michael G
Member
- Jul 28, 2018
- 31
- 47
Habari za Jumapili. Poleni kwa majukumu na pole kwa Mashabiki wenzangu wa SIMBA ila safarii bado.
Nina mpenzi wangu tupo kwenye mahusiano kwa miaka 5 sasa (2016-2021) ila shida inakuja kwenye Simu yakee, hataki niishike na nikiishika nakuwa natumia nguvu sana, na anasema hataki nimkague ila Simu yangu akija lazma aishike na aikague kila sehemu.
Juzi alikuja wakati yupo nje ananisaidia kufua, niliingia ndani nikashika mkoba wake nikakuta kuna simu ndogo mpya ila hajawahi kuniambia kuwa ana simu ndogo niliiwasha, nikakuta haina laini ila ina sms za mapenz mfano Bby, wife, mke wangu kwa namba 3 tofauti.
Nikaizima nikairudisha kwenye mkoba na sikumwambia kama nimeona simu hiyo ndogo, baada ya muda nikatumia akili binafsi kumuuliza kuhusu sms kwa sababu sikutaka ajue kuwa nimeona simu ndogo, akaniambia kuwa hao watu wanamtongoza tu ila hajawah kulala nao na hana mpango nao.
Nikachukua zile namba alivyoondoka nikazipiga ili nijue ukweli moja ya zile namba ilikua ni namba ya Daktari ambaye wanafanya wote kazi katika hospitali moja hapo Dar, akaniambia hana yeye hana lolote linaloendelea na huyo mpenzi wangu, japo huyu mpenzi wangu alishawahi kunielezea kuhusu huyo Dkt kuwa anamtongoza.
Sasa nawaza kwanini huyu mwanamke alinificha kuhusu hiyo simu ndogo?? Na mpaka leo hajaniambia.
Je hizo chating kwenye simu nizieleweje ni kweli wanamtongoza tu au kuna namnaa hapoo??
Na kwanini hataki nishike simu yake ili hali yangu anashika muda wowote?
NB; Baada ya kumpigia yule Dkt baada ya muda mpenzi wangu alinipigia na kuanza kunilaumu kwanini nimefanya vile na kuanza kunikejeli kuwa najidhalilisha na sijiamini, na kuongezea kuwa kama mimi ni rijali kwanini nafanya vilee??
Na tumepanga kutambulishana mwez wa 8 mwaka huu.
Ingekuwa wewe ungefanyajee?