Ushauri na ombi kwa Wizara ya Ulinzi na Usalama

Ushauri na ombi kwa Wizara ya Ulinzi na Usalama

hiv din nchi hii ni Ukristo na Uislam tu? kwa taarifa yako hayo unayosema hata katika Ukristo wameambiwa wanawake wavae nguo za kujisitir na za heshima. sasa kwa mtizamo wako unafikir wale wanaoamin iman ya vibuyu watavaa nguo gan? shida ya dini yenu ni ubinafs zaid na kujiona ndio inayotakiwa kusikilizwa zaid.
 
Umeleta hoja.Tumeiheshimu hoja yako kwa sababu ni haki yako kutoa mawazo bila kubughudhiwa (kwa mujibu wa katiba yetu)

Lakini hujaeleweka hata kidogo kwa sababu;

"We can't discuss impossible to be possible"

Tusipotoshane hapa!!!
 
kama unalijua hilo vipi sasa wale ambao dini zao hazruhusu wafanye kazi yyte siku yao ya kuabudu,tukimaliza la mavazi kwa waislam tuwatetee na wao wawe wanakuwa off siku hao ya kuabudu!!?yote si ni mambo ya kiimani??
Haiwezi tokea maana hata waislamu hawajalalamika ijumaa iwe siku ya kupumzika na kufanya ibada japo kuwa ijumaa ni siku muhimu sana.
 
Umeleta hoja.Tumeiheshimu hoja yako kwa sababu ni haki yako kutoa mawazo bila kubughudhiwa (kwa mujibu wa katiba yetu)

Lakini hujaeleweka hata kidogo kwa sababu;

"We can't discuss impossible to be possible"

Tusipotoshane hapa!!!
Sawa mheshimiwa.
 
hiv din nchi hii ni Ukristo na Uislam tu? kwa taarifa yako hayo unayosema hata katika Ukristo wameambiwa wanawake wavae nguo za kujisitir na za heshima. sasa kwa mtizamo wako unafikir wale wanaoamin iman ya vibuyu watavaa nguo gan? shida ya dini yenu ni ubinafs zaid na kujiona ndio inayotakiwa kusikilizwa zaid.
Kama na wakristo wameamrishwa hivyo basi tuwe kitu kimoja katika kuomba swala hili,hao Wa vibuyu watasemewa na watu wao kama watavaa mipera ni wao.
 
Kama na wakristo wameamrishwa hivyo basi tuwe kitu kimoja katika kuomba swala hili,hao Wa vibuyu watasemewa na watu wao kama watavaa mipera ni wao.
una mawazo ya kizee mshikaji wangu hii sio nchi ya dini hii ni free state mzee. kama unahic kukwazikika kwa nguo hizo wavaazo hamia somalia.
 
Niite NDUGU sio Mheshimiwa.

Ndugu Cyprian Musiba huwa anapenda aitwe NDUGU SIO MHESHIMIWA.

Namsapoti kwa hilo.

Musiba Cyprian Muraaa tunakusalimia sana, huwa anapiga za uso na hakopeshe wala kupepesa macho kwa sababu data huwa anazo.

Hahahaha!!!

Tusipotoshane!!!!

Sawa mheshimiwa.
 
una mawazo ya kizee mshikaji wangu hii sio nchi ya dini hii ni free state mzee. kama unahic kukwazikika kwa nguo hizo wavaazo hamia somalia.
Sawa,mimi ni mzee kijana wangu.
 
Niite NDUGU sio Mheshimiwa.

Ndugu Cyprian Musiba huwa anapenda aitwe NDUGU SIO MHESHIMIWA.

Namsapoti kwa hilo.

Musiba Cyprian Muraaa tunakusalimia sana, huwa anapiga za uso na hakopeshe wala kupepesa macho kwa sababu data huwa anazo.

Hahahaha!!!

Tusipotoshane!!!!
Sawa,mkurugenzi wa majeshi.
 
Hapana mkuu,kwa nini kusiwepo na haki kwa wafuasi Wa dini zote tukizingatia maamrisho ya dini zao kwa mujibu Wa katiba.
Angalia Siku za mapumziko ya kazi ni siku za kuabudu kwa imani mojawapo kwa nini na hawa wasipate Uhuru wa kujistiri wakiwa kazini.
Japo kuwa ni watu wazima wanachagua kuingia huko lakini si vibaya ombi hili linafanyiwa kazi kuwapa fursa wale wanaoshindwa kuingia huko kwa kuhofia stara.

We ni moja kati ya watu wengi wenye mbongo dhaifu sana, yaani wee karne hii unawaza mambo ya uislamu na ukristu sijui kujistili sijui nn. watu wanawaz kwenda sayari nyingine wewe unawaza mavazi.Kuna jamaa limoja lilikosa ajira miaka flani et kwa kushindwa kufanyiwa vipimo kwa kuvua nguo .Saiv anauza duka la kaka yake mwaka wa saba huu.Haya mambo ya mungu na dini mmeletewa halafu mnajifanya kama vile mlianzisha nyie.
 
