




malalamiko ya.mishahara imekuwa mingi sana mkuu.
Pole sana kwa unalopitia na nikuhakikishie kabisa hauko peke yako ni mtego ambao waajiriwa wengi wamenasa.
Hapo namba 1 ni kwamba una matumizi makubwa kuliko pesa uipatayo na kadri upatavyo pesa nyingi basi unakuta inakulazimisha kufanya matumizi makubwa pia.
Mengine unakuwa hata huna umuhimu nayo ila tu kwa kuwa pesa ipo basi wakuta umefanya.
Ku solve.
Hakikisha unapanga kabla matumizi ya mwezi.
Tenga kiasi kwa ajili ya dharura(kukopesha kutoa kwa rafiki na ndugu). Kiwe fixed hapa mtu atakayekuja baada ya hiyo hela kuishi hapati kitu.
Then jizoeshe kufanya matumizi ya kawaida ndipo utaona pesa yako inabaki.
Hakikisha wewe ndio una i control pesa na si pesa ina ku control wewe.
Pesa ni kama mpira wa miguu ule.Vile unaona mtu anauchezea na ku u control vile atakavyo wakati mwingine anashindwa hata dana dana moja unakuwa umemtoka mguuni.Tatizo linakuwa ni mchezaji na si mpira kwakuwa mpira hauna akili bali mchezaji ambaye anaweza tumia akili yake akaufanya anavyotaka ukatii.
Nb: Nidhamu ya pesa ni muhimu mno hapo