Ushauri kwa Wasafi Classic Babies (WCB)

Ushauri kwa Wasafi Classic Babies (WCB)

Maelau

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
1,365
Reaction score
1,343
Ni hivi, kama wanamuziki wa wasafi wanapitia humu naomba wabadilike kama wanataka kuendelea kushindana katika nyanja za muziki.

Hawa jamaa wamekuwa wakijaribu kuimba live katika show zao za hivi karibuni, mfano Kenya na Oman.

Uzoefu unaonesha kwamba wanashindwa kabisa kuimba na kujikuta wakija na sauti za ajabu kabisa zinazopoteza radha ya nyimbo na show zao kabisa.

Sababu kubwa ninayoiona ni wao kuwa na mihemuko mikubwa (kupagawa)mbele ya mashabiki. Hali hii inawanyima utulivu wa kuja na sauti nzuri ya wimbo husika na kujikuta wakiimba fyongo kabisa.

Sasa hilo ni moja. La pili, ni tabia yao iliyoshamiri ya kusimamishasimamisha wimbo( mziki) kwa minajiri ya kuwaimbisha watazamaji. Hii kitu huharibu kabisa mtiririko wa melodi za muziki na kujikuta wakiwachosha na kuwaboa mashabiki wao.

Tafadhali badilikeni!!!!!!!
 
Yani wewe naamini kabisa hujui muziki hata kidogo, Muziki wa live unahitaji sauti nzuri?? Msikilize Babylon bayser anavyoimba live na anavyoamsha kwa sauti wewe unayoiita mbovu.

Kina Eminem, Dbanj, Casper nyovest, K.O n.k unawajua niliowataja?
Najua unataka waimbe kama Ruby sasa nakupa ushauri kashawish sponsors waandae tamasha Muscat mumpeleke Ruby mkipata 10 watu nahama duniani
 
RUBY ni level nyngne bro, juzi kwenye malkia wa nguvu kaimba nyimbo zake nikaona kama zinakua nzuri zaidi akiimba live zaid hata ya nyimbo ikipigwa redioni

jamani ruby umfananishe na diamond?

mziki wa ruby unasikilizwa tanzania tu . hauziki nje ya nchi
 
Kwanini asisikilizike?
Hawezi kupata wafuasi hata kidogo promoter atapata hasara, huko kuna waimba cover matata sana hata akienda nairobi hawezi Nandy unaemuona wewe anafanya kazi na willy paul hana hata fan base kubwa kama aliyinayo matonya hukohuko kwao.

Nyimbo anazoimba Ruby ni feelings songs zinahitaji angalau uelewa mdogo nani atamuelewa kule??

Back to WCB wanafanya nyimbo za aina mbili za E.A na internationally, mtu kama Rin marii anaimba mpaka anakera lakini tatizo aina ya muziki anaofanya unamfanya abaki hapahapa.

Mchukue Ruby wako mpeleke samora akaimbe live watu wanaumwa ghafla wanatamani ashuke wanataka amsha amsha tu
 
Yani wewe naamini kabisa hujui muziki hata kidogo, Muziki wa live unahitaji sauti nzuri?? Msikilize Babylon bayser anavyoimba live na anavyoamsha kwa sauti wewe unayoiita mbovu.

Kina Eminem, Dbanj, Casper nyovest, K.O n.k unawajua niliowataja?
Najua unataka waimbe kama Ruby sasa nakupa ushauri kashawish sponsors waandae tamasha Muscat mumpeleke Ruby mkipata 10 watu nahama duniani
Ten people's,😂😂😂 kwekwekwekwe🤣🤣🤣
 
Vipi hili nalo la kusimamisha ala za muziki na kuanza kuwafundisha mashabiki kuimba kila mara?
 
Vipi hili nalo la kusimamisha ala za muziki na kuanza kuwafundisha mashabiki kuimba kila mara?
Wow! swali zuri tunakuza lugha yetu adhimu mzee, ili msanii atambue anachokiimbaga kinawafikia watu wengi lazima afanye hivyo wiki iliyopita ariana grande alikuwa na show huko kwao alifanya hivyohivyo mfatilie IG uone
 
Mmmh! nahisi wewe waweza kuwa mmojawapo wa hao WCB kwa jinsi unavyojenga na kutetea hoja. Je unadhani watu wanafurahia hilo? Mtu kalipia elfu kumi kwa mfano kuja kuimbishwa tu kweli? Ulifuatilia show za wasafi kule Kenya ukaona yale malalamiko ya mashabiki?
 
Mashabiki Nairobi hawakupata kile walichokitarajia kutoka kwa Simba ila Mombasa walikipata!

Nairobi mboso aliuwa sanaa aliimba flashback na wanavyompenda ndo kama akawatia chachandu, Simba kuna baadhi ya nyimbo alitumia Flashback kama kwangwaru na Katika hawajamzoea hivyo!

Ngoja nikupe kamfano kazuri mkubwa alikuja Davido bongo mwaka jana uliona alichokifanya?? Laiti angewaimbia hivyo walala hoi aiseee angetukanwa sana ila kwakuwa aliwaimbia wenye fedha zao hakukuwa na tabu tusubiri show ya korea.
 
Na tabia ya kusema piga keleleeeeeeeee nayo inakera. Mara Mbwembwe Nyingi mashabiki hawapendi. wanapenda show mwanzo mpaka mwisho
 
Na tabia ya kusema piga keleleeeeeeeee nayo inakera. Mara Mbwembwe Nyingi mashabiki hawapendi. wanapenda show mwanzo mpaka mwisho
Ni kweli lakini hawa jamaa pamoja na kushauriwa kwenye page zao za instagram na YouTube hawataki kubadilika sijui kwa nini.
 
Back
Top Bottom