Ushauri kwa watanzania waishio Afrika Kusini

Ushauri kwa watanzania waishio Afrika Kusini

Habari za jioni wana JF. Nimuombe Mungu azidi kuwajaalieni Afya, riziki, na nguvu zaidi.

Haya twendeni kwenye mada.
Kwa wiki kadhaa sasa SA kumekuwa na wimbi la maandamano sehemu mbalimbali za miji kama JOBURG (JOZ), DEBENI (DURBAN) nk. Maandamano haya wameyaita kwa jina la OPERESHINI DUDULA.

OP hii imelenga kuleta uhuru kamili kwa wazawa, hapa wanadai kuna maeneo hata hao wazawa hawawezi kupita au kwenda au kuingia kisa WAGENI (FOREIGNERS) hasa wasio na vibali (ILLEGALLY). Pamoja na yote haya lkn wameenda mbali sana wakiwashutumu wageni hao kuwa ni WEZI, WAUAJI, NA WANAWANYIMA FURSA ZA AJIRA. Pia wazawa wanadai hata wawapo kwenye vituo vya daladala (TAX RANKS) bado hawako salama, wazamiaji wanamiliki bastola na bunduki na polisi hawafanyi kitu.

Operesheni hiyo ilipaswa kusogea mpaka HILLBROW na hapa ndipo niliposhtuka kidogo.
Mitaa hiyo imejaa Watz sana, huwezi pita hatua ishirini au 50 usisikie kiswahili, (OYAAA), mitaa hii imejaa vijana Masikini wa kitanzania, na wale madon wa SEMBE/NGADA wako kibao pia.

Sasa lengo sio hizo biashara zao, lengo ni vibali vya kuishi.
Namnukuu mmoja wa viongozi wa hiyo DUDULA "Sisi hatujali, kama watakuja kistaarabu tutakuja nao hivyo, na wakija na bunduki tutawakabili kwa bunduki."

Kauli hii inaonesha chuki kubwa juu ya wageni wakijificha kwenye kichaka cha VIBALI vya kuishi.
Kama raia wa SAUZ ana haki kisheria kukagua documents zako?? Kwann wajichukulie sheria mkononi?? Na kwanini wana deal na weusi wenzao tu??

USHAURI
Ndugu zangu WATZ mlioko huko na mnaotarajia kwenda huko, zama zimebadilika, tafuta passport yako, ingia kwa halali, muda wa kustay ukiisha rudi nchi jirani kisha inga tena utagongewa mpakani au lipia VISA uishi kwa amani angalau kidogo.
Sehemu yoyote ukienda kwa halali hata kama hauna ndugu ni rahisi kupata ndugu, tunaona hata hapa mtu kumpokea mhamiaji haramu ni mziki.

Hivyo basi nendeni mkapate passport halali na kama imeisha sogea hapo kwa Balozi wetu hapo PT.
Pia waTZ mnawawekea wenzenu maisha magumu pindi wanapopita mipakani kisa tabia zenu mbovu hasa za kuuza ngada na uhuni wa kifala.

Kama huna shule, fani, mtaji, ndugu au hata kazi maalumu usienda AFRIKA KUSINI.

Nawasilisha.
Wasauz kwa kweli wanahitaji kuondoa wahamiaji haramu hasa wanaijeria(wauza madawa na waendesha biashara ya umalaya uliopitiliza) wazimbabwe(majambazi ynayouwa watu wengi kila kukicha)

Haya mataifa mawili kwa kweli yameharibu vijana wengi ambao ni future ya South Africa.Watanzania wa Hillbrow wengi ni wauza simu za wizi na vikete vya unga- sawa sikatai wapo wauza unga wakubwa kiasi wa Kitanzania South Africa lakini awawafikii Wanaijeria.

WaTZ wengi wanauza Sigara na pipi kwenye mitaa ya hillbrow,Berea na kwenye mjengo wao maharufu wa FLAMINGO .Serikali ya Sauz wapo wanafuata Sheria za haki za Binadamu ,

Vijana wanasema wamechoka wanataka nchi yao , Amakwerekwere out
 
Baadhi ya wa Tz wanaozamia SA huwa wakirudi nawaonaga ni Kama ndo wanazidi kukosa ramani kabisa maana hata wakirudi hawana wanachorudi nacho zaidi ya kujua kusalimia kizulu na kuwa na tabia chafu zaidi ya awali yaan huwa wananifanya nisijute kwenda SA
Badiliken Uhuni wa kishamba hauna nafasi dunia ya sasa sanasana utaharibu Future yako, tujifunze kuwa waaminifu msingi wa chochote unachofanya ni kuweka uaminifu kwanza.
 
Mkuu nipo SA.. mmeisikia hiyo tu ambayo imepenya kwenye vyombo vya habari.. ila ubaguzi nchi hii ni kila siku lazima mgeni anyanyaswe kama sio kuuliwa kabsa awe ni kibaki na hata asiwe na kibaki awe mwizi, muuza ngada au hauzi kiufupi tu jamaa ni wabaguzi ukiacha na hii kuwa wageni wanauza ngada na wezi.. wao wenyewe wezi wapo na wauza ngada pia wapo ila hawadhuriani kisa wazawa kwa kweli ushauri mzuri.. nna miaka minne now unaenda mwaka wa tano hapa napanga ndonga zangu nnapesa ambayo inatosha vibiashara hata nane vya laki nane nane yaani nahakikisha mwezi mtukufu ukiisha InshAAllah narudi home kuja kupiga vibiashara vyangu niangalie upepo.. ila sifanyi biashara haramu nipo dukani mwaka wa tano huu na pia nna share hapa dukani naofia kuiacha nguvu yangu kibure bure ila ntaiacha tu.. maisha ya ugenini ni utumwa sana haswa sisi tuliopo huku.. Daah
Dua tu mimi wenyewe mungu akipenda mwaka huu mwishoni inshallah tunarudi home nshachoka maisha ya stress, unapata pesa kweli, lkn huna Amani, POLISI WANAKUTAMANI, MATEJA WANAKUTAMANI, WAZAWA NDO USISEME., USIKU HULALI KWA RAHA, MCHANA NDO KABISAAAA.
 
Naishi PE.. mtanzania aliye tanzania ambaye ajawahi kuja/kwenda SA anaamini kila mtanzania aliyekuwa huku kuwa hana elimu na kwenye akili yake amejipandikiza kuwa anafanya kazi ya uharifu tu..

Wapo wanaoshona nguo yaani cherehani na hawafanyi mambo ya haramu wapo wanuza maduka na wapo pia wanaouza chakula nk na hawachanganyi biashara zao na madawa au wizi,ujambazi.. na wapo pia wanaofanya mazabe..

Watanzania waliopo bongo wenyewe tu wana chuki na watanzania waliopo SA .. unaona kabsa hizi coments unaona chuki kiasi gani? Inavyopandiana ndio maana wengi wetu tunachelewa sana kufanikiwa..

Hauwezi kumzuia mgeni asikuchukie kwa mfano unafanya biashara mf: duka unapata pesa nyingi na unanunua gari au nyumba SA .. wao wanaajiliwa na wazungu mpaka kupata uhuru wa kifedha ni baadae sana kwa hivyo akikuona na mafanikio automatically chuki inamjaa..

Sema ngoja tuwaachie mtumalize humu mtandaoni pengine roho zenu zinanufaika mkituponda na kutubagua watanzania wenzenu..
Ndugu yangu umeongea kwa uchungu Sana, pole ndo ndugu zetu walivyo, yaani wakiwaona watoto wanarudishwa na dege la umoja,, basi wanaona wote tulipo huku wahuni, hawajui kwamba wengine uko uko bongo wamepanga kwenye nyumba zetu sisi tuliopo huku kutafuta,

Dawa yao tukirudi bongo ni kuwachapia tu Dada zao, si unajua madem wa kibongo wakisikia baharia karudi mtamu
 
Nimekupata kabisa mkuu, tuje kwenye uhalisia WASOUTH AFRICAN hasa BLACKS wamesoma sana? Kwa sababu nimeona kazi kama 101 zimeorozeshwa mwaka huu kama kazi ambazo zinahitaji watu hata wa nje wazifanye, tena maajabu nimeona hadi wahasibu, wakaguzi wa hesabu, mambo kilimo nk.

