Ushauri kwa waliochaguliwa UDOM

Ushauri kwa waliochaguliwa UDOM

Joining Instructions, kuna sehemu kwenye website ya UDOM imeandikwa ALIS, Not Aris. hiyo ni admission letter information system. Kwa sasa hawajairuhusu. Kama sijasahau sana pindi wakiifungua, Utaingia hapo, utaandika jina lako na index number ya form 4. itakutambua na itaifungua barua yako.Utaidownload, Utaiprint na utaijaza. Kama wewe haupo kwenye database ina maana haitakutambua. Kwa sasa bado hawajaachia hiyo system. Tembeleeni hapo mara kwa mara. Ila pia yaweza wakabadili mfumo mwaka huu na naomba nisiisemee Udom kuhusu ALIS kwani mambo yote yanaweza kubadilika muda wowote.
 
King postyako imenikumbusha mbali sana, Ushawahi kuishi ndani ya rum ya wanamume 4 na jinsia KE ndani ya semista nzima? Au wanawake 4na Me 1 hata wiki moja tu? Eeeh Mungu tunakuomba uwasamehe waja wako kwani hawajui wayatendayo= nahisi hii ndio itakuwa kauli mbiu yako utakapoyakuta!

mungu atatusaidia
 
Joining Instructions, kuna sehemu kwenye website ya UDOM imeandikwa ALIS, Not Aris. hiyo ni admission letter information system. Kwa sasa hawajairuhusu. Kama sijasahau sana pindi wakiifungua, Utaingia hapo, utaandika jina lako na index number ya form 4. itakutambua na itaifungua barua yako.Utaidownload, Utaiprint na utaijaza. Kama wewe haupo kwenye database ina maana haitakutambua. Kwa sasa bado hawajaachia hiyo system. Tembeleeni hapo mara kwa mara. Ila pia yaweza wakabadili mfumo mwaka huu na naomba nisiisemee Udom kuhusu ALIS kwani mambo yote yanaweza kubadilika muda wowote.

makole vp inakuwaje kuhusiana na misosi, ya huko mjengoni inaridhisha au akina mama ntilie wapo na je kwa makisio kwa siku msosi unaharimu kiasi gani?
 
Ushauri mzuri sana huu. Umesahau wale walozoea kufungiwa magetini na kuhesabiwa wakirudi toka outing, hapa ni uhuru binafsi lakini angalia uhuru bila mipaka utawasababishia matatizo makubwa ya kiroho na kimwili!
 
Jamani Mungu wangu wa mbinguni huyu anayehubiriwa kila mahali awabariki kwa kukumbuka swala zuri la kutoa hadhari kwa wale wanaokwenda UDOM mwaka huu wa masomo. Wasiwasi yangu ni kwamba huku ndani tunao wach2he maana wengi wanafikiri kutumia internet ni kwa wanachuo tu. Tutawasaidiaje hapa? Mnaonaje hizi post tukazipeleka hata facebook kwani huko wanaweza wakawepo?
 
daah thats usefull infos....ungewaambia vijana KUHUSU USALAMA WA MALI ZAO CHUO/WIZI WA LAPTOPS/SIMU/MAVAZI/PESA MABWENINI na mazingira ya chuo₪₪Makole
 
makole vp inakuwaje kuhusiana na misosi, ya huko mjengoni inaridhisha au akina mama ntilie wapo na je kwa makisio kwa siku msosi unaharimu kiasi gani?

Gharama ya msosi inategemea uko college gani na wewe mwenyewe unatumiaje pesa. Kwa msosi, sehemu ambayo wapo mama nijazie maarufu kama wajasi gharama inakuwa ndogo na misosi inaridhisha. Wakina mama hao ni msaada mkubwa sana kwani hata wakati ule wa Kuishiwa wao wanaweza kukupa huduma, kwani wanakuwa tayari wanakufahamu. Mara nyingi unatakiwa uwe unafahamika mahali maalum hivyo ukiishiwa inakuwa rahisi. Wengine wakati huo wa mwambo ukifika wanachukua vitambulisho vya chuo then wanatoa huduma bure na mkipata pesa mnawarudishia. Vilevile wengine wanapokea bili ya mwezi, miezi au hata semista, hivyo wewe unakula tu mpaka hapo bili itakapoisha. Kwa college ambazo hakuna mama ntilie hawa hawana budi kula kwa mwarabu (cafe nyingi zinamilikiwa na waarabu) Hao hawana sound kwani kila kitu kimeratibiwa. Hata bili zipo lakini misosi kwa kweli si ya kuridhisha ki vile. Hapo bei inategemea na ubora wa chakula. Misosi mingi inaanzia buku-2500. inategemea umetoka familia gani
 
daah thats usefull infos....ungewaambia vijana KUHUSU USALAMA WA MALI ZAO CHUO/WIZI WA LAPTOPS/SIMU/MAVAZI/PESA MABWENINI na mazingira ya chuo₪₪Makole