Uwe unaelewa jamaa yangu Mimi nimepinga wapi,Mimi NAtoa pendekezo sina chuki yeyote kidini.
Halafu ni bora kubaki na ustaarabu kuliko kudhalilishwa kisa ajira huyo jamaa yuko sahihi kusimamia anachokiamini..nyie imani zenu zinakubali mabaya yote ndio maana hili jambo mnaona kama ni uzamani na chuki zikiwemo dini na maendeleo yoyote ni mama na mtoto.

Kwa taarifa yako MTU au binaadamu Wa kwanza kufanya safari ya anga ni mtume Muhammad s.a.w kabla ya hao wazungu wenu mnaowaabudu na hakutumia mitambo au mamitungi ya gesi kupumulia kama wanavyofanya sasa,hizo safari zenu Leo ni marudio hakuna cha ajabu na hizi hizi mambo za kizamani unapata kujua hayo yote.
 
Unajua wewe ni mjinga, dini haina uhusiano na mavazi wewe.
Hijabu wanavaa wanawake wa maeneo ya Saudi na kwengineno kwa sababu wanawake wa huko wana nywele ndefu, hivyo hijabu ni kwa kulinda manywele yasitawanyike hovyo, wewe na kipilipili chako, nywele ngumu kama brush hijab ya nini kwa wabongo. Ndo maana hata wanaume wa huko huvaa kitu kichwani ili kukinga nywele na upepo kuvuruga nywele na kuziba macho ukikumbuka pia walitumia sana farasi enzi hizo kusafiri, hivyo kuzifunika nywele ni usalama pia.
Hata kuvaa kanzu sio dini bali ni mazingira yao,
Mtu anaenda kukojoa na kwa kuwa kule upepo ni mwingi kujirushia mkojo ni kawaida kama utakojoa huku umesimama, ndo maana mazingira ya mavazi yao yamewekwa ili hata ukitaka kukojoa nje barabarani uchutame kama mwanamke ama sivyo watu wangekuwa wananuka mikojo.
Wengi mnaopenda dini mna sifa kubwa ya kuwa na ujinga mwingi
Asalam aleykum wanajamii.

Moja kwa moja kwenye lengo nchi yetu pendwa ni moja kati ya nchi zinazompa Uhuru RAIA wake kuabudu dini yeyote aipendayo kikatiba.

Leo najikita zaidi kuiomba serikali na wizara husika kuwapa uhuru wa kuabudu watumishi wake.

Hapa nasimama kutoa hoja hii kama itafaa basi ifanyiwe kazi na vyombo husika, watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama, askari polisi, askari wa jeshi la wananchi, jeshi la zima moto, uhamiaji na jeshi la kujenga taifa.

Haya ni majeshi yanayoajiri watu wa dini zote hapa nchini na kuwapa uhuru wao wa kufanya ibada lakini kumekuwa na unyimwaji wa uhuru wa mavazi kwa waumini wa dini ya kiislamu hasa kwa waajiriwa wa kike.

Kwa mujibu wa dini ya kiislamu mwanamke anatakiwa kujistiri mwili wake popote alipo, sasa hapa kwetu mambo ni tofauti kidogo hakuna mavazi au sare katika majeshi yetu yanayompa uhuru mwajiriwa husika wa kike kujistiri.

Hivyo nashauri Wizara husika ziangalie uwezekano wa sare za kujihifadhi kwa hawa dada zetu wa kiislamu wapate angalau uwezekano wa kuficha nywele zao na mavazi yao yawe ya stara hata kama ni suruali basi ziwastiri kwa mujibu wa dini na imani yao.

Tunaweza kuangalia mifano kwa nchi zilizowapa uhuru wanawake wa kiislamu kujistiri wakiwa katika majukumu yao ya kijeshi, kwa kuwa nchi yetu haina dini basi haiwezi kuwa tatizo.

Kuna wakina dada wengi wanatamani kujiunga na majeshi yetu lakini wanaogopa kwenda kinyume na maamrisho kimavazi, zibuniwe sare ambazo zitawapa stara wakina dada wa kiislamu katika majeshi yetu ya ulinzi na usalama.

Huu ni ushauri na maoni yangu sijaleta malalamiko hapa.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika. Mungu mbariki Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli.
 
Ukumbuke pia majeshi yote hayana dini kwa kuwa naturally majeshi yote ni wauaji.
Haitakiwi kulazimisha inabidi iwepo ruhusa kwa anaetaka avae asiyetaka aache.
Unakuta labda MTU akiwa kwake anavaa mavazi ya stara akienda kazini anavaa mavazi kufuata kazi inavyotaka hapa unakuwa unamnyima haki yake ya kiimani.
 
Asalam aleykum afande
tapatalk_1559462066140.jpeg
tapatalk_1559462079408.jpeg
 
Back
Top Bottom