isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,125
- 6,250
- Thread starter
- #21
Dah..wadau mmeandika mengi as if ukiyasema yanatokea tu...guys hakuna kinachowezekana hapo Kama hakuna pesa..narudia tena hakuna kinachowezekana hapo Kama hakuna pesa..pesa pesa..pesa..aka.fedhaaa...
Maligi yote hayo hayataanzishwa kwa tamko la TFF ama Serikali..lazima pesa awepo...
Ambacho nafikiria kwanzA tuangalie namna ya kutatua changamoto ya pesa ambayo ndio itafanikisha haya yote..pesa ikishapatikana hii mipango mizirui itatekelezeka tu.
Mtazamo wangu ni hivi..Serikali iweke sheria kwa makampuni na taaisisi kwa kila mkoa,walaya kuhakikisha wanatumia pesa zao za SRF ( Social Responsibility Fund) kutenga nusu na kuzitekeleza kwenye shughuli za kimichezo aidha kwa kudhamini timu katika maeneo hayo ama kujenga miundombinu ya kimichezo ama kuikarabati..hii policy iko Sana Afrika kusin , Namibia na baadhi ya nchi nyingine za kusin huko.
Hii itasaidia kwanzA, kuboresha Hali za timu, kuzipa timu Hali ya ushindani na kukuza ajira .
Emu fikiria now ligi kuu iko na timu 16 what if kila timu inapotoka ikawa inapata hii support..ni wazi ushindani ungeongezeka..ushindani ukiongezeka..mashabiki wanajitokeza..mashabiki wakijitokeza..ligi inakuwa na mvuto na kuvutia kampuni nyingi zaidi kuwekeza kwenye soka..matokeo yAke tunakuwa na ligi yenye ushindani na inayouzika ..
Kule uingereza pia wanatumia policy hii..unakuta katimu ka daraja la sita huko..kifuani mwa jezi zao kumepachikwa mdhamini..
Kingine..naungana na mtoa hoja..TFF wanafaa waiache ligi kuu iwe ni project inayojitegemea waipe nafasi ya kuwa Kama kampuni ama taasisi binafsi ..yenye kujitosheleza..ikiwezekana iwe na wataalamu na wajuzi wa mambo ya marketing katika football Ili lengo litimie.
TFF ibaki kwenye kusimamaia maendelo ya mpira wa miguu na kuandaa sera za muda mrefu ,wakati na mfupi kwa timu za Taifa.
"...TFF wanafaa waiache ligi kuu iwe ni project inayojitegemea waipe nafasi ya kuwa Kama kampuni ama taasisi binafsi ..yenye kujitosheleza..ikiwezekana iwe na wataalamu na wajuzi wa mambo ya marketing katika football Ili lengo litimie."
Hakika!