Ushauri kwa waliochaguliwa UDOM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa waliochaguliwa UDOM

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MAKOLE, Aug 22, 2012.

 1. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hongereni kwa kuchaguliwa "The White University" Nawashauri hivi:-

  1. Yapo makampuni ya mabasi yatawataka mlipe pesa benki ili yawasafirishe hadi UDOM- Kataa kwani watakupiga hela halafu safari utaiona chungu. Hata wakijifanya wameingia mkataba na chuo, usiingie mkenge. Chukua basi kwa kujitegemea wewe mwenyewe.

  2. Stendi ya daladala zote ndani ya Dodoma huanzia safari zake stendi ndogo ya daladala-Jamatini. Kuwa makini na eneo hilo kwani waleti na simu za mkononi hapo zinasakwa kwa udi na uvumba.

  3. Uwe na uhakika wa College unayokwenda. Kwa kifupi, ziko daladala zinazokwenda Education, jina jingine wanapaita Ng'ong'ona ama Ng'ox. Wale waliochaguliwa college of Education, Medicine, Informatics na natural Science upande daladala hizo, vinginevyo utapata tabu kubwa.

  4. Wewe unaekwenda College of social science pamoja na humanities panda daladala inayokwenda Social au Bondeni.
  Kinyume na hapo utajiju.

  5. Nauli kwa daladala ni Tsh 350 kwa safari yoyote ndani ya College, Kutoka Jamatini hadi Chuo ni 350 pia. Wahuni wanapiga hadi 1500/- kwani wanajua kuwa ni wageni hamjui kitu.

  6. Tax inategemea maelewano, standard bei ni elf 8-10. epuka kupanda tax kwani utazungushwa mjini mitaa karibu yote na watakwambia bei kubwa, hata hivyo, kama huna uhakika wa college yako pia wanaweza kukuingiza ndani ya chuo wakakuzungusha college zote, watakuchanganya na majengo then watakupiga hela ndefu.

  7. (kwa wanaokwenda social science) Chagua mavazi ya heshima kwani ukidhani unakwenda kujiachia unaweza ukajikuta unarudi nyumbani siku hiyo hiyo, Kwa wanadada, vimini, suruali za kubana, nguo za ajabu ajabu waachie wadogo zako. Kama huna za kushonesha anza kuzitafuta. Kwa wanakaka, punguza idadi ya majinzi (Hasa kwa wanaokwenda social science), mitindo ya kata K, kusuka nywele, kuvaa heleni potezea kwenu.

  8. Kama mnasafiri kwa kampani, kuweni makini na College mnazokwenda, ikitokea kwamba mmefika Dodoma na si wenyeji hivyo kwenda chuoni moja kwa moja, na ikiwa College zenu ni tofauti mtalazimika kutengana hapo ili kila mmoja apande gari ya college inayomhusu ili kuepusha usumbufu,

  9. Wenyeji wenu (mwaka 2na 3) hawapo na mtakuwa wageni watupu eneo hilo, Usimwamini mtu yeyote pahala popote pale ndani na nje ya College.

  Huu ni ushauri wangu kwa uzoefu mdogo nilioupata pindi nilipokuwa huko Idodomiya. Kila la Kheri!
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Mtu mwema kama wewe asante sana kijana. watanzania wote wangelikuwa hivi , tungelikuwa mbali, mafisadi wangeliwaonea huruma watanzania wenzao kama wewe ulivyoona huruma kwa wenzako wanaokuja hapo freshers.
   
 3. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  twapaswa kuwa hivyo ili kusaidiana, Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe, pia Mtanzania atasaidiwa na mtanzania mwenzake. Asante sana mkubwa
   
 4. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asante bro kwa kuwashauri wadogo zetu,wakumbushe na issue za cafeteria vs wajasi wacje wakaingia mkenge.Mimi nshaua kitambo.
   
 5. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  thanx alot...
   
 6. M

  Mfukunyuzi Senior Member

  #6
  Aug 22, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  vp kuhusu college ya medicine mavazi yako vp, majeans hayaruhusiwi, au na yenyewe ni mwendo wa mchomekeo kwa kwenda mbele maana me shna suruali ya kitambaa hata 1
   
 7. Thomas D Segeja

  Thomas D Segeja Member

  #7
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 95
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 25
  sanx sana kwa taarifa mtanzania mwema.ila ningependa kufahamu ni lini hasa firts year wanatakiwa kuripoti,nilidhani,mkifungua basi tutaenda wote
   
 8. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hapana, mwaka wa kwanza watatangulia wiki moja kabla ya wanaoendelea. Hamuwezi kwenda pamoja.
   
