Ushauri kwa TFF, bodi ya ligi na ligi kuu Tanzania

Dah..wadau mmeandika mengi as if ukiyasema yanatokea tu...guys hakuna kinachowezekana hapo Kama hakuna pesa..narudia tena hakuna kinachowezekana hapo Kama hakuna pesa..pesa pesa..pesa..aka.fedhaaa...

Maligi yote hayo hayataanzishwa kwa tamko la TFF ama Serikali..lazima pesa awepo...

Ambacho nafikiria kwanzA tuangalie namna ya kutatua changamoto ya pesa ambayo ndio itafanikisha haya yote..pesa ikishapatikana hii mipango mizirui itatekelezeka tu.

Mtazamo wangu ni hivi..Serikali iweke sheria kwa makampuni na taaisisi kwa kila mkoa,walaya kuhakikisha wanatumia pesa zao za SRF ( Social Responsibility Fund) kutenga nusu na kuzitekeleza kwenye shughuli za kimichezo aidha kwa kudhamini timu katika maeneo hayo ama kujenga miundombinu ya kimichezo ama kuikarabati..hii policy iko Sana Afrika kusin , Namibia na baadhi ya nchi nyingine za kusin huko.

Hii itasaidia kwanzA, kuboresha Hali za timu, kuzipa timu Hali ya ushindani na kukuza ajira .

Emu fikiria now ligi kuu iko na timu 16 what if kila timu inapotoka ikawa inapata hii support..ni wazi ushindani ungeongezeka..ushindani ukiongezeka..mashabiki wanajitokeza..mashabiki wakijitokeza..ligi inakuwa na mvuto na kuvutia kampuni nyingi zaidi kuwekeza kwenye soka..matokeo yAke tunakuwa na ligi yenye ushindani na inayouzika ..

Kule uingereza pia wanatumia policy hii..unakuta katimu ka daraja la sita huko..kifuani mwa jezi zao kumepachikwa mdhamini..

Kingine..naungana na mtoa hoja..TFF wanafaa waiache ligi kuu iwe ni project inayojitegemea waipe nafasi ya kuwa Kama kampuni ama taasisi binafsi ..yenye kujitosheleza..ikiwezekana iwe na wataalamu na wajuzi wa mambo ya marketing katika football Ili lengo litimie.

TFF ibaki kwenye kusimamaia maendelo ya mpira wa miguu na kuandaa sera za muda mrefu ,wakati na mfupi kwa timu za Taifa.

"...TFF wanafaa waiache ligi kuu iwe ni project inayojitegemea waipe nafasi ya kuwa Kama kampuni ama taasisi binafsi ..yenye kujitosheleza..ikiwezekana iwe na wataalamu na wajuzi wa mambo ya marketing katika football Ili lengo litimie."

Hakika!
 
Shukrani Castr kwa hint! Kubwa, naona mfungo na structure zibadilike sasa kuwezesha mageuzi.

Ni kweli Ligi ya Wanawake ipo lakini haieleweki ni Ligi au bonanza. Katika hili ni lazima kwa vilabu kuwa na timu za wanawake, vijana na watoto.
Ligi kuu ya wanawake ni copy and paste ya ligi kuu wanaume..kwa sababu timu mbili zenye nguvu ndizo zinatawala pia huko..angalau timu za jeshi zinajitutumia..lakn nazo sioni zikiwa na muda mrefu wa kutamba..maana kwa nzia msimu huu ushindani uko kwa Simba Queens na Yanga Princes ..msimu ujao na mingine Hali itabaki hivi hivi..kwa sababu hizo timu zingine hazina uwezo wa kuhudumia wachezaji kwa msimu mzima..jiulize timu haina hata mdhamini..wachezaji hawalipwi mshahara..wengi wanacheza walitarajia kusajiliwa na Simba Queens ama Yanga Princes ndio angalau walipwe..kwa namna hio ushindani huku nako utakuwa ni zero plus zero...mdhamini aliyepo anatoa milioni 5-19 kwa msimu kwa kila hii pesa uitumie kutunza wachezaji (camp cost) safari za timu kucheza mechi, ulipe mishahara kwa wachezaji na makocha plus gharama zingine kwa timu ..BADO mwenye timu hajajigawi na yeye gawio lake hapo..so unajikuta pesa yote hii hazitoshi hata ..
 
