Dena Amsi
R I P
- Aug 17, 2010
- 13,080
- 4,275
Nieleweke ni ndugu yangu 'Damu' mtoto wa Baba Mkubwa.
Kamaliza form four mwaka 2010 kafail alipata ziro na 'D' moja tu, 2011 akareseat ndo kavurunda kabisa, 2012 nikamwambia njoo huku nchi jirani nilipo mie akaja akaanza kusoma Diploma ya HR kaharibu mbaya semister ya kwanza kachemsha na vitabia fulani sio vizuri.
Nikamrudisha home nikamwambia chagua usome nini he jibu nililopata nusu nizimie 'Dada mie kusoma siwezi' nikasema wataka nini sasa. Ngoja nifikirie mie haya he kaenda kwa Mdingi wangu ambaye ni Mdogo kwa Baba yake kawashiwa moto hatari kwa ujinga wake na ushauri wa kipumbavu wa marafiki katoroka akaenda kuishi hostel na rafiki anayesoma CBE.
Jana nimekwenda mahali kula kiti ya moto mara namuona kabeba tray anakuja kunihudumia mie mdomo wazi. Namuuliza hii ndo kazi uliyotaka kufanya ama?? Anaanza kulia eti dada nisamehe nimekosa pesa ya kula imebidi nifanye hii kazi nisaidie.
Mwenzenu mate yalinikauka, maneno yalipotea sikujibu hata neno moja kiti ya moto yenyewe ilikuja nikafunga hata apetite yote iliyeyuka.
Naomba ushauri wenu nifanyeje