Ushauri: Nataka kufuga nyoka kwa ajili ya ulinzi

Yaleyale

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
1,789
2,383
WanaJF kichwa cha habari chajieleza.

Watu wengi wamekuwa wakifuga wanyama kama mbwa kwa ajili ya ulizi usiku kuzuia vibaka. Tumekuwa tukiona vibaka wakivamia nyumba za watu na hata kuua hao wanyama kwa sumu au risasi. Binafsi vibaka wamewahi kulizia mara mbili kwa nyakati tifauti. Mara ya kwanza walikwangua kiIST yangu ikabaki nyeupe. Mara ya pili nikiwa safari wakakwangua TV yangu niliyokuwa naipenda kweli. Sasa nimepata wazo la kufuga nyoka tena nyoka hasa kama koboko na kobra kwa ajili ya ulizi wa nyumbani na hata kuwauzia wadau wengine.
Kama tunavyojua hapa JF pana wengi na palipo na wengi pana mengi pia. Naomba kujua kama kuna mdau anajua chuo au sehemu ninayoweza kupata hayo mafunzo ya kuwafunga nyoka na kuwafundisha kutokudhuru mfugani (kama ilivyo kwa mbwa).
Naona kama nikifanikiwa wadau wengi wataachana kuwafuga mbwa ambao ni gharama na sasa kugeukia mnyama nyoka kwa ajili ya ulizi wa makazi yetu.
Uzi tayari
 
Nyoka ana uma pale tu anapohisi unataka kumdhuru, bila hivyo anatulia tuli, kama sio kusepa..
 
Ndiyo maana nataka nipate chuo cha kuwafundisha kulinda. By the way, vibaka hawatoki mbali hivyo kujilikana tu kuwa umefuga hao wadudu kwako hawawezi kuthubutu kuruka ukuta usiku.
 
Sawa, ila sidhani kama wanafundishika viumbe wale, sanasana kuwazoesha kutulia ili uweze kumbeba bila kukudhuru.
 
Fuga mbwa kama German Shepard halafu ufundishe wajibu wake utakuta kawakalisha chini hao vibaka
 
Ukifanikiwa kuwafuga mkuu niambie tupinguluwe urafiki............maana kwa kuusoma tu huu uzi wako ushanigeuza mlinzi wa leo maana sitolala. Hamna mdudu namuogopa kama huyu. :(:(:confused:
 
Hahahaha. Mkuu bado natafuta chuo
 
Nimesoma na kuona umejaa kufatwa na roho ya mauti.. inayokupeleka kuja kufuga vitakavyokutoa uhai wako kabisa.

Embu sali uondoe hiyo roho ya ulimwengu wa giza unaokutawala kwa sasa.
 
WanaJF kichwa cha habari chajieleza.

Watu wengi wamekuwa wakifuga wanyama kama mbwa kwa ajili ya ulizi usiku kuzuia vibaka. Tumekuwa tukiona vibaka wakivamia nyumba za watu na hata kuua hao wanyama kwa sumu au risasi. Binafsi vibaka wamewahi kulizia mara mbili kwa nyakati tifauti. Mara ya kwanza walikwangua kiIST yangu ikabaki nyeupe. Mara ya pili nikiwa safari wakakwangua TV yangu niliyokuwa naipenda kweli. Sasa nimepata wazo la kufuga nyoka tena nyoka hasa kama koboko na kobra kwa ajili ya ulizi wa nyumbani na hata kuwauzia wadau wengine.
Kama tunavyojua hapa JF pana wengi na palipo na wengi pana mengi pia. Naomba kujua kama kuna mdau anajua chuo au sehemu ninayoweza kupata hayo mafunzo ya kuwafunga nyoka na kuwafundisha kutokudhuru mfugani (kama ilivyo kwa mbwa).
Naona kama nikifanikiwa wadau wengi wataachana kuwafuga mbwa ambao ni gharama na sasa kugeukia mnyama nyoka kwa ajili ya ulizi wa makazi yetu.
Uzi tayari
KAZI NDOGOHIYO KUNA BABU YANGU YEYE ANAWEZA KUTENGENEZA NYOKA AU CHUI XIMBA WANA KUA WALINZI WAMALIZAKO ZOTE UNAZO MILIKI HAIJALIXHI IPO WAPI MTU AXIYE MTOTO WAKO AU MKE WAKO HAWEZI CHUKUA LAZIMA ATAKUTANA NAHAO NILIO WATAJA KATI YAO HATAXHAMBANI MTU AKIOKOTA EMBE ATA ONANA NA MNYAMA MOJA WAPO JUU
 
Andika kibao kuzunguka eneo lako,pia kwenye fance,KUNA NYOKA MKALI ENEO HILI,
Mimi kuna watu walikuwa wanakojolea fance yangu.nikamwaga oil kuzunguka fance,na KIBAO KUNA NYOKA WAKALI ENEO HILI Rafiki hakuna MTU anasogea,hata wageni hupiga Simu KWA mbali niwafuate
 
fuga nyoka vibaka wamwage siafu tuone nani mjanja..... MNYAMA PEKEE ANAYEFAA KWA ULINZI NI MBWA NA HAO MBWA BILA MAFUNZO PIA ANDIKA MAUMIVU.
 
Back
Top Bottom