Ushauri na ombi kwa Wizara ya Ulinzi na Usalama

Muulize swali hili, Mwanamke akipewa silaha( bunduki full magazine( kwenda vitani kuua atakwenda au atasema kuua Ni katazo la Allah?
Naongelea mavazi wewe,mfano Dubai askari Wa kike wanavaa hijab na mavazi ya stara,mengine yote sipingi.
 
Zimefanyaje mkuu hizo hijabu tafadhali huko mashuleni?
Miaka ya nyuma wanafunzi Wa kike walikuwa hawaruhusiwi kuvaa hijab mashuleni watu walipoliongelea nakuomba walirusiwa kuvaa na serikali ,mpaka sasa hakuna baya lolote lilotokea.
 
Siku ukisikia neno MADAM huko majeshini ndiyo uje na huo ushauri wako
 
Mkuu tukiendelea hivi iko siku tutaomba mbwa wa police wasiwepo au uwanja wa ndege kusiwe na mbwa wa ukaguzi mimi nadhani ombi lako ni nzuri ila lingefaa lifanywe na wale wahusika kabla ya kuomba kazi.
 
Miaka ya nyuma wanafunzi Wa kike walikuwa hawaruhusiwi kuvaa hijab mashuleni watu walipoliongelea nakuomba walirusiwa kuvaa na serikali ,mpaka sasa hakuna baya lolote lilotokea.
Mkuu unaweza mlazimisha mtoto kuvaa hijabu shule ya msingi mpaka Olevel akifika Chuo kikuu anavua. Cha msingi wapate mafundisho yatakayofanya wawe na hofu ya Mungu.

Hata hawa unao waombea hapa unaweza kuwaona hawajavaa hijabu., lakini wakawa na hofu ya Mungu zaidi ya wale wanaovaa hijab.
 
Haitakiwi kulazimisha inabidi iwepo ruhusa kwa anaetaka avae asiyetaka aache.
Unakuta labda MTU akiwa kwake anavaa mavazi ya stara akienda kazini anavaa mavazi kufuata kazi inavyotaka hapa unakuwa unamnyima haki yake ya kiimani.
 
Ukimaliza kushauri habari ya mavazi utaanza kushauri na zile siku ambazo watu hawa huenda kwenye ibada wasiwe wanaenda makazini ilhali ukijua kazi zao ni 24/7. Sasa sijui nchi na mipaka yake, Makambi ya jeshi na vifaa vyake vitakuwa vinalindwa na nani?
 
Asalam aleykum wanajamii.

Moja kwa moja kwenye lengo nchi yetu pendwa ni moja kati ya nchi zinazompa Uhuru RAIA wake kuabudu dini yeyote aipendayo kikatiba.

Leo najikita zaidi kuiomba serikali na wizara husika kuwapa uhuru wa kuabudu watumishi wake.

Hapa nasimama kutoa hoja hii kama itafaa basi ifanyiwe kazi na vyombo husika, watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama, askari polisi, askari wa jeshi la wananchi, jeshi la zima moto, uhamiaji na jeshi la kujenga taifa.

Haya ni majeshi yanayoajiri watu wa dini zote hapa nchini na kuwapa uhuru wao wa kufanya ibada lakini kumekuwa na unyimwaji wa uhuru wa mavazi kwa waumini wa dini ya kiislamu hasa kwa waajiriwa wa kike.

Kwa mujibu wa dini ya kiislamu mwanamke anatakiwa kujistiri mwili wake popote alipo, sasa hapa kwetu mambo ni tofauti kidogo hakuna mavazi au sare katika majeshi yetu yanayompa uhuru mwajiriwa husika wa kike kujistiri.

Hivyo nashauri Wizara husika ziangalie uwezekano wa sare za kujihifadhi kwa hawa dada zetu wa kiislamu wapate angalau uwezekano wa kuficha nywele zao na mavazi yao yawe ya stara hata kama ni suruali basi ziwastiri kwa mujibu wa dini na imani yao.

Tunaweza kuangalia mifano kwa nchi zilizowapa uhuru wanawake wa kiislamu kujistiri wakiwa katika majukumu yao ya kijeshi, kwa kuwa nchi yetu haina dini basi haiwezi kuwa tatizo.

Kuna wakina dada wengi wanatamani kujiunga na majeshi yetu lakini wanaogopa kwenda kinyume na maamrisho kimavazi, zibuniwe sare ambazo zitawapa stara wakina dada wa kiislamu katika majeshi yetu ya ulinzi na usalama.