Tayari niliwaeleza, usimwamini mtu. Kuna nwakati hasa wakukaribia kufunga chuo nguo na viatu vinapigwa sana, Ukifua nguo ukianika kizembe umepigwa. Kuhusu simu na Laptop epuka kuacha mlango wazi. Pia kuna watu wanauza biashara vyumbani, kuweni makini nao. Yawezekana mwenzenu room akatoka asubuhi sana na hajafunga mlango. Wengine wote mkawa mmelala, akiingia muuza chapati ( Yawezekana akawa mtu yoyote) akakuta simu na laptop zipo mezani, atagonga hodi mara mbili kuwasikilizia then kama hamjastuka anapiga simu au lapper then anatembea. Take care guyz
 
Ushauri mzuri sana huu. Umesahau wale walozoea kufungiwa magetini na kuhesabiwa wakirudi toka outing, hapa ni uhuru binafsi lakini angalia uhuru bila mipaka utawasababishia matatizo makubwa ya kiroho na kimwili!

Wana tabu kubwa hawa watu, huko wanakamatwa na kuchinjwa kama kuku wa sherehe, yaani ni kama wanazinduka usingizini hivi
 
Nitakushangaa wewe unaetoka kijijini, wazazi na ndugu wote wanakutegemea wewe, nyumbani hata umeme bado haujafika, unafika chuo. Kwa kuwa tu unakutan ana wanarum wenzako wanamiliki readio kubwa, sub woofers, pamba za hatareee, na anasa nyingine, nawe ukajiona ni muda muafaka wa kujivinjari, pamoja na kwamba sio vibaya lakini mwisho wa semista vitu hivyo ni lazima uviuze kwa bei ya hasara kwa maana huna pa kuvipeleka.

Kuna tabia pia ya kusalimisha ATM kadi kwa wanadada, hili linafanywa na baadhi ya wanaume ambao ni malimbukeni. Wanawake wako kwa ajili ya huduma tu. hawana la maana la kusaidia. Mara nyingi posho ya bodi ikitoka ndio wanakomaa sana na wewe wakijua utagharamia maisha yake. yeye akaunti yake ianasoma wewe yako inashuka. Pia kumbuka nao wanakategorize kama kawaida. Utakuwepo wewe wa vocha, yupo wa starehe na yupo wa misosi. Yupo wa msalato ( Mnada wa nyama kila jumamosi) yupo wa vipodozi. Hivo mtajikuta mko wengi mnahudumia mwanamke mmoja.

Wapo wale ambao, ukinunua music, laptop au tv, wanalazimisha uwape wakae nazo wao. kwa mapenzi yako kwake ukampa akae navyo. take care brother, itakula kwa wewe.

Kwa wale wadada, Wapo wanaume wanakuhadaa watakuoa. Wakaka hao mara nyingi wanawarubuni watumishi (ma-inservice) Lengo lao ni kula mishahara yao tu na mwisho wa siku atakutema, ombea asikuache na mimba.
 
Mkuu MAKOLE vipi TV zinaruhusiwa I mean Unaruhusiwa kumiliki TV in campus?? maana naona umeongelea suala la kununua Electronics, Pia Kama College of Earth Science ikiwa imekamilika Tutapanda daladala za kuelekea wapi??
Kitu kingine kunamdau alileta mada humujamvini kuhusu usajiri kufanyika uwanja wa jamuhuri, je unaliongeleaje Hilo?
 
Last edited by a moderator:
Gharama ya msosi inategemea uko college gani na wewe mwenyewe unatumiaje pesa. Kwa msosi, sehemu ambayo wapo mama nijazie maarufu kama wajasi gharama inakuwa ndogo na misosi inaridhisha. Wakina mama hao ni msaada mkubwa sana kwani hata wakati ule wa Kuishiwa wao wanaweza kukupa huduma, kwani wanakuwa tayari wanakufahamu. Mara nyingi unatakiwa uwe unafahamika mahali maalum hivyo ukiishiwa inakuwa rahisi. Wengine wakati huo wa mwambo ukifika wanachukua vitambulisho vya chuo then wanatoa huduma bure na mkipata pesa mnawarudishia. Vilevile wengine wanapokea bili ya mwezi, miezi au hata semista, hivyo wewe unakula tu mpaka hapo bili itakapoisha. Kwa college ambazo hakuna mama ntilie hawa hawana budi kula kwa mwarabu (cafe nyingi zinamilikiwa na waarabu) Hao hawana sound kwani kila kitu kimeratibiwa. Hata bili zipo lakini misosi kwa kweli si ya kuridhisha ki vile. Hapo bei inategemea na ubora wa chakula. Misosi mingi inaanzia buku-2500. inategemea umetoka familia gani

ahsante Makole but ningependa kufahamu sisi wa hostel za social science ao wajasi wapo na kwa ao akina mamantiliye harama za msosi kwa wao ni sh ngapi?
 
