Matutusgrandchild
Member
- Aug 29, 2014
- 73
- 2
sasa me tayari nshachaguliwa udom, hii inanihusu
bb kwan post zimeshatoka?
sasa me tayari nshachaguliwa udom, hii inanihusu
bb kwan post zimeshatoka?
kaulize tcu
wanaruhusu kurent out of campus?
Hongereni kwa kuchaguliwa "The White University" Nawashauri hivi:-
1. Yapo makampuni ya mabasi yatawataka mlipe pesa benki ili yawasafirishe hadi UDOM- Kataa kwani watakupiga hela halafu safari utaiona chungu. Hata wakijifanya wameingia mkataba na chuo, usiingie mkenge. Chukua basi kwa kujitegemea wewe mwenyewe.
2. Stendi ya daladala zote ndani ya Dodoma huanzia safari zake stendi ndogo ya daladala-Jamatini. Kuwa makini na eneo hilo kwani waleti na simu za mkononi hapo zinasakwa kwa udi na uvumba.
3. Uwe na uhakika wa College unayokwenda. Kwa kifupi, ziko daladala zinazokwenda Education, jina jingine wanapaita Ng'ong'ona ama Ng'ox. Wale waliochaguliwa college of Education, Medicine, Informatics na natural Science upande daladala hizo, vinginevyo utapata tabu kubwa.
4. Wewe unaekwenda College of social science pamoja na humanities panda daladala inayokwenda Social au Bondeni.
Kinyume na hapo utajiju.
5. Nauli kwa daladala ni Tsh 350 kwa safari yoyote ndani ya College, Kutoka Jamatini hadi Chuo ni 350 pia. Wahuni wanapiga hadi 1500/- kwani wanajua kuwa ni wageni hamjui kitu.
6. Tax inategemea maelewano, standard bei ni elf 8-10. epuka kupanda tax kwani utazungushwa mjini mitaa karibu yote na watakwambia bei kubwa, hata hivyo, kama huna uhakika wa college yako pia wanaweza kukuingiza ndani ya chuo wakakuzungusha college zote, watakuchanganya na majengo then watakupiga hela ndefu.
7. (kwa wanaokwenda social science) Chagua mavazi ya heshima kwani ukidhani unakwenda kujiachia unaweza ukajikuta unarudi nyumbani siku hiyo hiyo, Kwa wanadada, vimini, suruali za kubana, nguo za ajabu ajabu waachie wadogo zako. Kama huna za kushonesha anza kuzitafuta. Kwa wanakaka, punguza idadi ya majinzi (Hasa kwa wanaokwenda social science), mitindo ya kata K, kusuka nywele, kuvaa heleni potezea kwenu.
8. Kama mnasafiri kwa kampani, kuweni makini na College mnazokwenda, ikitokea kwamba mmefika Dodoma na si wenyeji hivyo kwenda chuoni moja kwa moja, na ikiwa College zenu ni tofauti mtalazimika kutengana hapo ili kila mmoja apande gari ya college inayomhusu ili kuepusha usumbufu,
9. Wenyeji wenu (mwaka 2na 3) hawapo na mtakuwa wageni watupu eneo hilo, Usimwamini mtu yeyote pahala popote pale ndani na nje ya College.
Huu ni ushauri wangu kwa uzoefu mdogo nilioupata pindi nilipokuwa huko Idodomiya. Kila la Kheri!
COLLEGES zipo sita kama ifuatavyo:-
1. COED-walimu wote wa BED isipokuwa BAED na BSC(Ed).
2. COES-ma-engeneer wote wa resource za ardhi
3. CIVE- ma~engeneer wa computer.
4.CNMS-madaktari,matabibu,wa~takwimu pamoja na walimu wa BSC(Ed).
5. CHSS-sanaa na sayansi za jamii pamoja na walimu wa BAED.
N.B: CHSS ni colleges 2 kwa moja yaani college of humanities(CH) and college of social science(SS).
Hivi Dodoma kuna chuo kikuu? Kile chuo cha kujiuza kiko mkoa gani
kile kile alichosoma mama yako kwani hakukwambia kipo mkoa gani?
Yes! It is a white university but does it produce white students and practitioner? No! It is just painted white but the quality of education is not yet white, it is still some how grey. So it is not competitive. Plz make the quality of education white then you proud for that.
ahsante kiongoz tunazid kufanya vizur ndani ya home of great thinkers na logo ya emblacing knowledge
Pole sana Permanides, hiyo post ilitolewa Tangu 5/2/2012, na wewe taarifa za uanachama wako fb ziko hivi:
Join Date : 18th May 2013
Posts : 158
Rep Power : 376
Likes Received33
Likes Given0
ulichelewa mwaka mzima nyuma ya POST hiyo, By the way; uko mwaka wa kwanza hapo UDOM? Msalimie MLACHA HAHAHAAAAAA! Fanya utafiti kabla ya kukurupuka kaka
Huku kiingereza kinakuwa kwa kasi ya ajabu! "Emblacing knowledge"