Ushauri na mawazo yenu ni muhimu hapa

Ushauri na mawazo yenu ni muhimu hapa

Well said!!
kumsaidia imekua nongwa? Itakuwa unamnyanyasia msaada wako la sivyo usingeandika humu kama ulimsaidia......

Pili ndugu mambo gani hayo ya kufuatana fuatana mpaka facebook? Kwa nini hujiamini? Maana ukijiamini utamuamini na yeye pia......

Ushauri wangu huyo dada asikurudie....... In reality hakuna kitu kibaya kama kuwa na mpenzi anakufuatilia unachati na nani, unaongea na nani? Msg, nani kakupigia simu, nani amekuongelesha , emails etc inaudhi inaudhi inaudhi .....

Kumbuka ni mara ya pili unarudia huo mchezo....mwisho wa siku
utaanza kumchagulia marafiki..... Akimaliza chuo akapata kazi
itakuwaje? Au utamwambia awe mama wa nyumbani? INAKERA SANA KUWA NA MTU ASIYEJIAMINI KUTWA ANAKUCHUNGUZA UNAONGEA NA NANI UNACHATI NA NANI NANI KAKUTONGOZA

jiamini kijana


na ushauri kwako unahitaji upewe ushauri nasaa...muine Mtambuzi au dada AshaDii maana unakoelekea sio kwema
 
Last edited by a moderator:
Kwa post hii nashawishika kuamini thamani yake kwako ni kitumbua tu!!! Kweli wanaume wamekwisha wamebaki wa kiume.....hatari
nimekizoea bhana, kitu hakina harufu usiku mzima, kitu safi tuu, huko nje nakutana na harufu za ajabu, ya nini shida hiyo? nakuwa nabahatisha kupata kitumbua kizuri kama hiki, ukiona bado nakitaka ujue kinalipa, huko nje mpaka nianze kutest tena khaaa!
 
Kwa post hii nashawishika kuamini thamani yake kwako ni kitumbua tu!!! Kweli wanaume wamekwisha wamebaki wa kiume.....hatari

Hahahah....
jamaa anaogopa kukutana na mabumunda "mkate wa kienyeji"....ye kashakizoa kitumbua chake hata akikikamua vipi hakitoi mafuta kumkinai...
 
khaaaaa! FP naona umekuwa mbogo, punguza munkari basi nimekuelewa, hata hivyo mimi sina tabia hiyo ya kukumbusha vitu nilivyompa, ila kiukweli inakera? kama mtu anakupa bila kuomba in mana anakujali
Nimefurahi kama umeelewa........ndo essence nzima ya kuomba na kupewa ushauri
kama rafiki yangu BAK alivyosema, wivu unahusika kwenye mapenzi ya kweli, huwezi kusema unampenda mtu na usimwonee wivu, lakini unachokifanya wewe ni kumwonyesha kuwa humwamini, huu sio wivu.
hakuna kitu kinakera katika mahusiano kama kuona mtu uliyenaye hakuamini (hii ni according to me), na hasa kama unajiamini hufanyi hayo anayofikiria unayafanya.....inauma sana
 
Last edited by a moderator:
asante mdida, nimeongea nae na kumbembeleza anaonekana kulegeza kamba, amenipa nafasi ya kukaa na kuongea nae this weekend, ndio nitaenda huko chuoni kwao, ila nataka kumwambia nilale nae wikiend hii ili tuweze kuongea kwa uhuru, hapo vipi nitamboa? ingawa simanishi ni lazima 2sex, ila nilipenda nikae mazingira kama hayo ndio niongee nae sijui kama atakubali,
pia nafikiria kumpelekea kazawadi ili nimpoteze hasira zake, ni vyema nikaipeleka hiyo zawadi ai nikamchukue twende wote dukani?
Bro inaonekana umependa mpaka umekuwa dhaif, sasa kama huyu mrembo ana nguvu kiasi hiki kwa nini unatingisha kiberiti?... Unamkasirisha wakati unajua fika huwezi kuhimili mapigo!
 
Wivu upo ktk mapenzi na ni kitu cha kawaida ila inatakiwa uwe na kiasi, cha msingi mwache kwanza apate mda wakutulia kisha nenda moja kwa moja hapo chuo muelezee kilichojiri natumai ni mtu ka binadamu wengine atakuelewa ikishindikana watumie wenzie walewale unaohisi walimshauri muachane waelezee kwa lugha ya busara,, ila jiangalie sana kumwekea akili sana mwanamke inaweza kua risk kwa maisha yako,,, kozi anawezafanya kitu ambacho hukutarajia kama kukuacha au kuolewa na mtu mwingine
Nb: wajinga ni chakula cha wasomi
"Watchout"
 
