ikiongezeka na walaji huongezeka kifupi ni kuwa mungu anapitisha riziki za hao ndugu kwa mama huyo wakiondoka huenda hata mipango ya mama ikawa mingi inakwama kwa kuwa walaji watakuwa wamepungua tahadhari kabla ya kutenda
 
Ahsante kwa ushauri wako
 
Upuuzi wa ndugu nishaukataa kabisa, yani nimepiga marufuku hayo mambo hata me walitaka kumfanya bi mkubwa mgodi, na kuna watu wanakaa kwenye nyumba yake bure miaka zaidi ya 15 nimewambia mwakani wanaanza kulipa kodi unless otherwise walale mbele. Bora kuwa mwenyekiti wa kamati ya roho mbaya kuliko kulea ndugu wasio na shukurani.
 
Ningekuwa mm ni mpenzi wako, au rafiki yako wa karibu sana zaidi ya ndugu yako hilo jukumu ningekuomba kwa mikono miwili uliniachie nilimalize kibabe...

Hao wapuuzi wote ningelala nao mbele wote Perpendicular..... Hata baba yako angeleta upuuzi wakati nasafisha huo uozo akiingilia kati nalala nae mbele...

Mm usoni ni mpole ila na rohoooo mbayaaaaaa.....

Ningeanza na huyo mpuuzi wa gari then nadeal na hao wa nyumba kuendekeza sana ndugu ni sawa na kumlipa fundi hela kabla hajakamilisha kazi....
 
Pole sana aisee! Ushauri wa watu wote Jitahidi uufanyie kazi! Mama anahangaika na vitu vyake mwenyewe! Ushauri wangu kama unajitegemea;
1. Mchukue Mama kaa naye kwa muda, hapo ni rahisi kuchukua gari pia lake.
2. Mwambie Mama mdogo unataka nyumba ya Mama ili kwamba sasa hali ya kodi ya nyumba imekuwa kubwa ili sasa awapatie hiyo nyumba!
Kumuacha kuhangaika wakati anavyake ni kumuacha anyanyasike, maana mtu anasaidia na chake, sasa yy anahangaika wakati vitu vipo anavyoo?! Hakuna namna ambavyo utaacha kuchukiwa Ila ukichukiwa kwa haki furahi maana hata Mungu anakupenda, kuliko kuishi kwa manunguniko
 
Ahsante ndugu yangu kwa ushauri wako nimejaribu kukaa na mama na kumuelewesha kiasi naanza kuona matokeo I hope mda si mrefu mambo yatakuwa sawa bila kuleta mtafaruku wala uhasama na ndugu zangu
 
Aisee,mi pasingekalika kiukweli.unaomba na ushauri mkuu...kumbuka ni MAMA huyo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom