Ushauri kwa watanzania waishio Afrika Kusini

Ushauri kwa watanzania waishio Afrika Kusini

CARDLESS

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2017
Posts
7,868
Reaction score
16,005
Habari za jioni wana JF. Nimuombe Mungu azidi kuwajaalieni Afya, riziki, na nguvu zaidi.

Haya twendeni kwenye mada.
Kwa wiki kadhaa sasa SA kumekuwa na wimbi la maandamano sehemu mbalimbali za miji kama JOBURG (JOZ), DEBENI (DURBAN) nk. Maandamano haya wameyaita kwa jina la OPERESHINI DUDULA.

OP hii imelenga kuleta uhuru kamili kwa wazawa, hapa wanadai kuna maeneo hata hao wazawa hawawezi kupita au kwenda au kuingia kisa WAGENI (FOREIGNERS) hasa wasio na vibali (ILLEGALLY). Pamoja na yote haya lkn wameenda mbali sana wakiwashutumu wageni hao kuwa ni WEZI, WAUAJI, NA WANAWANYIMA FURSA ZA AJIRA. Pia wazawa wanadai hata wawapo kwenye vituo vya daladala (TAX RANKS) bado hawako salama, wazamiaji wanamiliki bastola na bunduki na polisi hawafanyi kitu.

Operesheni hiyo ilipaswa kusogea mpaka HILLBROW na hapa ndipo niliposhtuka kidogo.
Mitaa hiyo imejaa Watz sana, huwezi pita hatua ishirini au 50 usisikie kiswahili, (OYAAA), mitaa hii imejaa vijana Masikini wa kitanzania, na wale madon wa SEMBE/NGADA wako kibao pia.

Sasa lengo sio hizo biashara zao, lengo ni vibali vya kuishi.
Namnukuu mmoja wa viongozi wa hiyo DUDULA "Sisi hatujali, kama watakuja kistaarabu tutakuja nao hivyo, na wakija na bunduki tutawakabili kwa bunduki."

Kauli hii inaonesha chuki kubwa juu ya wageni wakijificha kwenye kichaka cha VIBALI vya kuishi.
Kama raia wa SAUZ ana haki kisheria kukagua documents zako?? Kwann wajichukulie sheria mkononi?? Na kwanini wana deal na weusi wenzao tu??

USHAURI
Ndugu zangu WATZ mlioko huko na mnaotarajia kwenda huko, zama zimebadilika, tafuta passport yako, ingia kwa halali, muda wa kustay ukiisha rudi nchi jirani kisha inga tena utagongewa mpakani au lipia VISA uishi kwa amani angalau kidogo.
Sehemu yoyote ukienda kwa halali hata kama hauna ndugu ni rahisi kupata ndugu, tunaona hata hapa mtu kumpokea mhamiaji haramu ni mziki.

Hivyo basi nendeni mkapate passport halali na kama imeisha sogea hapo kwa Balozi wetu hapo PT.
Pia waTZ mnawawekea wenzenu maisha magumu pindi wanapopita mipakani kisa tabia zenu mbovu hasa za kuuza ngada na uhuni wa kifala.

Kama huna shule, fani, mtaji, ndugu au hata kazi maalumu usiende AFRIKA KUSINI.

Nawasilisha.
 
Kuna mshkaji iliwai kukaa huko miaka kumi hana mbele wala nyuma.

karudi bongo hana kitu zaidi ya mapicha mapicha tu ya huko.

kakaa hapa miaka miwili akapewa fursa ya kuchanga hela watu watatu au zaidi kisha mnaagiza lonya za china mnauza,sasahivi anamaliki mijengo yake kausafiri kakiani kakulia bata basi maisha yanakwenda.
 
Dah mnatudharirisha Sana sisi tuopo huku, lkn kwani uko bongo Hakuna masela?Hakuna wauza Unga? Hakuna wanaobagua wageni? Wengine tuna Familia mjue uku na tunaishi vzr tu Sana, na tuna biashara za halali.
Tatizo kubwa asilimia kubwa ya Watz ni wauza ngada na hilo unalijua pia hamna shule hivyo mna usela mavi sana, mnawakaba au kuwaibia waTZ wenzenu
 
Kwa hiyo uko tz Hakuna wauza ngada? na Hakuna wakabaji?
Iko hivi, mnavyokutana nje ya nchi yenu basi hakikisheni mnakuwa ndugu, mnasaidiana bila kujali mtu anatokea mkoa gani wala nn.

Shida yetu waTz hatuwezi watetea wenzetu pindi wapatapo matatizo tuwapo ugenini. Tunategemea tuwapo huko tuwacheck tunakaa kama ndugu tunakula na kunywa na kubadilishana mawazo na ikibidi tuweze kupanga namna gani tunasaidiana kama waTanzania.

Niliwahi kufika huko, nikakutana na Watz yaan hali mbaya, nakumbuka kuna dogo mmoja alikuwa na shida ya Nauli, nilimbeba yule dogo mpaka TZ.

Tuwe na ushirikiano tuwapo nje, tusaidiane, tushikamane, tuteteane pale ambapo tunaona kabisa mwenzetu anaonewa au kupata matatizo hata ya kiserikali.
 
Iko hivi, mnavyokutana nje ya nchi yenu basi hakikisheni mnakuwa ndugu, mnasaidiana bila kujali mtu anatokea mkoa gani wala nn. Shida yetu waTz hatuwezi watetea wenzetu pindi wapatapo matatizo tuwapo ugenini. Tunategemea tuwapo huko tuwacheck tunakaa kama ndugu tunakula na kunywa na kubadilishana mawazo na ikibidi tuweze kupanga namna gani tunadaidiana kama waTanzania.

Niliwahi kufika huko, nikakutana na Watz yaan hali mbaya, nakumbuka kuna dogo mmoja alikuwa na shida ya Nauli, nilimbeba yule dogo mpaka TZ.
Tuwe na ushirikiano tuwapo nje, tusaidiane, tushikamane, tuteteane pale ambapo tunaona kabisa mwenzetu anaonewa au kupata matatizo hata ya kiserikali.
Sasa ilo la kukosa nauli, uyo muongo, watoto kibao wanozurula ovyo joz na miji mingine mikubwa huwa tunawatudisha kwa kuwachangia, wengine sio waaminifu wanakimbia, wengine hawataki wenyewe kurudi bongo.

Wabongo wangapi wanakufa wanarudishwa bongo kwa michango yetu? Ukiona maiti imetoka South ujue imechangiwa mpaka kurudishwa.

Na tunashirikana vzr Sana, na tuna Chama chetu kinaitwa TACOSA, em Google kidogo upate Habari zake. Hao wahuni wahuni wengine usichukulie kwamba ndio woote.
 
Back
Top Bottom