Jeff
JF-Expert Member
- Sep 26, 2009
- 1,293
- 202
- Habarini wadau wa MMU
Naombeni ushauri kwa hili, nimegombana na mpzn wangu jana nimejaribu kuplease but anaonekana kukaza usi wa kuvunja mahusiano, sababu ni kuwa namfuatilia sana analalamika kuwa hana uhuru kwani namfuatilia sana kwenye simu na facebook kwa watu anaochati nae, na sasa yuko chuo na nimemsaidia sana kipindi cha kwanza wakati anaripo chuo mana wazazi wake hawakuwa vizuri kifedha wakati huo, nimekuwa nae karibu sana kwa muda wote huo, kiukweli naweza kusema ni mwaminifu kiasi mana amekuwa muwazi kwangu kwa kila kitu, ila anapenda sana kuchati na nikifuatilia nakuta hakuna uhusiano wa kimapenz na hao anaochati, sasa amechukia na amewaomba ushauri wenzake huko hostel wakamshauri eti aachane na mimi kwani namfuatilia sana,na hii ni mara yapili kukosana but tulisameheana, nimemuomba msamaha sana lakini amekataa anasema ni mara pili nimerudia hivo ni tabia yangu hii anaogopa, jinsi alivyo ni mtu ambae si mwepesi wa kuchukia but ni mgumu kusamehe akishachukia, naombeni msaada wenu wadau, nimvutie muda afu nirudi tena kuomba msamaha au nipotezee? mana kwa sasa niko mbali nae ila nimemwahidi kwenda wikiend ijayo lakini amekataa, hayuko tayari kuonana na mimi, hivyo nimemuacha pending kwanza! nataka nikienda ndio nimwambie kama nimerudi so nimuone, nipeni ushaurini ndugu zangu,