Ushauri kwa waliochaguliwa UDOM

..je kubadili course hapo udom inawezekana ama!
Plz waelewa mnijibu
 
Ndugu yangu first year karibu sana UDOM, ikiwa kuna jambo unataka kulijua la UDOM kwenye college ya humanities and social science niulize nitakusaidia kwa kukujibu na kukupa ufafanuzi.KARIBU SANA UDOM

..........
Nikuulize Wewe ukiwa kama na ni?????
 
me cwez kumuuliza mlinzi wa chuo me namuulza vice chancellar kwan we nan kwanza ? na nan kakupa haya majukumu?
 

nikitokea dar nishukie wapi mkuu?
 

Sasa ndio umeongea nini?eti great thinker
 
nikitokea dar nishukie wapi mkuu?
Sorry jamaa zangu Stand imesharudi Mjini TAFADHALINI SHUKENI STAND YA MKOA ni mjini kabisa hapo utapata usafiri wa kufika UDOM
Ila kwa mwaka huu sijui Registration ni nje ya UDOM maana kuna wakati

  • [*=1]Walifanyia Uwanja wa jamhuri baada ya Chuo kufungwa uokana na migomo
    [*=1]Wakaja kufanyia uwanja wa Relways njia ya UDOM baada ya DUWASA
sasa angalia Joining Instruction yako itakuonesha ni wapi pa kujisajili​
Hii Mada ilikuwa ya 2012 leo tupo Oktoba 2013
 



MADENTI HUKO VYUONI

Hakika sisi wazazi,mno mwatufedhehesha,
Madenti wa siku hizi,sana mwatunyong'onyesha,
Kwanza ni hayo mavazi,kweli mwatuaibisha!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.

Madenti huko Vyuoni,bure mwajidhalilisha,
Mwazurura mitaani, na usiku "kujirusha",
Mkifeli Mitihani,Mwalimu "kanikomesha"!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.

Haiba ya Mwanafunzi,siku hizi imekwisha,
Si kama za kwetu enzi,mengi tulijiepusha,
Masomo tuliyaenzi,tulisoma tukakesha!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.

Zimewajaa tamaa, kuharakia maisha,
Chumbani vitu hujaa,wenzenu kuwaringisha,
Usiku ndio balaa,mambo yenu yanatisha!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.


Zama hizi kuna ndwele,tena zinapukutisha,
Si kwamba naona gele,bali ninawakumbusha,
Malizeni kwanza shule,anasa hazitakwisha!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.

Kaditamati Madenti,maongezi nafupisha,
Wavulana na mabinti,Betord na Mwanaisha,
Msicheze na wakati,jueni mwajipotosha!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.

Lambert F. Chialo( Mhadhiri wa Malenga)
Magogoni, Dar es Salaam
0713961860
Reply With Quote
 
MADENTI HUKO VYUONI

Hakika sisi wazazi,mno mwatufedhehesha,
Madenti wa siku hizi,sana mwatunyong'onyesha,
Kwanza ni hayo mavazi,kweli mwatuaibisha!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.

Madenti huko Vyuoni,bure mwajidhalilisha,
Mwazurura mitaani, na usiku "kujirusha",
Mkifeli Mitihani,Mwalimu "kanikomesha"!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.

Haiba ya Mwanafunzi,siku hizi imekwisha,
Si kama za kwetu enzi,mengi tulijiepusha,
Masomo tuliyaenzi,tulisoma tukakesha!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.

Zimewajaa tamaa, kuharakia maisha,
Chumbani vitu hujaa,wenzenu kuwaringisha,
Usiku ndio balaa,mambo yenu yanatisha!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.


Zama hizi kuna ndwele,tena zinapukutisha,
Si kwamba naona gele,bali ninawakumbusha,
Malizeni kwanza shule,anasa hazitakwisha!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.

Kaditamati Madenti,maongezi nafupisha,
Wavulana na mabinti,Betord na Mwanaisha,
Msicheze na wakati,jueni mwajipotosha!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.

Lambert F. Chialo( Mhadhiri wa Malenga)
Magogoni, Dar es Salaam
0713961860
Reply With Quote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…