Ushauri: Mwanamke wa nje ananichanganya

Mti wa Chuma

JF-Expert Member
Jul 2, 2015
331
99
Habari msomaji wa uzi huu.

Hii stori si yangu nimeona vyema nishare nanyi kwa kuwa JF ni jukwaa kubwa lenye watu wanaoweza kushauri.

Stori...
Habari ndg.
Mimi ni kijana wa umri wa miaka 26 nimeoa nina mtoto mmoja wa miaka mitatu.

Hivi karibuni kuna mdada mmoja amekuwa akinipenda sana, hali hii imesababisha nami nimpende kwa dhati. Maana kila siku jioni lazima afike ofsini kwangu kunipokea.

Hatujawahi kufanya mapenzi. Kinachonishangaza ni kwamba anajua kuwa nina mke, na kila nikimweleza hivyo anasema kuwa ananipenda sana.

Ndugu naomba ushauri wako.

Wanajukwaa hii ndivyo ilivyo, tumshauri huyu mpendwa.
 
.....kuna vitu kama mwanaume hautakiwi kuomba ushauri...wewe ni kichwa uliaminika kwa MUNGU ukawekwa juu ya utawala wa mwanamke....unatakiwa kuweka kipaumbele cha familia kwanza...mtoto akiwa wa kwanza,mkeo wa pili na ww nyuma yao ukiwa kama mlinzi wao ....being gentleman is another task.Kama hata ww unashindwa kwa jaribu la kutongozwa mkeo je?....be strong so that she can feel confortable when she's beside you.....UMWAMBA WA MWANAUME SIO KUWA NA MICHEPUKO MINGI...UMWAMBA WAKO NI KUIWEZESHA FAMILIA YAKO IWE BORA NA IMARA MAANA WW NDO KIONGOZI...FURAHA NA AFYA BORA NI KITU MUHIMU
 
Mkuu unataka tukushauri uiache familia yake kwa sababu ya mchepuko? Aah huwezi kuwa sawa
 
Aisee....!
Sasa wewe ulioa nini? Kwani ulilazimishwa? Kwani nini kinakushinda kumwambia mwanamke embu achana na mimi nina familia yangu ukasema kiume kabisa? Au tu mnapenda kusumbua watu humu na hizi chai?
Kamwambie LWENYI kasema achana na mimi nina mke na mtoto wananihitaji sana
 
ampende tu kwani kuna shida gani, kwanza tunatakiwa kupendana wooote.

hata kama akijitokeza mwingine wewe mpende tu hakuna namna
 
Mpaka hapo na wewe pia unampenda, lakini kumbuka kipo anachokitaka kwako,na sio wewe,fikiria sana tena sana..
 
Afu yakikukuta utaanza kumlaumu huyo mdada while unamuentertain mwenyewe. "Ikimbieni zinaa",... wewe endelea kuichekea
 
Em behave kama mume basi si umeoa wewe ridhika na akupacho mkeo kama Kuna mahali anakosea kaeni myarekebishe usilifuge joka litakalo kudhuru baadae kua makini usije kutulilia bure
 
Maana naona kama story haijaisha unataka tuseme aanzishe uhusiano na huyo dada af badae uje useme ulishauriwa hvyo na wana jf.... Mwambie amalizie story huyo mshkaj wako then tutajua cha kumshaur
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom