Hapo wanapaita St social, (samahani kama ntawakwaza watu), hapo kuna mapinduzi ya mavazi, ndipo palikuwa panavaliwa vivazi. Ila kwa sasa nadhani ndio college inayoongoza kwa nidhamu ya mavazi. wanawashinda walimu kwa haiba hapo. Hostel za kumwaga sana, maisha ya hapo ndo ivyo tena, mtu pesaaaaa na watoto wa kishua. ingawa wapo watoto wa wakulima lakini nao wanabadilika wakifika hapo.
Ukiingia eneo hilo heshimu "pavement" usikate njia ukakanyaga nyasi kufuata njia zisizo rasmi, utakinukisha mapema, wako vijana wa SMA-JKT (SINA HAKIKA KAMA BADO WANALINDA ENEO HILO), unaweza kujikuta uapanda na kumwagilia hayo majani, Usimwage maji dirishani, usianike kitu chochote dirishani, utaingia matatani. Hapo ni sosho ndugu!