Ushauri kwa wanawake wenzangu wa JF

LadyAJ

JF-Expert Member
Oct 21, 2015
7,173
9,641
Siku za karibuni kumeibuka thread nyingi sana zenye aidha kuponda au kukashifu wanawake, ninachoweza kusema ni kwamba hazinifurahishi lakini hazinifanyi nichukie maana najua ni mapungufu yaliyotokana na makuzi Duni ya baadhi ya wanaume ambao wao hudhani kumuumiza na kumfadhaisha mwanamke ndio furaha pekee waliyoibakisha.

Sipingi kua hata sisi wanawake baadhi yetu tumekua tukiongea vibaya juu ya wanaume ila ni ukweli pia viungo vyetu vya mwili vimepunguzwa thamani kubwa humu JF kwa maana haipiti siku bila ya kuzungumziwa kua vinanuka, vikubwa kama bwawa, vichafu n.k na kila avizungumziaye hutoa reference ya mpenzi/wapenzi wake.

Wanawake hatukatai ushauri, tunaomba kama kuna ulazima wa kuvingumzia basi mnapovizungumzia mvizungumzie katika namna ya ushauri ili sasa mtu mwenye hali ya kufanana na hiyo au vyovyote vile apate faraja na maana nzima ya MMU na si kejeli, matusi na kushutumiwa, hapo awali niliamini ndani ya MMU kuna Mpenzi, Mahusiano na urafiki ambavyo huzaa upendo lakini kadri siku zinavyozidi kwenda naiona MMU ya migogoro na ukosefu wa amani ya moyo miongoni mwa wafuatiliaji. Hakika hili si jambo zuri.

******** USHAURI WANGU********
1. Wakina mama wenzangu na akina Dada wote wa JF nawashauri tuwe wavumilivu maana Mwanamke ni jalala kila jambo baya hutupiwa yeye, sisi ni ngazi tunatumika kuwaweka wanaume juu huku sisi tukisalia pale pale na kwa bahati mbaya wakifika juu uwezekano wa kukumbuka kuipandisha ngazi pia iliyomfikisha hapo ni finyu sana, zaidi zaidi ataitia teke ili wengine wasipande.

2.Tuache kubishana nao, kadri tunavyojibishana na watoa thread zinazotuweka katika hali ya kudharirika ndivyo tunavyozidi kuchochea kuni za kibuli chao, hivyo ni vyema sasa tukaacha kuchangia Uzi wowote wa aina hiyo, kumbuka " jibu la mjinga ni kimya ". Naamini tukikaa kimya hawatapata tension yoyote ya kurumbana na Ku attack some girls ambao wanaonyesha kuto kukubaliana na mtoa post

3.Nawasukuru sana wanaume wote na nawasisitiza kina mama wenzangu tuzidi kuwaombea, tuwaombee hebu fikiri kizazi tulicho nacho kipo hivi je kijacho kitakuaje? Ni muda sasa umefika wa kukaza mikanda na kuiarisha malezi ya watoto wetu, maana bila shaka hawa wachache hawa wanasadifu malezi Duni waliyoyapata katika ukuaji wao na kifikia hatua kuanika kiungo cha mwanamke kama waanikavyo nguo juu ya kwamba.

Wa Allaahu A’alam.
 
Na mimi naruhusiwa kuchangia au ....

Menichekesha sana

humu kila mtu anatumia id fake na hakuna mpango wa kujuana na mtu yeyote. ila ukianzisha mada hapa kuna wengine wanafuka volkano ya oldonyoo lengai

embu mjirekebishe bwana kama mtu katoa mada ya kujirekebisha, jirekebisheni kimya kimya na mshukurru mmeambiwa ukweli

leo wakitkea wakakuambia wewe mzuri, una chura, sijui mnato kwwa nini msikasirike kwa nini mnasifiwa na mkaanzisha mada kwa nini mnatusifia sana na sisi

mwisho wa siku mtasema tunawataka pyeeee zenu mbadilike muache drama za bongo muvi

anyway kumbe inawahusu wanawake ila msitubague tunaingia popote pale
alahhhhh mxiuuuuuuu
 
Waliowengi huwa wanaongea tu!
Kumbe huwa mnachukulia siriaz kiasi hicho!
Kwa uelewa tu hakuna mwanamke au mwanaume aliyekamilika kiasi cha kukosoa upande mwingine!
Tulio wengi tunatake advantage ya fake I'd kuelekeza mashambulizi upande mwingine though bado ukimfuatilia unakuta nae anamapungufu kibao!

So ladies take it easy
 
Story not balanced. Ni vema ukawaonya sana wamama vile wanavyowatukana wanaume kuwa ni mario, sijui vibamia wakikohoa tu kinachomoka nk. Hiyo kitu umegusia kidoooogo sana.

Hata hivyo nakuunga mkono tuwaheshimu wamama na maumbile yao, tusitukane uumbaji. The same should apply to women as against men
 
Waliowengi huwa wanaongea tu!
Kumbe huwa mnachukulia siriaz kiasi hicho!
Kwa uelewa tu hakuna mwanamke au mwanaume aliyekamilika kiasi cha kukosoa upande mwingine!
Tulio wengi tunatake advantage ya fake I'd kuelekeza mashambulizi upande mwingine though bado ukimfuatilia unakuta nae anamapungufu kibao!

So ladies take it easy


Si suala la kuongea tu, kimtokacho mtu ndio kilichopo moyoni. So wanavyoongea mengi ni uhalisia wao.
 
Back
Top Bottom