Ushauri: Nataka kumfungulia biashara ya Salon

MR LINKO

JF-Expert Member
Aug 20, 2016
3,034
3,481
Habari wana jukwaa wa jamii forums

Niende kwenye mada moja kwa moja nina idea ya kumfungulia dogo salon, nina maana salon ya kiume simple tu wala sio ya gharama. Namchukulia vitu vya kawaida tu kama mashine za kunyolea mbili na vitu vidogo vidogo, kiti ataanza nacho kimoja na kochi la wateja wa kusubiria na subwoofer kwa ajili ya mziki.
Nia yangu ya kwanza ni moja kuliko zote nije ni mkabidhi iwe yake ila sita mwambia kwa sasa, maana nilimpa wazo akakubali kwa aslimia zote 100% japo hajui kunyoa hata kidogo mfano kipara, na mitindo mingine hata kushika mashine hajawaii.

Ila nimemlipia mahali anze kujifunza kwa mtu kwa vichwa vya wanafunzi wa msingi maana najua akiwakosea hawezi pigwa ngumi.

PLAN YANGU IKO HIVI:
Nikimfungulia nitampa masharti kuwa nataka niwe naona hesabu kamili kwa week hii najua miezi miwilii ya kwanza itakuwa mi ngumu ila sio kesi.

Asiwe mzembe asababishe vitu kuibiwa na Salon sio kijiwe ni sehemu ya biashara maana najua kwakikaa masela sana itakuwa kuna changamoto kwa baadhi ya wateja.(Hii ina maana wanaweza kaa watu wa 4 ndani mtu anataka kunyoa akajua kuwa kuna foleni)

Baada ya yote hayo nikijua kuna mafanikio kwenye upande wa salon basi sitakuwa nakuja tena kumuuliza kuhusu hesabu na nitamuachi salon kisha asiinijue kabisa na kuhusu kodi, kula na pesa za pango ajilipie mwenyewe kifupi aishi maisha yake.

MASWALI YANGU NI HAYA KAMA UKIJIBU KWA UFASAHA NITAFURAHI SANA:

1: Je biashara ya salon ina lipa au huwa ni kawaida tu kwa ajili ya kusukuma maisha?

2: Changamoto za salon tukiachana na wateja?(kipikina tia hasara sana au ni kuwa nacho makini)

3:Je kwa salon ya chini kabisa lazima nikakate leseni TRA maana ni simple tu.

4: Kama mtu yuko serious kwa kiwango cha chini cha kuingiza kwa siku inaweza kuwa kiasi gani hii tuchukulie kwa location ya kawaida. (maana kuna utafiti nimefanya kuna jamaa kaniambia kwa siku inaweza kuwa hadi 5000-8000)

5:Vifaa muhimu kabisa kwa salon ya kawaida maana nimepanga kuweka kijijini huko nje kidogo na mjini sehemu ambayo kuna wanafunzi wa msingi.(maana huko najua jero jero na buku ni nyingi sana)

6: Biashara gani nyingine naweza ongeza kuweza kuongeza mahitaji ya kipato kuepuka kusubiria salon pekee hapa nina maana hapo hapo kwenye frame moja.

NB: Bei ya frame nimepata mahali ni 50 elfu kwa mwezi na ndo sehemu karibu na shule ya msingi na pia kuna saloon kama mbili sema sio karibu sana na mimi na nilipo hakuna salon hata moja.

WAZO LANGU: Nilikuwa nataka niweke na PS 2 kwa ajili ya kuwavuta hawa watoto wa msingi mfano akinyoa ana cheza bure au akiniletea mteja anacheza mechi moja bure na pia kwa mechi kawaida itakuwa ni 200 kama hivyo tu. (kumbuka hapa nitazingatia wanao cheza tu na sio kuwa watajazana)

Kuweka movie ila hii ni ngumu maana itashindikana maana dogo sio mtu wa movie za kutafsiriwa yeye ni HD na za kihindi sijuii kifilipino hizo hayupoo kabisa.

Kama unawazo niongeze nitashukuru.
 
Hata kipara kama hiki hajui mkuu...
Tafuta mtu wa maana amfundishe dogo vizuri ujenge jina kwanza aisee.
FB_IMG_1659252578420.jpg
 
Wazo la kuweka ps nakuunga mkono mtawavuta watoto na watapenda kuja kunyoa ila wasiwasi wangu ni huyo dogo kupunyua watoto wa watu..mwambie azingatie sana namba za mashine kuwanyoa watoto na asikimbilie kuwanyoa mitindo itamsaidia zaidi kuongeza ujuzi siku hadi siku..na pia wanafunzi style yao ni lowcut au fresh ya unga wengi wanaijua hivyo asiogope atajua tu na utakuja kushangaa.
 
Kwanza kabisa biashara yeyote inalipa as long as mhusika atakuwa na nidhamu na biashara pamoja na kuwa na hulka ya kujiongeza kuikuza biashara. Kama dogo atakuwa serious itafanya vizuri.
Pili suala la PS2 lina faida na changamoto zake. Faida ni nyingi kwa sababu ya hulka ya watoto kupenda games ila changamoto huja pale itakapotokea games kuwaelemea watoto au kuchochea udokozi wa hela majumbani kuja kuchezea games. Hivyo inabidi nidhamu ya kuchezesha games iwe ya hali ya juu kwa kuweka muda pamoja na siku maalum za kuchezesha.
Pia ukitaka faida zaidi weka mashine la mchina la kubetia utapiga faida sana
 
Mi sio mtaalamu ila kwa biashara ya saloon fanya mahesabu haya ili uweze mdai hela, tena dai mahesabu ya Siku sio ya Week.

1. Tufanye kodi ni 50 kwa mwezi, kwahiyo kwa siku ni elfu 2

2. Umeme kwa siku ni elfu 5.

3. Maji, ulinzi, usafi wa choo, takataka, kwa mwezi tufanye jumla elfu 30 kwahiyo kwa siku ni Buku 1.

4. Kodi TRA itakua kama 60 hivi kwa mwezi na Manispaa/Halmashauri kama elfu 40 kwahiyo jumla kama 100,000 kwahiyo kwa siku ni elfu 3.5 (makadirio)

5. Gharama za vitu (mashine, viti, ps, tv, etc) sasa kurudisha hela kwa siku elfu 5.

Kwahiyo dogo kwa siku akupe elfu 20 bila kujali hela yake ya kula kutoka saloon, bila kuangalia PS.

Mahitaji ya saloon Tukiacha fremu na mazaga mazaga mengine tuliotaja hapo juu.

1. Mashine nzuri mbili andaa 100-200,000/=

2. Vifaa vidogo vidogo kama vitana, chanuo, vitambaa, mataulo, ndoo, etc andaa kama 100,000/=

3. Kiti cha saloon bei kinoma vinafika hadi Mil 1.5 ila unaweza kuchonga vile vya cheap ata kwa laki 1-2.

4. Usisahau TV hapo uliposema subwoofer.

5. Usimsahau mdada mzuri wa kuosha vichwa vya juu ya shingo kama target ni madogo wa s/msingi tu hii namba 5 skip.

6. Kua na bei elekezi, yaani andika kabisa kunyoa mtoto buku, mtu mzima buku 2, kuna saloon tunaogopa kuingia kwasababu bei elekezi hamna.

vingine wata edit wadau.

Mwisho, kwahiyo dogo muda huu angeanza mdogo mdogo kujifunza kunyoa. Saloon unayoendaga kila siku nenda kamuombee. Ila VETA wana kozi iyo.
 
Habari wana jukwaa wa jamii forums

Niende kwenye mada moja kwa moja nina idea ya kumfungulia dogo salon, nina maana salon ya kiume simple tu wala sio ya gharama. Namchukulia vitu vya kawaida tu kama mashine za kunyolea mbili na vitu vidogo vidogo, kiti ataanza nacho kimoja na kochi la wateja wa kusubiria na subwoofer kwa ajili ya mziki.
Nia yangu ya kwanza ni moja kuliko zote nije ni mkabidhi iwe yake ila sita mwambia kwa sasa, maana nilimpa wazo akakubali kwa aslimia zote 100% japo hajui kunyoa hata kidogo mfano kipara, na mitindo mingine hata kushika mashine hajawaii.

Ila nimemlipia mahali anze kujifunza kwa mtu kwa vichwa vya wanafunzi wa msingi maana najua akiwakosea hawezi pigwa ngumi.

PLAN YANGU IKO HIVI:
Nikimfungulia nitampa masharti kuwa nataka niwe naona hesabu kamili kwa week hii najua miezi miwilii ya kwanza itakuwa mi ngumu ila sio kesi.

Asiwe mzembe asababishe vitu kuibiwa na Salon sio kijiwe ni sehemu ya biashara maana najua kwakikaa masela sana itakuwa kuna changamoto kwa baadhi ya wateja.(Hii ina maana wanaweza kaa watu wa 4 ndani mtu anataka kunyoa akajua kuwa kuna foleni)

Baada ya yote hayo nikijua kuna mafanikio kwenye upande wa salon basi sitakuwa nakuja tena kumuuliza kuhusu hesabu na nitamuachi salon kisha asiinijue kabisa na kuhusu kodi, kula na pesa za pango ajilipie mwenyewe kifupi aishi maisha yake.

MASWALI YANGU NI HAYA KAMA UKIJIBU KWA UFASAHA NITAFURAHI SANA:

1: Je biashara ya salon ina lipa au huwa ni kawaida tu kwa ajili ya kusukuma maisha?

