Ushauri: Mpenzi wangu amempa mimba msichana mwingine

Ushauri: Mpenzi wangu amempa mimba msichana mwingine

H
Nakuonea huruma unavyodanganywa na wewe unakubali.
Huyo mwanaume anapretend hana lolote huko kulia ili umuone hana kosa.
Usiingilie mambo yao acha wayamalize wenyewe.
Jitoe kabisa katika hilo sakata kama kalikoroga mwenyewe alimalize mwenyewe.
Halafu my dear hebu jiulize kama huyo mpenzio anakupenda kweli kwanini akucheat?
Hebu jiulize je ingelikuwa ni wewe huyo dada halafu mwanamke mwenzio anakufanyia hivo ungejisikiaje?Hebu vaa viatu vya huyo bidada.
Kaa na mpenzio ongea nae mpe condition kama bado unataka kuwa nae na unampenda mwambie arekebishe hilo vaga mwenyewe kwani kumkimbia huyo mwenye mimba sio solution.
Kumbuku unavyomsaidia kwenda kuchukua hizo nguo sijui vitu ili amkwepe huyo bidada usishangae Siku nyingine ikawa ni kwako.
uyu dada hawajui wanaume vizuri we subiri
 
U
Mkuu nikupe ushauri huyo jamaa usimwache ila huyo mtoto mtarajiwa amuhudumie ni damu yake. Akimkataa wakati kweli ni wake mtapata laana. Huyo jamaa anakupenda kweli na amejifunza ndio maana kapagawa. Sasa mwambie asiwe chapombe ataharibu kila kitu, hayo maji makali atuachie wadau wazoefu. Kumbuka takwimu siku hizi zinaonesha wanaume wa kuoa au kuwa mpenzi wa kudumu ni bidhaa adimu. Kanuni ya Demand and supply uizingatie. Ukimwacha huyo inaweza kukugharimu kumpata mwingine tena alie bora zaidi yake.
Uko moyoni mwake hadi useme “huyo jamaa anakupenda”. ? Hauko serious
 
Duh ishu ya 2017 hadi 2023 bado mnatoa ushauri tu
 
Kwa hapa nilipofikia naombeni msaada wenu wa mawazo yanaweza yakanifungua kichwa.

Kiujumla mimi ni Ke, nina uhusiano na mwanaume mmoja hivi ananipenda,ananijali na kunithamin sanaaa na tulikuwa tunamipango mizuri tu hapo baadae ya kuja kuishi kama mume na mke kwa kufuata taratibu stahiki ila mwezi January 2017 kuna meseji za binti mmoja hivi niliona amemtumia meseji mwanaume wangu, kama kuna kitu linaendelea kati yao mimi nikapuuzia kwa wakati ule ila nilikuja kumuuliza kuhusu huyo binti baada ya muda kama mwezi kupita akasema walisoma nae chuo na mambo kadhaa mimi nikaelewa nikapotezea.

Sasa kilichosababisha nikaandika haya ni kuwa Jumapili ya Pasaka tulipanga kwenda Cinema century hivyo nilitakiwa niwe kule kwa mpenzi wangu kuanzia Jumamosi until Jumatatu kwa ajili ya sikukuu ila hali ilikuwa kwan yote tuliyopanga kuhusu Pasaka yamekuwa ndivyo sivyo kwa sababu kumbe yule binti ambaye niliona txt zake amemtumia mpenzi wangu alikuja kutembea na mwanaume wangu na akapata mimba.

Hivyo navyoandika hapa mwanamke yule amekuja hom kwa mwanaume wangu kuanzia alhamis kuu mpaka sasa yupo na amegoma kuondoka mpenzi wangu ameondoka home kwake kuanzia Jumapili ya pasaka mpaka sasa ni kulala gesti anakunywa pombe (alikuwa hatumii kilevi) mpenzi wangu aliniita na kunieleza ukweli wote na analia sana na ameshamuambia huyo mwanamke kuwa ampendi yeye huyo binti ndo alimlazimisha atembee nae siku hiyo moja.

Hivyo jana tumekaa na mpenzi wangu tukashauriana kuwa ajifanye kupretend kwa yule mwanamke kuwa wanataka waende kwa kina mwanamke wakaongee hayo masuala then akimtoa pale mimi niende kuchukua nguo zote za mpenzi wangu na vitu vya muhimu then nifunge nyumba aje tukae kwangu pamoja kwa ajili ya kufikiria nini cha kufanya na Leo kuna mtu tumemtumia ili ampeleke yule mwanamke hospital akapige ultrasound ili ijulikane ni mimba ya miezi mingapi kwa sababu alidate nae mwezi wa kwanza mwishoni coz huyu binti anasema Mara mimba ya miezi miwili Mara miezi mitatu, Mara niliona siku zangu mwezi wa pili na kumbuka walidate siku moja tu na ni mwezi wa kwanza mwanzoni, kesho natumai kuonana na mpenzi wangu tena kuongelea kuhusu hiyo ultrasound imeonyesha nini.

Mpenzi wangu anakunywa tu pombe yaani anajuta na kulia tu.
Mpenzi wangu yeye ni mhandisi ila mimi nipo ofisi za watu binafsi.
Wana jamvi naombeni mnishauri kitu zaidi ya haya niliyosema naweza nikapata mwanga zaidi, mpenzi wangu bado ananihitaji ndio maana ameamua kunishirikisha.
Tit for tat is a fair game.

Na wewe beba mimba ya mwanaume mwingine. Period!

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom