Ushauri naomba

Ngwamba mefani

New Member
Aug 5, 2019
4
0
Nahtaji kufungua karakana ya magar mkoa wowote. Naomba kushauliwa ni mkoa gani ntaweza kuiendesha karakana yangu kwa kipato kizur.
 
Nahtaji kufungua karakana ya magar mkoa wowote. Naomba kushauliwa ni mkoa gani ntaweza kuiendesha karakana yangu kwa kipato kizur.
Karakana mbona unafungua tu mkoa wowote ule mkuu? Kwa sababu kila mkoa kuna watu wana magari, na hivyo ni wazi kabisa kuwa wanahitaji huduma za karakana.
Ila kwa jinsi ulivyouliza swali lako, nachelea kusema kuwa umejiandaa kufeli katika hiyo biashara kwa sababu bado inaonekana hujafanya utafiti wa kutosha kwenye hiyo biashara. Yaanj hata eneo bado hujajua ni eneo gani.
Hiv lets say mtu akakwambia nenda kafungue karakana yako Mwanza. Itakua imekusaidia nini?
Bado unahitaji kufanya utafiti zaidi.

Ushauri wangu:
Chagua mkoa mmoja (wowote ule) ambao utakua rahisi zaidi kwako kufanya biashara (kutokana na connection zako,kujuana na watu huo mkoa,kujua maeneo ya hiyo sehemu, etc). Halafu sasa, lenga karakana moja uende hapo (kama ni fundi inaweza kuwa rahisi zaidi, unaweza kuomba kibarua na kukaa kwa muda ukifanya kazi ili uweze kujua mambo muhimu kuhusu karakana na ufanyaji kazi wake). Kama wewe sio fundi, itakua ngumu zaidi ila sasa ndo itakua muhimu zaidi ujue hivi vitu; Kwa hiyo unaweza kuzoeana na mafundi na kuwa unaspend nao muda kupiga nao story za hapa na pale; Pia unaweza kuongea na wamiliki watatu wanne wa karakana wakupe uzoefu pia....!! Tumia muda wa kutosha kufanya hili. Ukiliruka hili, utakuja kulia mbele ya safari.
Baada ya hapo sasa, tumia muda pia kufanya uchunguzi wa eneo ambalo linaweza kukufaa kuanzisha karakana (inabidi kutembelea haya maeneo, kuzunguka:kupiga story na mafundi, wenye magari,wauza maduka ya spea za magari) ili kuweza kujua ni eneo lipi specifically linaweza kukufaa.
Muda wote huu wa utafiti uwe na diary au daftari lako unaandika mambo muhimu unayoyagundua katika safari yako hiyo ya uchunguzi, ambayo yatakuja kukusaidia sana kwenye kufanya uamuzi.
Pia umeshafikiria utapataje wateja wako? Utaitangaza vipi biashara yako? Utapokeaje mrejesho kutoka kwa wateja wako? Mafundi utakaowaajiri utawapata wapi?
Kodi unazohitajika kulipa ili kusajili, kufungua na kuendesha biashara yako ni zipi na kiasi gani? Kipi cha utofauti kitakachomfanya mteja aje kwenye karakana yako na sio ya kwangu? Je, kuna wadau wenye biashara zingine karibu na itakapokua karakana yako ambazo kwa namna moja au nyingine zinaweza kutegemeana na karakana (duka la spea, car-wash,kituo cha kujaza mafuta) kiasi kwamba mnaweza kushirikiana na kuwa mnaleteana wateja? Mambo yote hayo ni muhimu kuyafikiria.
All the best mkuu.
Ngwamba mefani
 
Back
Top Bottom