USHAURI:Nahitaji kuuza madawa ya binadam

jojoe35

JF-Expert Member
Aug 2, 2014
262
378
Wasalaam wakuu, kama kichwa kinavyojieleza,nina haja yakuanzisha biashara ya kuuza madawa ya binadam( nmefikiria zaidi ile ya kuuza jumla pharmacy) ila ata reja reja wazoefu nisaidieni

Naomba msaada wakuu
1.pharmacy inahitaji mtaji minimum shingap?
2. Mm cna chet cha pharmacy je naweza tumia mtu aliye na chet akafungua? Na huyo mtu ni lazima awe amesomea pharmacy au hata wale waliosomea ile coz fupi yauuzaji madawa?

Msaada wenu wa mawazo wakuu, natanguliza shukrani
 
Ukiweza Pharmacy,unamanisha Duka la Madawa.Vitu mhimu
1)Pitia sheria ya Pharmacy Council ya 2011
2)Nenda Pharmacy Council au Mtafute Mfamasia wa Halmashauri au Jiji unamotaka Kufungua biashara upewe maelekezo ya Eneo linatakiwa liweje.Kwa uchache Duka la Jumla linatakiwa liwe na Eneo la mraba meta 60.
3) Kama itakuwa ni Pharmacy (Tofauti na Duka la Dawa Mhimu kwa Maeneo ya Vijijini) unahitaji Msimamizi wa Biashara Aliyesajiriwa na Baraza la Pharmacy.Yeye utaingia Naye Mkataba.Waliosajiriwa wako wa aina 3:Wenye Shahada,Diploma na Certificate.Kwa kesi ya Pharmacy atapaswa kuwa kwenye shahada,ambaye kitaalam huitwa Mfamasia (Pharmacist).
4)Ujiridhishe vigezo ndiyo baraza Wataluma kibali.
5) Baada ya Kibali Unaweza ukaanza biashara.
6)Ikiwa utapenda Kufanya uagizaji wa dawa itakuwa kuwaona TFDA ili wakupe import permit nk
7)Hapo ndiyo issue ya Mtaji itakuja.
 
Back
Top Bottom