Ushauri: Mwanamke wangu kanifanyia haya Je nimsamehe Kweli?

Status
Not open for further replies.

Calvin Don

Senior Member
Nov 3, 2019
107
91
Habari wana JF

Kwanza nitangulize shukrani kwa yeyote aliyefungua uzi huu. Nina changamoto sana katika swala la mahusiano kwa mwanamke niliyekutana nae Dar na kuanzisha mahusiano. Tumedumu katika mahusiano kwa kipindi cha Miaka 5, muda huo wote tulikua tukiishi wote lakini atujaona. Na mwaka jana mwishoni tulibahatika kupata mtoto wa kike paka sasa mtoto ametimiza mwaka mmoja.

Twende kwenye Mada, Wakati nikiwa na uyo mwanamke alikua akinichit bila kujua. Lakin kunakipindi nilishtukia mambo yake nikaamua kuitrack simu yake. Nilingundua vitu vingi sana. Nikagundua ananisaliti nikapiga kimya. Sikuongea chochote. Siku moja usiku nimetoka kazini nakumbuka siku iyo niliondoka nyumban kwenda kazin hatukuwa sawa tulikwaluzana kwa mambo mengine kabisa. Niliporud usiku muda was kulala nikaenda kulala nikawanimemuacha sitting room nikochumbani muda sijui kinachoendelea huko nikatoka kwa kushtukiza nikakuta anachat na mwanaume mbaya zaidi nilingundua alishazini nae. Nakumbuka kutokana na jazba nilimpiga cjawai kumpiga but nilimpiga Sana, lakn yaliisha tukafanya suruhu yakaisha. Kwa kifupi uyu mwanamke mkikwazana kidogo yeye anachojua ni kuchit. Hata mbali na kuchit anaweza kukufanyia vituko tu ukasilike.

Tumeendelea na hayo maisha paka akapata ujauzito. Kipind Cha ujauzito. Kanichiti pia Mara kibao akiwa na mimbaa yangu paka nikajiuliza hivi iyo mimbaa no yangu kweli. Ukizingatia najituma kumtimizia mahitaji yake Kama mwanamke lakn mwenzangu yeye mkwazane anachojua kuchit. Wakati waujauzito nilingundua kalala na mwanaume siku iyo alikua anasubir nitoke niende kazini lakni wakati najiandaa nilikua namsemesha mwenzangu Yuko buz na simu kuchat. Nilipomkonya simu niliona anachat na mwanaume anasubir nitoke akalale nae mbaya Zaid mwanaume uyo anaforce aje kulala nae kwangu.

Nitaendeleza baadae kidogo nistor ndefu. Nahitaji ushauri
 
Iyo ni kwa upande wako ungeleta na yeye malalamiko yake tupate side zote mbili ili ushauriwe tujue ukweli ndio upate kitu ambacho kitakujenga kifikra na kukusaidia la sivyo ni sawa na kizoa kinyesi na sufuria ya kupikia


Ila narudia tena ila!!!! Kama uliyo sema ni kweli acha kupoteza wakati tafuta mke uoe
 
Kuvunja simu siyo suluhisho,
Tafuta suluhisho la tatizo! Halafu khabari ya kuvunja simu hizo ni khasira za kizungu usijaribu kuzi apply Bongo tena kwa maisha haya ya awamu hii ya 5..!!
Navunja! hasira zikiisha ntamnunulia nyingine

sina solution kwa mwanamke mwenye dharau zaidi ya kumzabua.
 
Kama jinsi nisivyo kusapoti kutetea mwanamke anaenionyesha dharau wazi wazi.
Ingekuwa kupigwa ni suluhisho la matatizo nadhani shule zote zinazochapa wanafunzi wangekuwa na nidhamu A+..!!
Mpaka mwanamke apate ujasiri wa kukufanyia dharau jitafakari unakwama wapi, halafu tumia uanaume wako kupanyoosha hapo na siyo kuanza kupiga, watoto wenyewe laini hawa sijui huwa mnawapiga wapi.!!
 
Ingekuwa kupigwa ni suluhisho la matatizo nadhani shule zote zinazochapa wanafunzi wangekuwa na nidhamu A+..!!
Mpaka mwanamke apate ujasiri wa kukufanyia dharau jitafakari unakwama wapi, halafu tumia uanaume wako kupanyoosha hapo na siyo kuanza kupiga, watoto wenyewe laini hawa sijui huwa mnawapiga wapi.!!
wooi SweetieLee acha tu ninyamaze mimi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom