Ushauri, nataka nitoke nje ya tanzania ki utafutaji, ni nchi gani naweza kwenda ki utafutaji?

Wakuu habarini za leo?

Nikiwa kama muumini ninae amini maisha ni popote, Leo nimeleta Uzi huu nikiwa na lengo la kupata mwongozo kwa walio nitangulia kutoka nje ya Tanzania au walio na uzoefu wa nchi zingine barani Africa au nje ya Africa.

Kwanza kutoka nje ya Tanzania kwenda ku-make life abroad ni ndoto yangu tangu nikiwa mtoto na kwasasa naona umri wa kuiishi ndoto yangu ni Sasa.

Hivyo basi naombeni mwongozo ni nchi gani ambayo unaweza nishauri kwenda kwa ajili ya utafutaji wa maisha kulingana na fursa za nchi husika? Pamoja na mwongozo wa kufika huko.

Mimi kama Mimi nchi ambazo nimekua nikiwaza kwenda nchi ambazo ni visiwa kama sheli sheli (Seychelles) Mauritius n.k
-kwa south Africa sipapi kipaumbele Sana may be Botswana na kwingine.

Kwa wale mtakao shauri kua Tanzania kuna fursa nyingi kuliko nje sikatai ni kweli zipo ila kama una mchongo nipatie nipige, kama na wewe una fursa za mdomoni bas naomba utulie.
NDUGU FANYA UTARATIBU FURSA ZIPO SOUTH SUDAN,
 
Towa muongozo huko south Sudan kuna fursa gani?
UPELEKAJI WA VYAKULA ( MAZAO) Sudani ya Kusini ndio kwanza wanaanza kuijenga nchi yao, wanachangamoto nyingi, sisi tunaweza kuwasaidia kwa maana ya kuwekeza na kwa kufanya biashara. Kwa mfano wale wanakula sana chapati, hawana ngano, tunaweza kuwauzia ngano, wanahitaji mafuta ya kupikia tunayo alizeti, wanahitaji vifaa vya ujenzi, tuna viwanda vya saruji na nondo pia, kwa kweli fursa zipo tunachotakiwa ni kujipanga.

Biashara ya hoteli badala ya kujenga vihoteli vidogo kariakoo
kwanini kama una mtaji usiende kujenga JUBA?au GOMA na kwingineko
 
Mh sawa sawa boss wenye mitaji wataenda.
 
Back
Top Bottom