Ushauri ni mzuri tu.
Huko mbeleni au kama si hivi karibuni ataanza kuitwa Mzee, kwa mila na tamaduni za Mtanzania hii inatosha.
Na ataitwa hivyo kwakuwa ni kweli atakuwa anafikia umri fulani wa kuitwa Mzee-ila kuna hili Mzeee, Ni heshima kubwa sana ambayo mtu huwa anapewa hata pale akiwa kijana....tunajipindisha tu lakini huo ndio Ukweli, sio rahisi mtu kupachikwa jina Mzee alimtmradi tu. Mara nyingi hufuatiwa kwa mambo,vitu, maneno, vitendo vinayoambatana na tabia fulani..ambayo anayeitwa huwa inamfuata, hata ikiwa alikuwa mtongozaji maarufu mtaani, au mcheza bao maarufu wa mtaani..au mtu mwenye upendo na watu mtaani au mtu mwenye pesa mtaani ambaye utamkuta ndie mwenye gesti mtaani au nyumba kadhaa n.k n.k Yaani watu wenye heshima fulani....
sasa haya mambo ya kuiga wenzetu yanaboa....Daktari, Sheikh, Professor, millionea , bilionea n.k yote ngeni tu na ndio tunazidi kuchanganyikiwa....
....Kuna utamu fulani vile kwa Kiswahili mtu kuitwa Mzee na mara nyingi huwa inafuatia na tabasamu....umeona wapi Unamwita mtu Doctor au Shehe au Bilionea na mtu akatabasamu?/ukatabasamu(najichekesha hapa) wapi? Ikiwa hivyo basi kwa namna moja au nyingine inakuwa kejeli ya kidizaini tuu! Kha
'Mzeee bwana'! Hapo lazima uta tabasamu.
'Mzeee Lissu'.
..wee wacha wee Kiswahili kitamu.
Ninapinga Tundu Lissu kuitwa Daktari au kuongezewa title yeyote ile ya Kidhungu! Napendekeza Mzeee Tundu au Mzeee Lissu.