Ndugu wanafunzi wenzangu, kwa majina ninaitwa Willbrod Burchad, ndo naingia mwaka wa 3 ktka chuo kikuu cha Dodoma, nipo college of humanities & social sciences. Mmi ndiye waziri wa mikopo katka college of humanities & social sciences.
Kama kiongozi na mwanafunzi mzoefu napenda kuwakaribisha sana wanafunzi wote mliochaguliwa katka chuo kikuu cha Dodoma. Lakini pia naomba niwafahamishe yafuatayo:
1. Kwa mwaka wa kwanza chuo kinafunguliwa tarehe 18/10 kwa mwaka wa pili na kuendelea tarehe 25/10 hivyo wakati mnaripoti mnaweza kuwakuta wanafunzi wachache wanaoendelea (continuing) ambao watakuwepo kwa ajili ya kurekebisha matokeo yao (supplementary). Hao wanaweza kuwaelekeza kwa namna moja ama nyingine.
2. Pia viongozi wa kila college(serikali ya wanafunzi) watakuwepo chuoni tayari kwa kuwapokea na kusaidiana na viongozi wa chuo kwa ajili ya kuwafanyia usajili (registration). Hivyo uwepo wa viongozi hao utakuwa ni msaada tosha kwenu.
3. Usafiri wa kwenda chuoni yaani kutoka Dodoma mjini kuja kwenda chuoni unataiwa kupata maelekezo baada ya kushuka katika stend kuu ya mabasi na kwenda stend ya daladala yaani Jamatini nauli ni sh 400-500 kulingana na college unayoenda na ukiwa na begi kubwa pia huwa linatozwa sh 500.
4. Chuo kikuu cha Dodoma kipo nje ya mji wa Dodoma takribani km 7. Unapoingia chuoni baada ya kuvuka lango kuu college ya kwanza ni college of humanities and social sciences, hivyo mnaombwa kuwa makini wakati wa kupanda daladala unapokuwa mjini kwani daradara zipo mara mbili yaani zinazoenda udom bonden (humanities and social sciences) na zile zinazoelekea education yaani ng'ong'ona (hizi zinapitia informatics, natural science, health science mpaka education).
Kwa ufupi haya ndo nimeona niwafahamishe nawe ukiwa na mwenzako, tafadhali muelekeze haya kwani ni muhimu. Kwa mara nyingine nawakaribisha sana sana sana katika chuo kikuu cha Dodoma InshaAllah mola akipenda tutakutana huko mwezi wa 10, kikubwa tuombe bodi ya mikopo iwatendee haki kwani hiyo ndo huwa kazi yangu tunapokuwa chuoni.