Ni hivi, kama wanamuziki wa wasafi wanapitia humu naomba wabadilike kama wanataka kuendelea kushindana katika nyanja za muziki. Hawa jamaa wamekuwa wakijaribu kuimba live katika show zao za hivi karibuni, mfano Kenya na Oman. Uzoefu unaonesha kwamba wanashindwa kabisa kuimba na kujikuta wakija na sauti za ajabu kabisa zinazopoteza radha ya nyimbo na show zao kabisa. Sababu kubwa ninayoiona ni wao kuwa na mihemuko mikubwa (kupagawa)mbele ya mashabiki. Hali hii inawanyima utulivu wa kuja na sauti nzuri ya wimbo husika na kujikuta wakiimba fyongo kabisa. Sasa hilo ni moja. La pili, ni tabia yao iliyoshamiri ya kusimamishasimamisha wimbo( mziki) kwa minajiri ya kuwaimbisha watazamaji. Hii kitu huharibu kabisa mtiririko wa melodi za muziki na kujikuta wakiwachosha na kuwaboa mashabiki wao. Tafadhali badilikeni!!!!!!!