THE SHADOW ONE
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,228
- 2,036
Nigeria wanatushinda nini ? Sisi ni wajanja wa hapa bongo tunakosoana sisi kwa sisi, hatuthamini vya kwetu.Wanatuaibisha tu huko!
Nigeria wanatushinda nini ? Sisi ni wajanja wa hapa bongo tunakosoana sisi kwa sisi, hatuthamini vya kwetu.Wanatuaibisha tu huko!
Hongera sana mkuuWahuni kweli wapo vitoto vinavyoiba simu za mama zao, kukimbilia South, ndio wanakuja kupata tabu huku, wanakuwa wezi, wanalala nje jorberg uko na miji mingine mikubwa, wanatoka Tanzania Kuja kuangalia free way south, sio kutafuta maisha. Mzee mimi naishi kijijini lkn nashukuru nimeleta Familia yangu watoto wanasoma, mama nimemfungulia salon na biashara ndogo maisha tunayasongesha. Apo nna miaka 3 toka niingie South
Wazawa wenyewe huko wavivuYaan huwa nachukia sana, mtu umeenda nchi za watu afu unafanya ujinga ujinga. Wengi hawana elimu kabisa yaan mtu hata kusoma anabahatisha tu, wanauza vitu vya wizi hadi kero.
Tatizo kubwa asilimia kubwa ya Watz ni wauza ngada na hilo unalijua pia hamna shule hivyo mna usela mavi sana, mnawakaba au kuwaibia waTZ wenzenu
Upo mji gani mkuu? Vp Rate ya uhalifu huko uliko?Mkuu nipo SA.. mmeisikia hiyo tu ambayo imepenya kwenye vyombo vya habari.. ila ubaguzi nchi hii ni kila siku lazima mgeni anyanyaswe kama sio kuuliwa kabsa awe ni kibaki na hata asiwe na kibaki awe mwizi, muuza ngada au hauzi kiufupi tu jamaa ni wabaguzi ukiacha na hii kuwa wageni wanauza ngada na wezi.. wao wenyewe wezi wapo na wauza ngada pia wapo ila hawadhuriani kisa wazawa kwa kweli ushauri mzuri.. nna miaka minne now unaenda mwaka wa tano hapa napanga ndonga zangu nnapesa ambayo inatosha vibiashara hata nane vya laki nane nane yaani nahakikisha mwezi mtukufu ukiisha InshAAllah narudi home kuja kupiga vibiashara vyangu niangalie upepo.. ila sifanyi biashara haramu nipo dukani mwaka wa tano huu na pia nna share hapa dukani naofia kuiacha nguvu yangu kibure bure ila ntaiacha tu.. maisha ya ugenini ni utumwa sana haswa sisi tuliopo huku.. Daah
Tupo nae temeke jamaa karudishwa toka south akachomwa hiyo sindana kwisha habari yakeWatanzania bado tuna ulimbukeni fulani hivi, nafikiri hii inaanza hata wakati wa kutafuta passport.. hii inapaswa kuwa ni haki ya mtu toka anazaliwa kuwa nayo isiwe ni kitu kikubwa sana... watanzania wasijibane hapa bongo kupiga siasa alafu badae siasa zao tena wanazipeleka majuu uvivu mwingi,unafiki,sembe,ukabaji na ujambazi.
Wengi waliorudi kutoka S. Africa niliowaona wamerudi wamedata,wengine mateja na wengine inasemekana eti wamepigwa sindano yakupoteza kumbu kumbu?? Wachache ndiyo hao kina Mswazi wamerudi wako super.
Upo mji gani mkuu? Vp Rate ya uhalifu huko uliko??
Unaweza kutujulisha ni sehemu zipi ambazo kuna watz wastaarabu? Binafsi watu kutoka Tanga na Zanzibar na kidogo Moshi wengi wao sio wakorofi.
Sema sijajua kwa Joz wanaishi mitaa ipi. Hao jamaa ni rahisi kuwasaidia wenzao.
Dah pole sana, shida wengi ndio huwa na tabia mbovu, tuliowahi kufika tunajua wapo wasomi pia. Sema wasouth wana kitu wanaita Critical skills yaan kuna kada ukienda unapata kibali cha kufanya kazi halali.Naishi PE.. mtanzania aliye tanzania ambaye ajawahi kuja/kwenda SA anaamini kila mtanzania aliyekuwa huku kuwa hana elimu na kwenye akili yake amejipandikiza kuwa anafanya kazi ya uharifu tu..
Wapo wanaoshona nguo yaani cherehani na hawafanyi mambo ya haramu wapo wanuza maduka na wapo pia wanaouza chakula nk na hawachanganyi biashara zao na madawa au wizi,ujambazi.. na wapo pia wanaofanya mazabe..
Watanzania waliopo bongo wenyewe tu wana chuki na watanzania waliopo SA .. unaona kabsa hizi coments unaona chuki kiasi gani? Inavyopandiana ndio maana wengi wetu tunachelewa sana kufanikiwa..
Hauwezi kumzuia mgeni asikuchukie kwa mfano unafanya biashara mf: duka unapata pesa nyingi na unanunua gari au nyumba SA .. wao wanaajiliwa na wazungu mpaka kupata uhuru wa kifedha ni baadae sana kwa hivyo akikuona na mafanikio automatically chuki inamjaa..
Sema ngoja tuwaachie mtumalize humu mtandaoni pengine roho zenu zinanufaika mkituponda na kutubagua watanzania wenzenu..
Dah pole sana, shida wengi ndio huwa na tabia mbovu, tuliowahi kufika tunajua wapo wasomi pia. Sema wasouth wana kitu wanaita Critical skills yaan kuna kada ukienda unapata kibali cha kufanya kazi halali.
Nikutakieni kila lenye kheri ndugy zetu. Maana nimeona leo hii wageni kibao hawajulikani walipo kutokana na operesheni DUDULA.
Binafsi kama ningekuwa Rais nchi hii, basi ningepeleka ndege za jeshi 3 zikawachukue raia wetu wanaotaka kurudi nyumbani na tena bila masharti.
Nimekupata kabisa mkuu, tuje kwenye uhalisia WASOUTH AFRICAN hasa BLACKS wamesoma sana? Kwa sababu nimeona kazi kama 101 zimeorozeshwa mwaka huu kama kazi ambazo zinahitaji watu hata wa nje wazifanye, tena maajabu nimeona hadi wahasibu, wakaguzi wa hesabu, mambo kilimo nk.Hakuna atayekubali mkuu kama itakuwa ni hiari kwa kuwa watu wana familia zao wamezaa na wenyeji kikubwa zaidi wana mali zao nyingi zikiwemo biashara kubwa yaani nnavyokwambia kuna wengine wana biashara za kuuza magari na wanauza kihalali tu sema wazawa kwa wivu wanawapakazia kuwa ni wauza dawa ili wawatimue wachukie mali zao
Nimekupata kabisa mkuu, tuje kwenye uhalisia WASOUTH AFRICAN hasa BLACKS wamesoma sana? Kwa sababu nimeona kazi kama 101 zimeorozeshwa mwaka huu kama kazi ambazo zinahitaji watu hata wa nje wazifanye, tena maajabu nimeona hadi wahasibu, wakaguzi wa hesabu, mambo kilimo nk.
Kwa ujumla wake miji ipi ni salama kwa foreigners, yaan tuseme sasa una mshauri kijana wa kitanzania ambaye anataka kuja huko, aende mji upi wenye kiwango kidogo ya vurugu (achana na ubaguzi) ambazo tunasikia kesi nyingi za watu kuawa, kuporwa mali, kubakwa, kutekwa na kadhalika.
Pia nilipitia ripoti ya polisi juu ya uhalifu yaani nikaogopa, nchi kwa miezi mitatu ina rekodi visa karibu 7000+ vya mauaji.
huko S.A sio mgeni ila ukweli mchungu tu.
kwa nini tufiche ukweli.asilimia 95 ya watanzania wawe na vibali,wasiwe na vibali,matajiri na maskini hiyo asilimia wote ni blackmarket .
blackmarket yenyewe ni unga,biashara haramu kama vitu vya wizi,ujambazi,mambo ambayo tanzania ni dakika chache wangeshakuwa gerezani.
Tunafichana na wengine wapo hapa tz wanajifanya wanageresha ya biashara na mmoja sitopenda kumtaja au kuwataja ila huko s.a biashara yake ndio ganda.
S.a ilikuwa miaka mwisho 2010 naweza kusema kushuka chini,wimbi la waamiaji ni kubwa sana na kupelekea hata fursa hakuna na watu kuingia kwenye biashara wasizotegemea.
Ukisikia simu ,laptop,tv,magari zimetoka s.a we jua 91% ya wizi .
watanzania waliopo huko walisha badilika roho kutokana na sheria sio za kwao na uhuru ambao anaweza kufanya kosa na kuondoka.
Alafu ni sisi pia tukirudi na rand zetu tunachukua Dada zenu, na wake zenu wanatushobokea wanaume tumetoka kutafuta.