Kila la heri. Usisahau kurudi jamvini kutoa update za juhudi zako.
pamoja BAK nitawapa feedback jumamosi usiku, ndio nitajua nini kinaendelea kati yetu,nashukuru kwa ushauri wenu wa kunipa moyo wa ukakamavu ili nikubaliane na matokeo yeyote yatakayokuja
 
daaah pole sana jaribu kumwambia muonane mpate kuyaongea vizuri na utaweza kubaini kama bado anakupenda au ndo kaisha jiachia na mwingine utamjua 2 kwa sura na hata majibu atakayo kupa ana kwa ana utaweza kugundua kitu ikishindikana jaribu kutumia marafiki zake wanaweza kukusaidia ubarikiwe sana
 
wadau nimerudi tena kwa feedback, siku niliyosafiri kwenda huko mkoani, alinisubiri kwa hamu tu tena nilichelwa kufika nikafika usiku kama saa moja na nusu, alinisubiri na rafiki yake then tukaenda mahali tukakaa, rafiki yake akaondoka hatukuweza kukaa nae usiku huo kwani alichelewa kwao yeye hakai hostel, hivyo nilikaa nae mpaka saa tatu usiku, lakini hakutaka tukalale wote alinipa sababu ambazo kweli niliprove ni kweli (room mate wake alikuwa mgonjwa so asingeweza kulala nje ya room na kumuacha wakati ni kama dada yake wa chuo) na wakati huo tumetoka hakupenda niwe naongelea sana kuhusu hilo tatizo kwani anasema anaumia sana,
nikamwacha akarudi hostel tukiwa tumepata tuonane next day yani jumapili, ilipofika jumapili yule rafiki yake akazidiwa zaidi akalzwa hospital na kweli niliprove hilo hakunidanganya, so hatukuonana tena
jumatatu ikabidi niende chuo mida ya jioni kama ambavyo ameniambia niende baada ya kunipa ratiba yake, nilipoenda tukaongea tukiwa pamoja na rafiki yake aliyekuja nae mjini siku niliyofika lakini kauli ilikuwa hivi," NIMECHOKA KWA MAMBO YAKO HIVYO CHAGUA MAWILI, TUENDELEE KUWA WAPENZI LAKINI HATUTAOANA AU TUACHANE KABISA KUANZIA SASA" nikamuuliza kama bado anaipenda akanijibu ndio nakupenda lakini siwezi kurudiana na wewe tena, kwani najua hautajirekebisha, nikamwambia unavyosema tuwe wapenzi lakni kila mtu awe huru kama atampata mwingine ina maana hakutakuwa na uaminifu na commitiment kati yetu hapo, nikamuuliza kama amepata mwingine aniweke wazi ili nijue moja akanijibu hana na hafikirii hilo kwa sasa, kwani amepoteza moyo wa kupenda tena kwa sasa, anaomba tu tubaki marafiki tuwe tunawasiliana kama kawaida na kusaidiana lakini sio kimapenzi tena
mimi sikumuelewa, nikampa muda siku iliyofuata nikaongea nae tena akabaki na msimamo wake huo, na akawa sasa anakataa kunipa nafasi ya kukaa na kuongea nae eti kwa sababu anajua nitamshaiwishi atanisamehe
tukaendelea hivyo akiwa na shida anaitafuta na kuniomba msaada kwa mfano alikuwa na ssigment akaniomba nimsaidie kufanya mimi nikafanya hivyo nikiamini kuwa atajirudi, nikimpigia na kuongea kuhusu mambo yetu anisamehe anachukia na kusema bora nisimpigie kama naongelea mambo hayo, ikabidi niwe mpole, nikamwachia kazi yake kweny flash yangu then nikasepa jana nikampigia simu nina shida na flashi lakini nilimwambia sio kama nakupokonya nina kazi nayo the nitakurudishia akaniambia njoo uchukue, nilipoenda nikakuta ile kazi niliyomfanyia hakuprint bado iko kwenye flash, ikabidi nimuachie tena akishaprint ndio nikachukue, leo amenipigia simu eti ile kazi imepotea kwenye flash so ameomba nimtafutie tena na nimuandikie hiyo assigmnet then nimpelekee, nikakubali nikaifanya hiyo kazi, wakati najiandaa kwenda akanipigia na kuniambia sorry nimpelekee kesho kwani leo hatopata muda wa kuniona na kuchukua hiyo kazi,
kwa hiyo hapa nasubiri anipigie ili nimpelekee hiyo kazi na nikachukue na flash yangu lakini nikiongea nae tu kuhusu mambo ya kumuomba msamaha anisamehe anasema nisiongelee hayo kwani namuumiza,
na nimemuomba tutoke jumamosi akanijibu ataangalia muda akiwa free tutatoka lakini hapendi niongelee tatizo letu na niombe msamaha
mpaka nimekata tamaa sasa, nataka kukubaliana na maamuzi yake sasa, mana amesema kwa sasa hata akikubali hatokuwa na upendo wa kweli kama mwanzo so itakuwa ni kuumizana tu, lakini kama akinipa nafasi si naweza kumrudisha katika mood na akanipenda kama mwanzo?
kiukweli nimejutia kosa na nimejirekebisha kabisa,sasa nafikiria kumshirika huyo dada yake wa hapo room mana niliyeongea nae ni kama mtoto mwenzie hauwa na power ya kumongea nae kiutu uzima na kumcomvince
nipeshi ushauri wenu na hapa jamani, nikate tamaa niachane nae au nivute subira ya kuendelea kuwasiliana nae kawaida then nione baade kama atabadilika? mana kuongea na mimi yuko tayari lakini hanichukulii kama mpnz wake tena bali ni mtu tu wa kawaida
nipeni ushauri wa mwisho ndugu zanguni, kwani kesho nataka nikahitimishe ikiwezekana na ushauri mtakaonipa
 
