Ushauri, nataka nitoke nje ya tanzania ki utafutaji, ni nchi gani naweza kwenda ki utafutaji?

Mangole Valles Michael

Senior Member
May 30, 2021
101
250
Wakuu habarini za leo?

Nikiwa kama muumini ninae amini maisha ni popote, Leo nimeleta Uzi huu nikiwa na lengo la kupata mwongozo kwa walio nitangulia kutoka nje ya Tanzania au walio na uzoefu wa nchi zingine barani Africa au nje ya Africa.

Kwanza kutoka nje ya Tanzania kwenda ku-make life abroad ni ndoto yangu tangu nikiwa mtoto na kwasasa naona umri wa kuiishi ndoto yangu ni Sasa.

Hivyo basi naombeni mwongozo ni nchi gani ambayo unaweza nishauri kwenda kwa ajili ya utafutaji wa maisha kulingana na fursa za nchi husika? Pamoja na mwongozo wa kufika huko.

Mimi kama Mimi nchi ambazo nimekua nikiwaza kwenda nchi ambazo ni visiwa kama sheli sheli (Seychelles) Mauritius n.k
-kwa south Africa sipapi kipaumbele Sana may be Botswana na kwingine.

Kwa wale mtakao shauri kua Tanzania kuna fursa nyingi kuliko nje sikatai ni kweli zipo ila kama una mchongo nipatie nipige, kama na wewe una fursa za mdomoni bas naomba utulie.
 
John makonda

Member
Mar 13, 2021
62
125
Kama yamekushinda Tanzania nikushauri Kama uko mjini Rudi Kijiji I ukiwa uko KijijiRudi porini kabisa vya burebure vipo tz pekee jaribu uje uwahadithie na wadogo zako
Maisha Sio lelemama
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
43,378
2,000
Unataka kwenda kufanya nini?
Kutafuta kazi?Kazi gani?
Biashara? Ipi?..

Umri wako?
Una mtaji?Kiasi gani?
 
Doha City

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
15,640
2,000
Duh watu mna maneno eti Kama yamekishinda hapa mbele utapaweza..? Mkuu Mimi nakushauri usiache ulichotaka maishani. Wewe pambania kombe tu maisha popote usiwire Wala Nini.
 
Tychob

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
2,274
2,000
Mkuu pambania unacho amini . Usisikilize stori za sisi wengine tunaojidai tunajua saaana kumbe waoga wa kutupwa.
 
Tango73

JF-Expert Member
Dec 14, 2008
1,753
2,000
Hongera sana mpiganaji mwenzangu. kwanza imarisha lugha ya kiingereza ili uwasiliane vizuri huko uendako. Tafuta nchi za ulaya, Israel na marekani tuu ili ufanikiwe .

Usithubutu kwenda kokote Africa, asia wala latin america.Asia wamebanana sana mijini wala hata mahali pa kuuzia magazeti hupaoni. Latin america crime ipo juu sana kwa sababu ya madawa ya kulevya.

Africa ndio kuna ushirikina sana sana waganga wa kienyeji ni matajiri kuliko wafanya biashara. Good luck!
 
SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
3,532
2,000
Subiri Corona iishe ili kupunguza usumbufu. Pia chanjo ikija usisite kuchomwa hiyo nayo itakupunguzia usumbufu huko duniani!.
 
Mangole Valles Michael

Senior Member
May 30, 2021
101
250
Kama yamekushinda Tanzania nikushauri Kama uko mjini Rudi Kijiji I ukiwa uko KijijiRudi porini kabisa vya burebure vipo tz pekee jaribu uje uwahadithie na wadogo zako
Maisha Sio lelemama
Nirudie kijijini au porini kufanya nini wakati nimesema ni wakati wa kuiishi ndoto yangu?

Kwani ni vibaya kupambana ndoto yangu ya kuishi nje ya Tanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mangole Valles Michael

Senior Member
May 30, 2021
101
250
Hongera sana mpiganaji mwenzangu. kwanza imarisha lugha ya kiingereza ili uwasiliane vizuri huko uendako. Tafuta nchi za ulaya, Israel na marekani tuu ili ufanikiwe .

Usithubutu kwenda kokote Africa, asia wala latin america.Asia wamebanana sana mijini wala hata mahali pa kuuzia magazeti hupaoni. Latin america crime ipo juu sana kwa sababu ya madawa ya kulevya.

Africa ndio kuna ushirikina sana sana waganga wa kienyeji ni matajiri kuliko wafanya biashara. Good luck!
Asante Sana mkuu kwa ushauri wenye nguvu kuna vitu nazidi kujifunza naiman nitatimiza ndoto yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom