Uchaguzi 2020 Ushauri muhimu sana kwa Tundu Lissu tukielekea Oktoba 2020

Ni kweli kabisa, kwa muundo wa serikali yetu kile kinachofanywa na serikali kina akisi moja kwa moja msimamo wa rais. Lakini ni vema kuikosoa serikali ya CCM na kuinadi serikali mbadala ya CDM.
Sasa hivi amekuwa malaika? Mwaka 2015 kipindi anamshambulia Lowasa na afya yake na push up majukwaani ilikuwa ni nini? Acha apate vidonge vyake
 
Mtoa maelekezo serikslini ni mmoja tu hao wengine wanafuata,wao hawana tatizo ni wenzetu ila wamebanwa.
Maamuzi muhimu yote huwa yanajadiliwa kwenye vikao vya baraza la mawaziri. Kwahiyo kumlenga kiongozi mkuu peke yake inaleta picha kuwa una ugomvi binafsi na huyo mtu.
 
Unapotoa mada lazima uanze na utangulizi ili upate mtiririko mzuri wa hoja. Huu ulikua utangulizi wa Lissu hoja zinakuja.
Kwakweli tunazingoja kwa hamu, sote tunatambua uwezo wa Lissu wa kujenga hoja na kuzipangilia vilivyo. Uchaguzi huu tayari umenoga.
 
Sasa hivi amekuwa malaika? Mwaka 2015 kipindi anamshambulia Lowasa na afya yake na push up majukwaani ilikuwa ni nini? Acha apate vidonge vyake
Magufuli binafsi huwa hataji majina, yes alipiga push up kama njia ya kumdhihaki ndugu Lowasa lakini hakumtaja hadharani.

Sasa Lissu anarusha makombora direct kwa Magufuli huku akimtaja kwa jina kabisa.
 
Hivi baraza la mawaziri lilipitishaje ujenzi wa Chato Airport wakati halikuwahi kujadiliwa bungeni.
Inawezekana walitaka kumfurahisha mwenyekiti wa baraza, lakini wakitoka nje maamuzi ni yao wote na wanabeba 'collective responsibility'
 
mwarobaini_

Mkuu hongera kwa ujumbe, Lissu atumie umahiri wake katika kushawishi watu ili apate kura, Ni vizuri kumwaga sera nini atakacho kifanya pindi atakapopewa ridhaa ya kuongoza nchi.
 
Wagombea wasome ustaraabu wa watanzania,saikolojia, desturi na mahitaji yao kisera na nyakati za sasa itawasaidia sana nini cha kusema.
 
Back
Top Bottom