Huu ni ushauri na maoni yangu sijaleta malalamiko hapa.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika. Mungu mbariki Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli.
Jeshini hakuna dela muraaa...kwanza askari hawana jinsia bhanaa! Chacha na Mwajuma wote ni poti muraa
 
Ukimaliza kushauri habari ya mavazi utaanza kushauri na zile siku ambazo watu hawa huenda kwenye ibada wasiwe wanaenda makazini ilhali ukijua kazi zao ni 24/7. Sasa sijui nchi na mipaka yake, Makambi ya jeshi na vifaa vyake vitakuwa vinalindwa na nani?
Ni mavazi tu mkuu.
 
Haitakiwi kulazimisha inabidi iwepo ruhusa kwa anaetaka avae asiyetaka aache.
Unakuta labda MTU akiwa kwake anavaa mavazi ya stara akienda kazini anavaa mavazi kufuata kazi inavyotaka hapa unakuwa unamnyima haki yake ya kiimani.
Mkuu huko wanataka uniformity tu sio vinginevyo, ndio maana hata viwandani kuna mavazi hayaruhusiwi sababu ni hatari kwa usalama.
 
Hahaahaa mkuu,kwa hiyo wote wameoa?
Bunduki ndo mchumba wako pot
sn.jpg
 
Nani alete udini wewe kuwa muelewa basi,mbona mashuleni mabinti Wa kiislamu wanavaa hijab kwa sasa lakini miaka ya nyuma haikuruhusiwa baada ya wanaharakati kulisemea serikali ikawa sikivu.
Ndio maana nikasema kama haikuwezekana wkt wa Mzee Mwinyi kwakuwa wkt wa Mwinyi ndio mambo ya hijabu mashuleni yalikuja so haitatokea tena na ndio maana neno uniform mashuleni halupo kwasababu uniform maana yake muonekane sawa sasa unataka kuleta haya mahovyo hivyo jeshini? Acha hizi mkuu
 
Nani alete udini wewe kuwa muelewa basi,mbona mashuleni mabinti Wa kiislamu wanavaa hijab kwa sasa lakini miaka ya nyuma haikuruhusiwa baada ya wanaharakati kulisemea serikali ikawa sikivu.
Uelewa ninao Mkuu! Yeyote aliyepita jeshini haya mawazo yako hawezi kuyakubali hata chembe! Ishieni huko huko shule za msingi na sekondary lakini sio majeshini
 
Asalam aleykum wanajamii.

Moja kwa moja kwenye lengo nchi yetu pendwa ni moja kati ya nchi zinazompa Uhuru RAIA wake kuabudu dini yeyote aipendayo kikatiba.

Leo najikita zaidi kuiomba serikali na wizara husika kuwapa uhuru wa kuabudu watumishi wake.

Hapa nasimama kutoa hoja hii kama itafaa basi ifanyiwe kazi na vyombo husika, watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama, askari polisi, askari wa jeshi la wananchi, jeshi la zima moto, uhamiaji na jeshi la kujenga taifa.

Haya ni majeshi yanayoajiri watu wa dini zote hapa nchini na kuwapa uhuru wao wa kufanya ibada lakini kumekuwa na unyimwaji wa uhuru wa mavazi kwa waumini wa dini ya kiislamu hasa kwa waajiriwa wa kike.

Kwa mujibu wa dini ya kiislamu mwanamke anatakiwa kujistiri mwili wake popote alipo, sasa hapa kwetu mambo ni tofauti kidogo hakuna mavazi au sare katika majeshi yetu yanayompa uhuru mwajiriwa husika wa kike kujistiri.

Hivyo nashauri Wizara husika ziangalie uwezekano wa sare za kujihifadhi kwa hawa dada zetu wa kiislamu wapate angalau uwezekano wa kuficha nywele zao na mavazi yao yawe ya stara hata kama ni suruali basi ziwastiri kwa mujibu wa dini na imani yao.

Tunaweza kuangalia mifano kwa nchi zilizowapa uhuru wanawake wa kiislamu kujistiri wakiwa katika majukumu yao ya kijeshi, kwa kuwa nchi yetu haina dini basi haiwezi kuwa tatizo.

Kuna wakina dada wengi wanatamani kujiunga na majeshi yetu lakini wanaogopa kwenda kinyume na maamrisho kimavazi, zibuniwe sare ambazo zitawapa stara wakina dada wa kiislamu katika majeshi yetu ya ulinzi na usalama.

Huu ni ushauri na maoni yangu sijaleta malalamiko hapa.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika. Mungu mbariki Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli.
Kila kazi Ina miiko yake kama inapingana na imani na utamaduni wako unakaa pembeni.
 
Back
Top Bottom