 9. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,890
  Likes Received: 4,743
  Trophy Points: 280
  Dah kazi itaoneka hiyo siku. Ahsante kwa taadhari yako kaka mungu akubariki.
   
 10. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kwa sasa medicine wanakaa College ya education na wanafanya kwenda chuoni kwao na kurudi. Isipokuwa kwa mwaka wa kwanza watakaa college kwao. Kuhusu mavazi mara nyingi huwa wanayo aina fulani ya sare yao. Kabla ya kuchanganywa hapo Education, walikuwa hawaruhusiwi kuvaa mapensi, jinsi, vimini, cap(kofia za chepeo) Manguo ya ajabu ajabu yalipigwa marufuku kwao toka zamani. Katika College walikokuwa wanafuatiliwa ni wao na nadhani ni kwa sababu ya maadili ya kazi zao. Uchache wao pia ulikwa unachangia kwani niliwahi kuambiwa na mtu anaesoma College hiyo kuwa hata uzururaji mjini hawakuruhusiwa, ila ni kwa taarifa maalum. Kama yupo mtu humu Jf anasoma medicine atatupa ukweli.
   
 11. songoros

  songoros Senior Member

  #11
  Aug 22, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  kamaunafaham tufahamishe tarehe mkuu!!!
   
 12. Kaka mwisho

  Kaka mwisho JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  wajasi cku hz wanapatikana ngox education na humanities , ukiwa ss ni cafeteria tu wali mbichi happy na bp na chakula kichafu taji.
   
 13. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kama tumbo lako limezoea vyakula softsoft utapiga kwa Mwarabu Cafe. Ila cafe huwa wanazingua, full kuumwa matumbo kwani vyakula vyao wako ki-faida zaidi. Kitu kwa wajasi, Huko ndo mambo yetu yale ya mama nijazieeeeeeeee! Full kukopa kama umeishiwa, Full mahuduma. Ingawa kwenye orientation course watawaambia msiende kwa wajasi kwani ni wachafu na hakuna hadhi. Hao watakuwa wanatetea ulaji wao tu.
   
 14. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kwa wale watoto wa mama waliozoea gari za nyumbani si vibaya wakianza mazoezi ya kuingilia madirishani kwenye daladala, Hapo kwenye usafiri ni suala tu la survival for the fittest. Kwa wanaotoka Dar na vitongoji kama Mbagala hii haitawapa tabu sana.
   
 15. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,890
  Likes Received: 4,743
  Trophy Points: 280
  Mkuu nani atakae tupokea? Je kuna utaratibu upi unatumika? Pia sina suruali za kitambaa hata moja, na nimepigika hata pesa ya kununua vitamba hakuna. Nitajitahidi kuvalia tumboni kwa kweli.
   
 16. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #16
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mkubwa wale wa College of Earth Science inakuaje mkuu
   
 17. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #17
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Chuo kikuu hakuna utaratibu wa kupokeana, ila utakayemkuta ndiye rafiki yako ingawa usimwamini kwa asilimi mia, inategemea uko college ipi kwani zipo college ambazo mawarden wanaishi chuoni, hapo utapata huduma ya malazi kirahisi, napo ni mpaka ulijue hilo na tatizo wote ni wageni. Kwa college ambazo hazina mawarden usiku ndio itakubidi utafute urafiki wa siku hiyo hiyo ili walau ujihifadhi, ukiwahi mapema chuo fresh utapata chumba na godoro, au tena unaweza kuchukua gest kuepuka usumbufu.
   
 18. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #18
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  sifaham taratibu zao kwa sasa kwani mwanzoni walikuwa wamechanganywa College of Education. Kuna tetesi kuwa College yao imeshakamilika hivyo watahamia kwenye college yao, ingawa pia sina uhakika kama hiyo college yao inazo hostel. Ikiwa tayari imekamilika zipo tetesi kuwa wataishi kati ya Education au Informatics. Mwenye updates kuhusu hili atakueleza fresh.
   
 19. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #19
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  tembelea website ya chu mara kwa mara, kwa sasa sifahamu ni lini hasa mnatakiwa kwenda,
   
 20. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #20
  Aug 22, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,890
  Likes Received: 4,743
  Trophy Points: 280
  Me nitakua collage ya social.
   
Loading...