GIRITA
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 4,128
- 5,236
Asalam aleykum wanajamii.
Moja kwa moja kwenye lengo nchi yetu pendwa ni moja kati ya nchi zinazompa Uhuru RAIA wake kuabudu dini yeyote aipendayo kikatiba.
Leo najikita zaidi kuiomba serikali na wizara husika kuwapa uhuru wa kuabudu watumishi wake.
Hapa nasimama kutoa hoja hii kama itafaa basi ifanyiwe kazi na vyombo husika, watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama, askari polisi, askari wa jeshi la wananchi, jeshi la zima moto, uhamiaji na jeshi la kujenga taifa.
Haya ni majeshi yanayoajiri watu wa dini zote hapa nchini na kuwapa uhuru wao wa kufanya ibada lakini kumekuwa na unyimwaji wa uhuru wa mavazi kwa waumini wa dini ya kiislamu hasa kwa waajiriwa wa kike.
Kwa mujibu wa dini ya kiislamu mwanamke anatakiwa kujistiri mwili wake popote alipo, sasa hapa kwetu mambo ni tofauti kidogo hakuna mavazi au sare katika majeshi yetu yanayompa uhuru mwajiriwa husika wa kike kujistiri.
Hivyo nashauri Wizara husika ziangalie uwezekano wa sare za kujihifadhi kwa hawa dada zetu wa kiislamu wapate angalau uwezekano wa kuficha nywele zao na mavazi yao yawe ya stara hata kama ni suruali basi ziwastiri kwa mujibu wa dini na imani yao.
Tunaweza kuangalia mifano kwa nchi zilizowapa uhuru wanawake wa kiislamu kujistiri wakiwa katika majukumu yao ya kijeshi, kwa kuwa nchi yetu haina dini basi haiwezi kuwa tatizo.
Kuna wakina dada wengi wanatamani kujiunga na majeshi yetu lakini wanaogopa kwenda kinyume na maamrisho kimavazi, zibuniwe sare ambazo zitawapa stara wakina dada wa kiislamu katika majeshi yetu ya ulinzi na usalama.
Huu ni ushauri na maoni yangu sijaleta malalamiko hapa.
Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika. Mungu mbariki Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli.