Nakumbuka nilipata scholarship fulani ya hela kibao huko majuu. kwa mtazamo wangu nikajua ukiacha tuition fee nyingine zote nitapewa mimi. Kwanza nilipotua New York nikachukua cab/taxi jamaa akanipeleka mitaa kibao mwisho nikafika chuo kusoma mita nikadaiwa nauli kibao baada ya wiki moja nikaanza kutembea mitaani lahaula kumbe nilichukulia taxi ni takribani kilometa moja tu kufika ninakoenda nikagundua jamaa kanikaribisha ugaibuni.
Kufika chuoni nikapewa ID kwenda bwenini nikaombwa kadi yangu kwaajili ya malipo ikachanjwa nikarudishiwa, kwenye chakula ni kadi, library card, treni kadi mwisho nikaomba hela ya kujikimu nikisingizia kwenda mjini, cinema, na vitu vidogovidogo. nikajibiwa everything is in your ID nikastuka ndio nikaambiwa itanisaidia kuwa na matumizi sahihi na kuwa nikinunua vitu ina limit kiasi siyo kununua tu kila unachokitaka. Pia nikaambia nilichopewa ni accommodation, meals, transport na stationary na si vinginevyo. Nimefurahi sana mtoa mada alivyotoa muongozo ili kusaidia ndugu zetu wanaoenda vyuoni. Natafuta facts zo UDSM niliposoma nami nitatoa msaada kama alivyofanya ndugu MAKOLE. Naongezea tu kuwa kwa wanafunzi wote waliochaguliwa kuingia vyuoni na kuhakikishiwa mkopo wa asilimia yoyote kuwa. Asilimia ya Mkopo ipo kwenye ada, na baadhi ya vitu vinginie vichache ila ya kula na kulala unapea yote. Hela unayopewa mkononi ni Meals and Accommodation Allowance tusiichanganye na hela ya nauli, dawa ya mswaki, sabuni, nguo, simu/mawasiliano, ada ya ndugu, kununua kiwanja, kujenga au kusaidia wazazi. Kupanga matumizi ni kitu cha msingi sana unapokua chuoni maana bila hivyo maisha ya chuo utayashindwa.