Katika sekta ya ujenzi kuna teknolojia za kisasa zenye ubora na bei nafuu. Ningependa kujua toka kwenu wadau ambao wako sekta ya ujenzi au waliojenga hivi karibuni kuhusu aina ya milango ambayo inayoweza kutumika kwenye nyumba za kuishi (residential house). Wapi ninaweza kupata milango mizuri, imara na kwa gharama nafuu? Asanteni