Kwa ujumla wake miji ipi ni salama kwa foreigners, yaan tuseme sasa una mshauri kijana wa kitanzania ambaye anataka kuja huko, aende mji upi wenye kiwango kidogo ya vurugu (achana na ubaguzi) ambazo tunasikia kesi nyingi za watu kuawa, kuporwa mali, kubakwa, kutekwa na kadhalika.

Pia nilipitia ripoti ya polisi juu ya uhalifu yaani nikaogopa, nchi kwa miezi mitatu ina rekodi visa karibu 7000+ vya mauaji.
Ndugu yangu tatizo sio kusoma au kutokusoma, wasauzi ni wavivu, walevi, kwa hiyo mtu akipokea mshahara wake basi ujue ni party, yani mwisho wa mwezi kila nyumba inakuwa bar, apo ni kuchoma nyama na bia, hela ikiisha wanaenda kukopa
 
Akili mgando

Wauza ngada wapo ila sio wote mkuu fikiria tena

Na tv, simu sijui na vitu vingine vipo vinavyouzwa second end mkuu.. tuliza tena akili utajichanganya.. ukisema vitu vya wizi au wezi wapo/vipo duniani kote fungua uelewa wako..

Sio majambazi wala wauza unga wapo duniani kote .. huku SA watanzania/wageni wajinga wajinga wapo yaani wasiotaka kazi na wafanya kazi pia wapo yaani ni maisha tu kama sehemu yeyote ya dunia wapo wenye vipato vizuri na wasio kuwa navyo..

Watanzania wengi ambao hawapo viwanja wamejawa na chuki na ni wavivu kufikilia.. yaani sitaki kufanya makosa nikirudi ninunue kiwanja nipige hata vyumba vinne vya kawaida then nitulie.. maana binafsi nna jamaa zangu wapatao wanne au watano hawapokei sim zangu wala kujibu sms zangu tangu nisafiri kuja SA na bila sababu yeyote ilee chuki tu wanahisi ntafanikiwa mapema kuliko wao wakati M/Mungu ndio anatoa baraka na neema katika mafanikio..

Punguzeni akili mgando na mioyo ya chuki muwahi kufanikiwa nyie wote wenye chuki..
Nashukuru mungu tumejitokeza kwa wingi sisi tuishio huku, maana zimeshatolewa nyuzi nyingi Sana za kutuponda sisi watafutaji wa South africa
 
Mimi sio msela kwanza, na unaweza ukawa mtoto wangu pia, maana mtoto wa kwanza ana miaka 24 sasa. Mimi ni mtu mzima kabisa mwenye, 1974, so sio kijana kama Unavyonichukulia
Oooh pole sana kaka.
 
Nashukuru mungu tumejitokeza kwa wingi sisi tuishio huku, maana zimeshatolewa nyuzi nyingi Sana za kutuponda sisi watafutaji wa South africa

Mchezo hauwezi kuuelewa mpaka uwe ndani mkuu.. ukiwa nje! Unaweza ukajifanya messi ukiingia ndani magwaya “ Captain wa man-u acha watuponde tu haki yao “ hawajauelewa mchezo siku wakiyavagaa hata kama marekani wataacha kutukana ovyo
 
Ndugu yangu umeongea kwa uchungu Sana, pole ndo ndugu zetu walivyo, yaani wakiwaona watoto wanarudishwa na dege la umoja,, basi wanaona wote tulipo huku wahuni, hawajui kwamba wengine uko uko bongo wamepanga kwenye nyumba zetu sisi tuliopo huku kutafuta, dawa yao tukirudi bongo ni kuwachapia tu Dada zao, si unajua madem wa kibongo wakisikia baharia karudi mtamu

[emoji23][emoji23][emoji23] punguza makali mkuu
 
Dua tu mimi wenyewe mungu akipenda mwaka huu mwishoni inshallah tunarudi home nshachoka maisha ya stress, unapata pesa kweli, lkn huna Amani, POLISI WANAKUTAMANI, MATEJA WANAKUTAMANI, WAZAWA NDO USISEME., USIKU HULALI KWA RAHA, MCHANA NDO KABISAAAA.