kashapata njemba huyo mpotezee

hapana mkuu naamini bado hajapata njemba ingine, kwani bado yuko free kuwa kukaa na mm ila tatizo ni amekufa moyo wa kupenda kwa sababu ya yaliyotokea ndio najitahidi kumrudisha moyo mkuu
 
Pole sana,achana nae,atakuumiza tu on da way,mpe km mwezi ukiona bado chapa lapa kwenye mapenzi ya kweli wivuu unahusika kama hajui hlo achana nae
 
hapana mkuu naamini bado hajapata njemba ingine, kwani bado yuko free kuwa kukaa na mm ila tatizo ni amekufa moyo wa kupenda kwa sababu ya yaliyotokea ndio najitahidi kumrudisha moyo mkuu

Jeff wanaume hatufanyagi hivyo huyo anakuburuza nimesoma hiyo habari ya asyment nimegundua kuwa huyo msichana anakuweza sana na utaburuzika vibaya kama utakuwa ni mista Lia lia.CHA KUFANYA HAPO MCHUNIE NA WEWE ILI USIKILIZIE KAMA ANAKUPENDA.huyo msichana gani akikasirika hatoi msamaha.KIMBIA NDUGU UTABURUZIKA HADI UKOME HUU MWAKA.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana,achana nae,atakuumiza tu on da way,mpe km mwezi ukiona bado chapa lapa kwenye mapenzi ya kweli wivuu unahusika kama hajui hlo achana nae

asanteee kwa ushauri wako, nimefikia maamuzi hayo sasa mana naona nitapenda pasipopendwa
 
Jeff wanaume hatufanyagi hivyo huyo anakuburuza nimesoma hiyo habari ya asyment nimegundua kuwa huyo msichana anakuweza sana na utaburuzika vibaya kama utakuwa ni mista Lia lia.CHA KUFANYA HAPO MCHUNIE NA WEWE ILI USIKILIZIE KAMA ANAKUPENDA.huyo msichana gani akikasirika hatoi msamaha.KIMBIA NDUGU UTABURUZIKA HADI UKOME HUU MWAKA.

asante sana ndugu BILLIE, nimefikia maamuzi hayo sasa, no more discussion, kuanzia leo naanza kumlia bati kila mtu kivyake, afu cha ajabu sasa eti anataka anipe tena na assgnment zingine nimfanyie kwani analialia eti assignment zimekuwa nyingi na test nyingi so nimsaidie, nikamwambia nitampa laptop atumie nikiwa na shida nayo nitaifuata, lakini sasa nimeghairi na hilo pia ngoja nimpe assignment yake ya leo then nisepe kimoja sirudi tena kuomba msamaha labda ajirudi yeye, alaaaaaaa,
 
Ndugu zangu wanaJF wote nashukuru kwa ushauri wenu, kwani umekuwa ukinipa faraja wakati mwingine,kwa wakati napenda kuhitimisha mjadala huu kwa kusema kuwa nimeamua kuafiki maamuzi yake na hivyo sitabembeleza tena, labda naweza kurudi tena hapa kama kutakuwa na mabadiliko kwa upande wake tofauti na maamuzi yake ya sasa, nami nitafikiria mara mbili kurudiana nae iwapo atabadili msimamo wake, mana na mimi nimegive up sasa
 
Big up kaka kwa kuamua kukaa kimya coz atakuumiza huyo,si anajua unampenda ndo mana anakudrive so fanya ishu zako.
 
Kama hujajua huyo ashakuona weak juu yake... Dawa mpe tym aone atakachokuja kipata kwa mwanaume ambaye hana wivu nae then atarud...
 
Kama hujajua huyo ashakuona weak juu yake... Dawa mpe tym aone atakachokuja kipata kwa mwanaume ambaye hana wivu nae then atarud...

duh kuna wanaume wavumilivu! Mi nimezinguli siku kadhaa nimefuta picha zake kwenye cm, pc na msg zake zote(anapendaga nizitunze). Kesho kuna kitu naconfirm ili nifute na namba yake kabisa. Wagonjwa wanipe challenge na mchuchu unisumbue! Pumbaf.
 
Back
Top Bottom