Ushauri: Nataka kusoma masters nyingine tofauti na ya education, nisome ipi?

Mwakamele 16

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
1,493
1,108
Ndugu zangu wana body, poleni kwa mihangaiko katika kujenga nchi yetu ya Tanzania. Mimi nina degree ya elimu(Bachelor of Education Languages) na kwa sasa ni Mwalimu, natamani kusoma masters lakini ya fani nyingine tofauti na Education na kwa nature ya kazi zetu sina option ya kusoma chuo kikuu kingine chochote hapa nchini tofauti na OUT. Kaka zangu, dada zangu , baba na mama zangu pamoja na ndugu zangu wote humu naomba kwa anayejua masters ambayo at least ipo marketable anishauri. Binafsi nilitamani sana ningesoma Public Administration lakini OUT hawana hiyo masters program, nimeona wana Masters ya Governance and Leadership kama substitute ya hiyo. Nimeshindwa kuamua kuchukua hiyo maana sijui marketability yake.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu kwa ushauri mzuri mtakaonipa.
Mungu awabariki sana!!!!
 
Pole ndugu nimefungua uzi huu nikitegemea kupata ushauri uliopewa, kumbe hukupata Jibu! Bongo haya mambo siyo kipaumbele chetu. Uliza kesho Gwajima ataongelea nini utashangaa ushirikiano.
 
Kwani unataka usome ili ujiajiri au unataka usome ili uajiriwe? Na kama ni kuajiriwa unataka usome ili ukistaafu uweze kujiajiri au ukistaafu upumzike moja kwa moja?
 
Hapo n vyema kufahamu malengo yako katika ajira.Kama unataka uajiliwe na serikali yaan uendelee na ualimu,uajiliwe na private sector au ujiajir mwenyewe
 
kaka wekeza hiyo hela.. usipoteze kuilipa ada.. ajira zinazidi kuyoyoma dunia nzima
 
Kwa ushauri wangu uko nje kidogo ya hii ikiwezekana tafuta sehemu ya kuwekeza hizo fedha .

Hakuna fedha inayoongezeka kwa MA yako utakayosoma ,kodisha hata mashamba Lima .
 
Back
Top Bottom