Amini mwananga.. muhimu sana nyumbani hata kama hauendi kuishi yaani kila baada ya miaka miwili.. unageuka zako kusoma ramani
 
[emoji23][emoji23][emoji23] punguza makali mkuu
No unajua mda mwingine mwanaume mzima anaanza kuponda watu ambao wamejitoa wako mbali na Familia zao, kutafuta ugari unaanza kuponda ponda, watu wamethubutu,

Sio umekaa sebuleni kwa shemeji unaanza kuponda watu wanalala nje kutafuta riziki, unamuona Hana akili, unaishi nyumba ya kupanga mwenye nyumba humjui we una deposit tu kodi, kumbe unaemtusi jamii forum ndo mwenye nyumba wako. Pambaff
 
No unajua mda mwingine mwanaume mzima anaanza kuponda watu ambao wamejitoa wako mbali na Familia zao, kutafuta ugari unaanza kuponda ponda, watu wamethubutu, sio umekaa sebuleni kwa shemeji unaanza kuponda watu wanalala nje kutafuta riziki, unamuona Hana akili, unaishi nyumba ya kupanga mwenye nyumba humjui we una deposit tu kodi, kumbe unaemtusi jamii forum ndo mwenye nyumba wako. Pambaff

Dawa yao kufanya mafanikio.. tu mwananga wekeza pesa zako mahali husika wekeza tena wekeza tena na tena then fanikiwa sanaa kadri ambavyo mtu akuogope hata kukuongeresha kama haujamuanza wewe kumsemesha alaf basi..
 
Amini mwananga.. muhimu sana nyumbani hata kama hauendi kuishi yaani kila baada ya miaka miwili.. unageuka zako kusoma ramani
Nauli sasa hivi ikoje kutoka Dar to Harare.
 
Akili mgando

Wauza ngada wapo ila sio wote mkuu fikiria tena

Na tv, simu sijui na vitu vingine vipo vinavyouzwa second end mkuu.. tuliza tena akili utajichanganya.. ukisema vitu vya wizi au wezi wapo/vipo duniani kote fungua uelewa wako..

Sio majambazi wala wauza unga wapo duniani kote .. huku SA watanzania/wageni wajinga wajinga wapo yaani wasiotaka kazi na wafanya kazi pia wapo yaani ni maisha tu kama sehemu yeyote ya dunia wapo wenye vipato vizuri na wasio kuwa navyo..

Watanzania wengi ambao hawapo viwanja wamejawa na chuki na ni wavivu kufikilia.. yaani sitaki kufanya makosa nikirudi ninunue kiwanja nipige hata vyumba vinne vya kawaida then nitulie.. maana binafsi nna jamaa zangu wapatao wanne au watano hawapokei sim zangu wala kujibu sms zangu tangu nisafiri kuja SA na bila sababu yeyote ilee chuki tu wanahisi ntafanikiwa mapema kuliko wao wakati M/Mungu ndio anatoa baraka na neema katika mafanikio..

Punguzeni akili mgando na mioyo ya chuki muwahi kufanikiwa nyie wote wenye chuki..
Umeongea ukweli mtupu wabongo wengi wamejawa na roho za husda na mawivu ya kijinga kwa watu walioko nje ya nchi.

Sio SA tu hata walioko ughaibuni wanaitwa majina kama yote wabeba mabox lakini ukiangalia sana ni wivu tu.

Bora wewe utarejea huko bongo kununua kiwanja mie huko bongoland sitaki hata kukusikia kurudi roho mbaya ndio kwake huko.
 
Umeongea ukweli mtupu wabongo wengi wamejawa na roho za husda na mawivu ya kijinga kwa watu walioko nje ya nchi. Sio SA tu hata walioko ughaibuni wanaitwa majina kama yote wabeba mabox lakini ukiangalia sana ni wivu tu. Bora wewe utarejea huko bongo kununua kiwanja mie huko bongoland sitaki hata kukusikia kurudi roho mbaya ndio kwake huko.

Na sijui kwanini? Mfano mzuri fatilia hizo coments kuanzia coment ya kwanza utaona tu yaani wana ubinafsi fulani hivi.. daah maisha haya daah
 
Back
Top Bottom