Mkuu MAKOLE vipi TV zinaruhusiwa I mean Unaruhusiwa kumiliki TV in campus?? maana naona umeongelea suala la kununua Electronics, Pia Kama College of Earth Science ikiwa imekamilika Tutapanda daladala za kuelekea wapi??
Kitu kingine kunamdau alileta mada humujamvini kuhusu usajiri kufanyika uwanja wa jamuhuri, je unaliongeleaje Hilo?

Mara nyingi usajili uwanja wa jamhuri unafanyika kwa mwaka 2 na kuendelea, nao pia inategemea huenda wakabadili mfumo. refreshers husajiliwa kwenye college zao, ingawa pia taratibu zaweza kubadilishwa. Umiliki wa TV unaruhusiwa ingawa baadhi tu ya college ndio unaweza kushika tbc na vitu vingine. Zaidi labda utumie tu kwa kuangalia cd. Hakuruhusiwi kuweka dishi wala antena, hiyo ni marufuku. Kwa COED hakuna ACCES ya tv, kwa maana ya kwamba hutaangalia channel zozote. ingawa pia inategemea, kwa wanaoishi gorofa za juu hapo coed wanapata TBC. hii ni kwa sababu ya location ya college. Unaruhusiwa kumiliki vifaa visivyozidi 13 amps. Zaidi ya hapo circuit breaker inakata na hivyo flooor nzima inakosa power.

Earth science utalazimika kupanda daladala zinazokwenda College of Education, kwa wakati huu hata hapo itakapokamilika utalazimika kufanya hivyo.
 
ahsante Makole but ningependa kufahamu sisi wa hostel za social science ao wajasi wapo na kwa ao akina mamantiliye harama za msosi kwa wao ni sh ngapi?

Social science kama wajasi wapo basi wako mbali sana, nna uhakika hapo hakuna wajasi. Kuna wakati fulani nilikuwa nawaona watu wa Social wakiagiziana misosi kutoka coed, Hii si kawaida sana na hutokea wakati viazi vikiwa vingi na mara nyingi mifuko ya watu hapo inakuwa tupu. Walichokuwa wamewekeana ni zamu kwa vyumba. Kila chumba kina zamu yake maalum ya kufuata viazi Ng'ong'ona (COED) huu ni wakati mgumu sana kwa wanafunzi.
 
Mara nyingi usajili uwanja wa jamhuri unafanyika kwa mwaka 2 na kuendelea, nao pia inategemea huenda wakabadili mfumo. refreshers husajiliwa kwenye college zao, ingawa pia taratibu zaweza kubadilishwa. Umiliki wa TV unaruhusiwa ingawa baadhi tu ya college ndio unaweza kushika tbc na vitu vingine. Zaidi labda utumie tu kwa kuangalia cd. Hakuruhusiwi kuweka dishi wala antena, hiyo ni marufuku. Kwa COED hakuna ACCES ya tv, kwa maana ya kwamba hutaangalia channel zozote. ingawa pia inategemea, kwa wanaoishi gorofa za juu hapo coed wanapata TBC. hii ni kwa sababu ya location ya college. Unaruhusiwa kumiliki vifaa visivyozidi 13 amps. Zaidi ya hapo circuit breaker inakata na hivyo flooor nzima inakosa power.

Earth science utalazimika kupanda daladala zinazokwenda College of Education, kwa wakati huu hata hapo itakapokamilika utalazimika kufanya hivyo.

Vipi kuhusu hali ya usafi, kila mtu atajitegemea vifaa vyake au la?? na pia mabafu na vyoo vimekaaje?
 
je vp kuhus boom[mkopo] unatolewa mkifika chuo? kama ndio unalazimika kuja na hela ya fees, accommodation,registration na za other expenses coz hutakuwa ujapewa hilo boom, wamesema mwisho wa kulipa hizo niaje ni 31 sept
 
je vp kuhus boom[mkopo] unatolewa mkifika chuo? kama ndio unalazimika kuja na hela ya fees, accommodation,registration na za other expenses coz hutakuwa ujapewa hilo boom

Swali zuli sana hili, naomba kuongezea nimeona Direct cost ni kama laki3 au laki2.8 sasa hizi fedha na out of mkopo au ukipata mkopo unalipia vitu vipi??
 
Social science kama wajasi wapo basi wako mbali sana, nna uhakika hapo hakuna wajasi. Kuna wakati fulani nilikuwa nawaona watu wa Social wakiagiziana misosi kutoka coed, Hii si kawaida sana na hutokea wakati viazi vikiwa vingi na mara nyingi mifuko ya watu hapo inakuwa tupu. Walichokuwa wamewekeana ni zamu kwa vyumba. Kila chumba kina zamu yake maalum ya kufuata viazi Ng'ong'ona (COED) huu ni wakati mgumu sana kwa wanafunzi.

kwa iyo COED wajasi kama kawaida au na je kwa kila mlo hawa wajasi wana cost shiling ngapi?
 
kwa wajasi msosi wa ghali kabisa ni 1500. coed wajasi full. quality kwa maana hata lecturers na wafanyakazi wengine kibao, librarians wote kwa mjasi
 
Back
Top Bottom