Ushauri: Nawaza kuuza kiwanja nifanye biashara baada ya kufukuzwa kazi. Nina familia inayonitegemea

Hiki ulichoandika hakitabadili uhalisia wa kile nilichoandika
Ni lazima uwe mtu wa kufikiri zaidi ya kufikiri...nimemwambia kama HAJAWAHI kufanya biashara kuuza kiwanja chake
Biashara ni taaluma yenye abc zake
Kuna aina ya biashara
Kuna eneo sahihi la biashara
Kuna mtaji
Kuna malighafi
Kuna matumizi
Kuna wateja
Kuna faida
Kuna hasara
Usijifanye motivational speaker ukamuingiza chaka mwenzako...kumbuka alichonacho ni kiwanja tuu ...biashara zikifeli kiwanja amekiuza unadhani atapata maumivu mara ngapi?
 

Yani point nyingi ulizozisema hapa ndivyo nilivyofanya baada ya kukosa kazi miaka miwil, nilipokua kazini nilinunua kiwanja nikawa na biashara ndogo ndo ikanisaidia kupata kwangu ili niondokane na msongo wa mawazo ya kodi na sehem za kuanika nguo.

Budget ya mboga ilikua wik moja ya mwanzo tu, maana kabla ya kuhamia nilinunua mbegu za kila aina ya mboga nikaweka bonge la bustani, uzuri pia mamlaka ya maji walishaniwekea maji nilipoanza harakati za ujenzi. So mboga sikuwahi kununua hadi nilipo stablelize uchumi wangu pia nikawa nauzia na majirani. Hivi vitu vinatesa sana.
 
Umenena vizuri. Hebu haraka haraka fasta tuambie kijana wetu afanyeje? Usiniambie auze genge maana nayo Ni biashara. Usiniambie akabebe zege au arudi shamba kwa Kijiji.
 


Pole noel oga kiwanja chako kiko wapi? mazingira ya kiwanja yakoje??

Kama una kitu kingine nje ya hicho kiwanja kama pikipiki au gari usiuze kiwanja vitumie kukuingizia chochote kitu

Kama una uwezo wa kukitumia hicho kiwanja kukuingizia walau elfu10 usikiuze. Hapa usome mahitaji ya kiliko kiwanja... ukute kiwanja kipo karibu na barabara, au sehemu unayoweza toa huduma flani tafuta m bia ufanye nae biashara mtaji wako uwe ni eneo lako

Wazo la kuuza hicho kiwanja unaweza kuwa nalo lakini ukakosa mteja au ukauza kwa bei ya hasara kuliko uliyonunulia na mteja unaweza mpata mwakani
 
Kuuza kiwanja zama hizi si mchezo.

Nimeanza kuuza Changu 2018. Mpaka leo hii sijapata mnunuzi. Anyway itategemea kilipo.
Acha kumkatisha tamaa, kila mtu na bahati yake, inategemea na eneo kiwanja kilipo, bei unayouza, madalali n.k
 
Kama hujawahi kufanya biashara usijaribu hilo jambo utaishia kufilisika na majuto mara 2
Nakazia hapa.
Yaani ni bora hata ukagonge mawe upate 5000 kila siku ulishe watoto kuliko kuuza asset kwa kutegemea utaanzisha biashara kubadilisha maisha.
Biashara si kitu cha kufanya kwa vile umefukuzwa kazi inahitaji uzoefu na maandalizi ya muda mrefu.
 
Hili pia ni wazo zuri. Maana biashara ya kufuga nyumbani haina usumbufu wa mambo ya kulipa kodi.
 
Kaombe kazi za chapu chapu sehemu kama ukuli, kumenya chipsi, deiwaka saloon, kusaidia fundi ujenzi, deiwaka boda boda au bajaji, nenda minadani muuzie mtu vitu vyake kama mitumba, vyombo, mazao halafu kamisheni atakulipa huku unaweka akili yako sawa.

Usiuze kiwanja, anza kujengea mabati kama mdau alivyo sema hapo.

Adui yako mkubwa ni status quo, ngoja nikwambie ukweli sisi binadamu tulikuja uchi na tutaondoka bila chochote, usijionee aibu uko uchi tayari usiangalie kushoto wala kulia pambana kianaume, acha wakuseme wala hutomeguka.
 
Ila jamaa kasema hana akiba hata punje
 
Hapana maisha ya hivi ni kitesa familia
 
ungeuza hiyo simu , hela kidogo utakayopata mwannzishie wife biashara ndogondogo kama vitumbua, maandazi ,samaki nk...ili mpate hela ya kula....halafu wewe angalia kama unaweza kukopea kiwanja then angalia mahiitaji ya hapo mlipo ufanye biashara
 
Kama hujawahi kufanya biashara usijaribu hilo jambo utaishia kufilisika na majuto mara 2
Aaah! Mkuu usimkatishe tamaa nadhani anatakiwa awekeze nusu ya mtaji ikitokea mambo yakaharibika ile nusu ingine itamsaidia lakini pia atakuwa amepata uzoefu huwezi Fanya biashara kwa Mara ya kwanza bila kupata hasara.
 
Chemsha mayai weka kwenye trey sambaza sehemu zenye msongamano au beach uko, yai moja la kisasa 400, trey jumala elfu 8000.

Beba trey 5, kuna mwamba mmoja anajaza kindoo kidogo mayai anatembeza usiku kwa usiku tuu anauza mbili kwa siku.
 
Mkuu, pole sana naweza kufeel hali unayopitia, mim natoa ushauri kwa kufikiria kuwa unaishi mkoa wa Dar es salaam na familia yako. Ijapokuwa hujaweka wazi kama mkeo anafanya kazi au la lakin mim nashauri yafuatayo kama unaweza kuendesha pikipiki hapa mjini chukua hati yako ya kiwanja nenda kwa ndugu, jamaa, rafiki yoyote ambaye unaamini anaweza kukuamini mueleze hali halisi, halafu muombe akupe hela ya kutosha kununua boda boda tu na muachie hiyo hati, nunua pikpik anza kupiga kazi bila kujali cheti chako wala status yako.

Baada ya mwezi mmoja naamini unaweza kuwa na mtaji wa kutosha kumfungulia mama biashara yoyote iwe ya mihogo, uji wa mchele, chai au samaki na vichipsi kiaina baada ya hapa naamini familia itakuwa na uhakika wa kula na kutuliza akili, fanya kazi kwa umakini na uaminifu mkubwa unaweza kujikuta unashukuru kwa kufukuzwa kazi baada ya hapo jipange kulipa deni halafu baadae Mungu akifungua njia ukapata kazi maisha yatandelea au pikipik inaweza kukupeleka ngazi nyingine.

CC : Mshana : biashara ni ngumu kuliko kufanya kazi ya kuajiriwa hivyo usikimbilia kuuza kiwanja ukiamini ni suluhisho la tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…