2: Changamoto za salon tukiachana na wateja?(kipikina tia hasara sana au ni kuwa nacho makini)

3:Je kwa salon ya chini kabisa lazima nikakate leseni TRA maana ni simple tu.

4: Kama mtu yuko serious kwa kiwango cha chini cha kuingiza kwa siku inaweza kuwa kiasi gani hii tuchukulie kwa location ya kawaida. (maana kuna utafiti nimefanya kuna jamaa kaniambia kwa siku inaweza kuwa hadi 5000-8000)

5:Vifaa muhimu kabisa kwa salon ya kawaida maana nimepanga kuweka kijijini huko nje kidogo na mjini sehemu ambayo kuna wanafunzi wa msingi.(maana huko najua jero jero na buku ni nyingi sana)

6: Biashara gani nyingine naweza ongeza kuweza kuongeza mahitaji ya kipato kuepuka kusubiria salon pekee hapa nina maana hapo hapo kwenye frame moja.

NB: Bei ya frame nimepata mahali ni 50 elfu kwa mwezi na ndo sehemu karibu na shule ya msingi na pia kuna saloon kama mbili sema sio karibu sana na mimi na nilipo hakuna salon hata moja.

WAZO LANGU: Nilikuwa nataka niweke na PS 2 kwa ajili ya kuwavuta hawa watoto wa msingi mfano akinyoa ana cheza bure au akiniletea mteja anacheza mechi moja bure na pia kwa mechi kawaida itakuwa ni 200 kama hivyo tu. (kumbuka hapa nitazingatia wanao cheza tu na sio kuwa watajazana)

Kuweka movie ila hii ni ngumu maana itashindikana maana dogo sio mtu wa movie za kutafsiriwa yeye ni HD na za kihindi sijuii kifilipino hizo hayupoo kabisa.

Kama unawazo niongeze nitashukuru.
Biashara ya kijinga hiyo futa hilo wazo mara moja.
Bora umfungulie duka la kawaida la mahitaji ya nyumbani.
 
Mi sio mtaalamu ila kwa biashara ya saloon fanya mahesabu haya ili uweze mdai hela, tena dai mahesabu ya Siku sio ya Week.

1. Tufanye kodi ni 50 kwa mwezi, kwahiyo kwa siku ni elfu 2

2. Umeme kwa siku ni elfu 5.

3. Maji, ulinzi, usafi wa choo, takataka, kwa mwezi tufanye jumla elfu 30 kwahiyo kwa siku ni Buku 1.

4. Kodi TRA itakua kama 60 hivi kwa mwezi na Manispaa/Halmashauri kama elfu 40 kwahiyo jumla kama 100,000 kwahiyo kwa siku ni elfu 3.5 (makadirio)

5. Gharama za vitu (mashine, viti, ps, tv, etc) sasa kurudisha hela kwa siku elfu 5.

Kwahiyo dogo kwa siku akupe elfu 20 bila kujali hela yake ya kula kutoka saloon, bila kuangalia PS.

Mahitaji ya saloon Tukiacha fremu na mazaga mazaga mengine tuliotaja hapo juu.

1. Mashine nzuri mbili andaa 100-200,000/=

2. Vifaa vidogo vidogo kama vitana, chanuo, vitambaa, mataulo, ndoo, etc andaa kama 100,000/=

3. Kiti cha saloon bei kinoma vinafika hadi Mil 1.5 ila unaweza kuchonga vile vya cheap ata kwa laki 1-2.

4. Usisahau TV hapo uliposema subwoofer.

5. Usimsahau mdada mzuri wa kuosha vichwa vya juu ya shingo kama target ni madogo wa s/msingi tu hii namba 5 skip.

6. Kua na bei elekezi, yaani andika kabisa kunyoa mtoto buku, mtu mzima buku 2, kuna saloon tunaogopa kuingia kwasababu bei elekezi hamna.

vingine wata edit wadau.

Mwisho, kwahiyo dogo muda huu angeanza mdogo mdogo kujifunza kunyoa. Saloon unayoendaga kila siku nenda kamuombee. Ila VETA wana kozi iyo.
Heheeh kwamb dogo akabidhi elf 20 per day
 
Mchanganuo mzuri sana huu unaingia kwenye kila biashara.
Hapo namba 4 kwenye kodi estimates zake zipo juu sana, kwa hair cutting mapato TRA weka 100,000/= kwa mwaka sawa na 8,333 kwa mwezi na 277.78/= kwa siku, na leseni ya biashara (Halmashauri) salon ni 41,000/= kwa mwaka sawa na 3,416.67/= kwa mwezi na 113.89/= kwa siku.
 
Back
Top Bottom