Zeddicus
JF-Expert Member
- May 5, 2012
- 627
- 540
Habari zenu wana-JF, bila shaka mu wazima wa afya. Nimekuja mbele yenu wanajamii wenzangu nipate ushauri kwani naamini mbele yenu great thinkers haritaharibika jambo, Nisiwachoshe sana ni hivi;
Mimi nimeoa na nina mtoto mmoja, ndoa yangu ina miaka miwili mpaka sasa. Wakati wa uchumba mimi na huyu ambaye ni mke wangu kwa sasa tulipendana sana, haswa kwa upande wake kwani alikuwa akija kwangu na kunifanyia yote ambayo responsible wife anatakiwa afanye. Hata pale nilipomuoa hali ilikuwa hivyohivyo alikuwa akihakikisha napata cha afya walau mzunguko mmoja asubuhi kabla ya kwenda kazini.
Sijui ni vipi nilijichanganya nikaanza ku-date na mwanamke mwingine pembeni ingawa nakiri bado nilikuwa nikimpenda sana mke wangu kipenzi. Nilikua nikifanya jambo hili kwa siri sana. Hapa mke wangu alikuwa mjamzito karibu kujifungua hivyo alienda kujifungulia kwa mama mkwe (mama yake mzazi) hii ilinizidishia nafasi kujivinjari na small house yangu. Kama ilivyo ada dunia haina siri jambo hili lilimfikia mke wangu lakini nilijitahidi sana kukana.
Alipojifungua alirudi nyumbani, kusema kweli kipindi hiki nilikuwa mkali sana kila alipokuwa akigusa simu yangu, na ikafika kipindi akagundua ukweli baada ya kufuma sms za mapenzi za small house wangu. Kwa kweli tangu agundue jambo hilo alikasirika sana na kuanzia siku hiyo amekua akininyima unyumba, Nimeachana na huyu hawala for the sake of my marriage lakini mke wangu mpaka leo hataki kunisamehe hili jambo tunalala mzungu wa nne, kila nilimuomba unyumba ananimbia niende kwa hawara wangu.
Bado nampenda sana mke wangu, Vitu vyote anafanya kama mke ila swala la unyumba ni mwaka sasa sijawahi pata na huwa ananiambia nikizidi kumlazimisha atarudi kwao (kuna kipindi kweli alirudi akakaa kama mwezi hivi na akarudi baada ya mimi kumbembeleza sana) ubaya zaidi mama yake yupo upande wake.
Wanajamii naomba ushauri wenu nifanyeje nirudishe upendo wake kwangu na aniamini tena, nampenda sana mama mtoto wangu na,nimemmiss kweli. Natanguliza shukrani na samahani kwa kuwachosha kwa thread ndefu.