Pesa za kufunga hizo screen waziokote wapi!!? Ligi yetu inavalue ya hivyo..wafunge LCD screen za matangazo hayo kwenye miundombinu ipi!? Je gharama za kurun hizo screen zitakuwa kwa TFF ama timu za ligi kuu ama wamailiki wa viwanjan!?

Kuna mahali nimeeleza TFF, Bodi ya Ligi, Ligi Kuu na wizara ya michezo zitafute udhamini na ushirika. Sio lazima pesa yote itolewe na TFF hapana! Ikiwa kupitia ushirika kuna namna ya kupata udhamini katika haya.

Mfano, taasisi tajwa hapo zinaweza kuomba ushirika kutoka kampuni na taasisi kadhaa kufanikisha haya. Tunaweza kupeleka proposal Sony, Xiaomi, Huawei au Samsung kuwekeza katika skrini hizo na LCD kwa makubaliano kadhaa ikiwamo kuonekana kama moja ya wadhamini.
 
Vizuri sana kugusia suala la kipawa, elimu na ajira kwa wakati. Ni wazi ziwekwe taratibu ambazo haziathiri kipaji na elimu kwa mtoto au kijana na itambulike wazi mpira na michezo ni sehemu ya ajira tena yenye ukwasi mkubwa.

Hata mimi nilikuwa mchezaji kwa bahati nzuri au mbaya nimewahi kucheza Walvis Bay City na FC Ulster ya watoto na nimewahi kutrain na Kagera Sugar nikiwa kinda kabisa. Nadhani baba angekubali niendeleze elimu na mpira leo hii ningekuwa Arsenal. 😅

Tunahitaji mabadiliko!
Bro..kipaji bila matunzo ni sawa na kupalilia Shamba lisilopandwa mbegu..kutaota magugu tu...watoto wengi Wanavipaji..matunzo hakuna...Kuna academy chungu laki huko mitaani..zipo kwa kuwa zipo..na haizja namna lakini hazifuati misingi ya kukuza mchezaji..leo hii halaand mchezaji wa Borusian Dortmund ana miaka 20 analimwili Jumba Kama vile..sisi huku mchezaji wa age hio anakamwili kalikodumaa kwa utapiamlo kea kukosa mlo sahihi...matokeo yAke..anavuka miaka ya kuwa kwenye academy lakini bado yupo hapo hapo anatafuta nafasi..akija kuipata nafasi anabadiliaha cheti za kuzaliwa kutoka miaka yake halsii anaipunguza ..Kama alikuwa na 24 ana ipinguza mpaka 17 ..matokeo yAke tunakuwa na wachezaji vikongwe kwenye timu zetu..ambao wanashindwa kutupa matokeo chanya hata pale inapoonekana kuwa tunastahili kuyapata.
 
Kuna mahali nimeeleza TFF, Bodi ya Ligi, Ligi Kuu na wizara ya michezo zitafute udhamini na ushirika. Sio lazima pesa yote itolewe na TFF hapana! Ikiwa kupitia ushirika kuna namna ya kupata udhamini katika haya.

Mfano, taasisi tajwa hapo zinaweza kuomba ushirika kutoka kampuni na taasisi kadhaa kufanikisha haya. Tunaweza kupeleka proposal Sony, Xiaomi, Huawei au Samsung kuwekeza katika skrini hizo na LCD kwa makubaliano kadhaa ikiwamo kuonekana kama moja ya wadhamini.
Uko sahihi, but kwa mvuto Gani ulipo kwenye ligi yetu mpaka hizo kampuni zikaja kuwekeza kwenye hayo Mambo!?..ukiacha mechi ya Simba na yanga, Simba vs Azam a, Yanga vs Azam ni mechi Gani zingine zinamvuto kwa watu na tentions kwa media!? Tena hapo itoe Azam ..ibaki Simba vs Yanga ama Yanga vs Simba..we have the only one match yenye mvuto..sasa kweli mtu she kupoteza karibu milioni 500-bilioni 10 kwa mechi Moja tu..tena ambayo imejaa ukiritimbana kuanzia dk 1-90!? Ngumu
 
Uko sahihi, but kwa mvuto Gani ulipo kwenye ligi yetu mpaka hizo kampuni zikaja kuwekeza kwenye hayo Mambo!?..ukiacha mechi ya Simba na yanga, Simba vs Azam a, Yanga vs Azam ni mechi Gani zingine zinamvuto kwa watu na tentions kwa media!? Tena hapo itoe Azam ..ibaki Simba vs Yanga ama Yanga vs Simba..we have the only one match yenye mvuto..sasa kweli mtu she kupoteza karibu milioni 500-bilioni 10 kwa mechi Moja tu..tena ambayo imejaa ukiritimbana kuanzia dk 1-90!? Ngumu

Ikiwa kufanikisha haya ni hadi tufikie kiwango fulani sioni tukipiga hatua. Ni kheri kuanza sasa.
 
Ikiwa kufanikisha haya ni hadi tufikie kiwango fulani sioni tukipiga hatua. Ni kheri kuanza sasa.
Sure..unahisi tuanze ..japo itachukua muda mrefu lkn sio mbaya...Ila shida watu tulionao kwneye mifumo ya Uongozi wa soka ..wanajiwaza wao na kesho yao tu..hawawezi kesho ya wajukuu zao...na hiki lipo lila mahali kwenye nchi hii..mtu anafanya Kazi kwa kujiangalie yeye na familia yake ..hawezi kuhusu wajukuu zake...ifike mahali..tufanye Kazi kwa kujiangalia , na kuwaangalia wajao ndio mafanikio yatapatikana ..
 
Sure..unahisi tuanze ..japo itachukua muda mrefu lkn sio mbaya...Ila shida watu tulionao kwneye mifumo ya Uongozi wa soka ..wanajiwaza wao na kesho yao tu..hawawezi kesho ya wajukuu zao...na hiki lipo lila mahali kwenye nchi hii..mtu anafanya Kazi kwa kujiangalie yeye na familia yake ..hawezi kuhusu wajukuu zake...ifike mahali..tufanye Kazi kwa kujiangalia , na kuwaangalia wajao ndio mafanikio yatapatikana ..
Hili suala la ustawi kwa pamoja ni muhimu sana kwa kila hali na mahali katika taifa.
 
Mambo kadhaa yanaanza uboreshwaji.

20210402_222840.jpg


20210402_222843.jpg
 
TFF na Ligi Kuu ihakikishe mgawanyo sawa wa mechi zitakazo oneshwa kwa vilabu vyote shiriki. Watakaochukua haki za matangazo wahakikishe wanajizatiti kwa kuongeza channeli zao kuwezesha kutoa fursa za uchaguzi wa mechi ya kuangalia mubashara.
 
Mkuu isajorsergio mwanzo sikuuona huu uzi. Nadhani ni moja ya nyuzi bora kabisa za football hapa JF. Mawazo yako ni mazuri sana na mengi kama sio yote yanatekelezeka ni kuwa na uthubutu tu.

Ningeendelea kuandika ila kwasasa nipo busy kidogo nitarudi tuendelee kujadili.
 
Nasikia Azam FC chini ya Azam - Bakhresa inafunga LED Lights, LCD Screens (Ads Boards) na kuongeza majukwaa katika kiwanja cha Azam Complex.
 
Habari 👋

Siku ya leo nimeona vyema nizikumbushe mamlaka za soka nchini Tanzania katika masuala kadhaa, nitumaini langu baada ya ushauri huu utekelezaji utaanza na msimu mpya 2021/2022 tutashuhudia makubwa na yaliyokuwa bora. Nimekuwa mfuatiliaji wa masuala mbalimbali lakini mpira wa miguu umekuwa kama sehemu ya maisha yangu. Nikiri wazi nazitambua jitihada na maboresho yanayofanywa na TFF, Bodi ya Ligi na Ligu Kuu japo naona kuna nguvu ya ziada inahitajika kuboresha mchezo wa soka na ligi zake.

1. Kutengeneza na kusimimia chapa ya Ligu Kuu

TFF, Bodi ya Ligi na ushirika wa Wizara ya Michezo zihakikishe zinatengeneza chapa ya Ligu Kuu, kuiendesha na kuisimimia kuleta tija katika kuinua mchezo husika ndani ya taifa, kuingiza mapato, kutangaza taifa na kutoa burudani. Ligu Kuu ni vyema isimame yenyewe huku ikiwa na wadhamini katika mlengo wake. Ligu Kuu kama chapa itambulishwe, itambulike na ifahamike kwa wepesi kwa kila rika, jamii na hali tofauti.

Kupitia chapa ya Ligi Kuu kama taasisi zitengenezwe taasisi ndogo chini yake ambazo zitakuwa katika mlengo wa soka kama ifuatavyo:-

i/. Uwepo wa ligi kuu itakayosimama kawaida katika mpira wa miguu unaohusisha timu za wanaume (Ligi Kuu).​
ii/. Uwepo wa ligi kuu ya wanawake ambayo itapewa nguvu, kusimamiwa na kuendeshwa katika mfumo sawa na unaondesha ligi ya wanaume hii itambulike (Ligi Kuu ya Wanawake au Ligi Kuu Women).​
iii/. Uwepo wa ligi kuu ya vijana chini ya miaka 23 itakayofahamika kama (Ligi Kuu ya Vijana au Ligi Kuu U23).​
iii/. Kuanzisha ligi kuu ya vijana chini miaka 18 itakayofahamika kama (Ligi Kuu ya Vijana au Ligi Kuu U18).​
iv/. Uanzishwaji wa ligi kuu ya watoto chini ya miaka 13 itakayofahamika kama (Ligi Kuu ya Watoto au Ligi Kuu U13).​
v/. Uanzishwaji wa ligi kuu ya mpira wa ndani au Fútsal ambayo itapewa nguvu kuwezesha kuinua, kuonesha na kutengeneza ajira na mapato kwa vijana, taaisi na taifa.​
vi/. Kuanzisha ligi kuu ya mpira wa fukwe maarufu kama Beach Soccer, ligi hii ipewe nguvu na isimamiwe vilivyo kuwezesha kuleta tija kwa vijana na taifa.​
vii/. Uanzishwaji wa ligi kuu ya michezo kimtandao eSport au eGames, ligi kuu hii itahusisha mfumo wa ligi tajwa hapa juu utofauti wake yenyewe ni michezo ya kimtandao au games ambayo itahusisha zaidi wapenzi na wafuatiliaji mchezo wa soka.​
Mfano wa haya ni kama picha ambatanishwa zinazoonesha ligi kuu ya soka nchini Chile.​
Ligi Kuu​
Ligi Kuu ya Wnawake​
Ligi Daraja la Kwanza​
Ligi Daraja la Pili​
Ligi ya Vijana​
Kombe la Ligi​
Kombe la Shirikisho​
Ligu Kuu ya Mpira wa ndani | Futsal​
Ligi Kuu ya Michezo | eFootbal/ eGames​

2. Kupitia na kuweka taratibu mpya za muenekano wa vilabu ndani na nje ya uwanja

Ligi Kuu na Bodi ya Ligi zitatakiwa kuandaa mfumo utakaosimamia vilabu viwapo uwanjani na nje ya uwanja kimuenekano na katika chapa husika. Chapa za vilabu, wadhamini na ligi kuu kama ifuatavyo:-

i/. Timu zote shiriki zitatakiwa kutumia mwandiko 'font' rasmi katika jezi zao utakaotumika kuwatambulisha wachezaji na namba zao mgongoni, benchi la ufundi na wahusika wa timu ziwapo uwanjani au katika sare za timu. Katika hatua ya awali naambatanisha mfano na mwandiko pendekezwa.​

View attachment 1737184

Hii ni font ya GONTSERRAT ambayo inaweza kusomeka na kuonekana katika jezi kwa uzuri.

View attachment 1737185

View attachment 1737186

View attachment 1737187

Muonekano wa majina katika jezi.
ii/. Jezi za vilabu zitatakiwa kuambatanisha nembo au matangazo ya wadhamini kama ifuatavyo:- Mdhamini mkuu atatakiwa kuchukua nafasi eneo la kifuani, mdhamini mkuu wa pili atatakiwa kuchukua nafasi mkono wa kushoto, nembo ya Ligi Kuu itatakiwa kuwa mkono wa kulia na nafasi ya chini ya mgongo itumike tuu kuweka tangazo linalohusisha jamii au kuigusa jamii (Inaweza kuwa taasisi, shirika au kauli mbiu) mfano, JamiiForums Foundation au Vijana na Ajira, Zuia Rushwa, Tokomeza Uviko na Ajali Basi. Sehemu ya ziwa la kulia ni nembo ya mtayarishaji jezi na sehemu ya kushoto ni nembo ya timu husika basi.​
iii/. Vilabu vyote shiriki vyatakiwa kuwa na bao za matangazo na mahojiano kwa kila timu na iv/. Kila timu ni lazima ifanye mahojiano kabla na baada ya mchezo (Pre Match Conference na After Match Conference) na mahojiano na waandishi wa habari kabla na baada ya mchezo. Bao hizo ni mfano wa picha ambatanishwa hapa​

3. Ligi Kuu na vilabu kidijitali na mawasiliano yake

i/. Ligi Kuu ihakikishe inaanda mawasiliano yake kama Ligi Kuu katika mitandao ya Facebook, Twitter, Instagram, YouTube, Spotify na LinkedIn mitandao hii isimamiwe ipasavyo siku hadi siku kuwezesha kufikisha taarifa na maendeleo ya mchezo wa soka na ligi yenyewe.​
ii/. Iwe ni lazima kwa vilabu kuwa na majukwa katika mitandao hasa Facebook, Twitter na Instagram kupita mitandao hiyo itatakiwa vilabu vyote viwe hai 'active' na kuendesha akaunti hizo katika misingi ya soka, nidhamu na uungwana.​
iii/. Ligi Kuu inatakiwa kuwa na tovuti rasmi ambayo itakuwa sehemu rasmi ya taarifa, ratiba, sheria, muongozo na masuala yote yanayohusisha ligi kuu. mfano Campeonatos Chilenos 2021 au Premier League Football News, Fixtures, Scores & Results
iv/. Vilabu vyote ni lazima kuwa na tovuti rasmi katika shughuli zake za utendaji wa kila siku.​
4. Ligi Kuu, washirika na wadhamini

TFF, Bodi ya Ligi na Ligi Kuu ihakikishe kuna wadhamini wafuatao ndani yao:- i/. Mshirika mkuu wa ligi kuu (Lead Partner/s) ii/. Mshirika mkuu katika utoaji vifaa kwa ajili ya ligi kuu mpira na jezi maalumu za waamuzi (Official Ball Partener) iii/. Mshirika mkuu katika masuala ya kifedha (Official Bank) iv/. Mshirika mkuu katika masuala ya vinywaji (Official Drink Partner) v/. mshirika muu katika masuala ya muda amabaye atatoa bao za muda na vifaa vya muda kwa waamuzi (Official Timekeeper) vi/. Mshirika mkuu katika masuala ya usafirishaji (Official Travel Partener).​

5. Ligu Kuu na taratibu za afya na usalama wa wachezaji na mashabiki

Ligi Kuu ihakikishe inasamimia na kupigania afya za washiriki katika mchezo na mashabiki ikiwa kwa kufuata taratibu za kujikinga na kupambana na UVIKO, maradhi ya moyo, magonjwa ya upumuaji, maradhi ya ngozi na usalama wa jumla kwa kufuata yafuatayo:-​
i/. Ligi Kuu itatakiwa kuwa na madaktari rasmi kama taasisi katika kila mchezo ambao watasaidia katika dharura na msaada wa nyongeza, hii iambatane na ulazima wa vilabu kuwa na madaktari idhinishwa na vyama na taasisi zinazosimamia madaktari na kila timu na gari la kubebea wagonjwa.​
ii/. Timu zote zitatakiwa kuchukua tahadhari kabla, wakati na baada ya mchezo dhidi ya magonjwa tajwa hapo juu.​
iii/. Vilabu vyote vitatakiwa kuwa na hati za afya ya jumla kutoka kwa Hospitali za kitaifa/mikoa na kuidhinishwa jopo la madaktari wa ligi kuu.​
iv/. Mashabiki watatakiwa kuchukua tahadhari wawapo viwanjani kwa kuacha nafasi ya kiti au mtu mmoja baina yao kujikinga na kupambana na UVIKO.​
v/. Ligi Kuu inatakiwa kuajiri walinzi binafsi maarufu 'stewards' ambao watakuwa chini yao katika kulinda usalama wa wachezaji, timu, viongozi na mashabiki, ligi kuu chini ya TFF itatakiwa kuomba msaada wa askari polisi wachache sana kuwepo uwanjani kwa hali za dharura. Hii ni kuondoa mkanganyiko wa mpira na siasa na hali zisizo za kiungwana kama zilivyoshuhudiwa katika vipindi tofauti waandishi na mashabiki wakipigwa na askari.​

6. Chombo huru ndani ya Ligi Kuu kitakacho husika na urushaji wa matangazo kwa washirika

Ligi Kuu inatakiwa kuanzisha chombo chini yake kitachokuwa na majukumu ya:-​
i/. Uandaaji, uchakataji na urushaji matangazo ya mchezo wa soka.​
II/. Ujenzi wa makao makuu hayo.​
iii/. Ununuaji wa vifaa husika.​
iv/. kuajiri watendaji husika.​
v/. Kuzalisha na kusimamia shughuli za kila siku.​
7. Ligi Kuu, waamuzi na usaidizi wa video (Video Assistant Referee

Ligi Kuu ihakikishe inapitisha sheria na kuanza kutumika kwa usaidizi wa video (Video Assistant Referee) ikiwa ni pamoja na:-​
i/. Kuagiza au kushirikisha chombo cha Ligi Kuu Productions kufanikisha hilo.​
ii/. Kutoa mafunzo kwa waamuzi au wataalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano kufanikisha hilo.​
iii/. Kutafiti mbinu wezeshi zitakazo wezesha uwepo wa mfumo wa maamuzi ya video.​
Haya ni machache natumai kupitia hapa wadau mbalimbali watatoa maoni mengi zaidi kuhakikisha tunakuza soka na ligi ya Tanzania.

Sergio
Hapo kwenye namba 5 ndipo ulipochemka! Ukiendekeza hilo mashabiki hawataruhusiwa viwanjani kwa kisingizio cha corona. Kumbe kilichoko nyuma ya pazia ni makampuni ya TV na mitandao wakitaka kupiga pesa ndefu!!
 
Sawa..je ligi yetu inauzika kiasi hiko...!? Kama hapa ndani tu Kuna baadhi ya timu zikivheza watazamaji hawafiki hata 10 sembuse kuuza haki za matangazo kwenye nchi zingine!?

Nadhan hoja iwe kwanzA kwenye kuboresha ligi yetu na kuifanya iwe na mvuto kwanzA kwetu sisi ..na hili litawesekana Kama lila timu itajengewa uwezo wa kushindana...

Mfano tazama Mbeya city ile ya Kocha Mwambusi. Wakati ule ilikuwa na full support ya mkoa..hamasa ilikuwa kubwa Sana Mbeya..timu yao ikicheza hata na timu ndogo watu walikuwa wanajitokeza kuwashangilia ..sasa ingaliea sasa..Mbeya city imeshuka hamasa..watu uwanjan wameisusa..

So tuzipe hamasa timu zetu kwanzA.kwa khziwezesha kiuchumi..zisajili vizuri. Kisha zishindane kwa uhalali wa kiuwezo ..na kuzingatia sheria za soka..timu ishinde kwa uweoz na sio kubebana..tukifanikiwa kwenye hiki..Hao EPL watakuja kuomba kozi hapa ...watanzania wanapenda soka..Ila soka halijafanyiwa mikakati ya kuwa la.kisasa
Mimi sipingani na hili la uwekezaji kwa watoto, kwani ushiriki wa watoto kwenye michezo mbalimbali huenda sambamba na ukuaji kwa maana ya rika na elimu iwe ya awali, msingi na kadhalika. Nilichokuwa nakilenga ni kudhani kuwa ukosefu wa miundombinu ya kisasa , ukosefu wa rasilimali fedha za kumaliza changamoto zote zinazotukabili na hivyo kutoa mianya kwa wajanja wenye fedha kidogo wenye malengo yao ya siri kuingiza fedha zao kwa mashindano ya muda mfupi ili kupata platform ya kupanda ngazi kisiasa , rejea Mashindano ya Diwani cups huwa yanafanyika kila uchaguzi mkuu ukikaribia then yanatoweka, vipindi vya michezo mashuleni ni kama havina tija tena, vimekuwa ni sehemu ya Waalimu na Wanafunzi kupata muda wa kufanya mambo yasiyokuwa na uhusiano na michezo ama wanafunzi kuvumbua aina mpya ya michezo isiyo rasmi kama vile kukimbizana juu ya madawati. Viwanja vya michezo Mashuleni vimekufa kwa kujengwa madarasa mapya. Mtoto nae amekuwa brainwashed kuwa bila ya kuvaa vifaa maalum vya mchezo husika, ufanisi hauwezi kupatikana hivyo kufifisha hata ile juhudi kidogo ya kujiendeleza. Fedha kidogo inayopatikana kwa ajili ya michezo, tayari wajanja wanakuwa tayari wameishaipigia mahesabu ya kuipiga.
 
Ligi kuu ya wanawake ni copy and paste ya ligi kuu wanaume..kwa sababu timu mbili zenye nguvu ndizo zinatawala pia huko..angalau timu za jeshi zinajitutumia..lakn nazo sioni zikiwa na muda mrefu wa kutamba..maana kwa nzia msimu huu ushindani uko kwa Simba Queens na Yanga Princes ..msimu ujao na mingine Hali itabaki hivi hivi..kwa sababu hizo timu zingine hazina uwezo wa kuhudumia wachezaji kwa msimu mzima..jiulize timu haina hata mdhamini..wachezaji hawalipwi mshahara..wengi wanacheza walitarajia kusajiliwa na Simba Queens ama Yanga Princes ndio angalau walipwe..kwa namna hio ushindani huku nako utakuwa ni zero plus zero...mdhamini aliyepo anatoa milioni 5-19 kwa msimu kwa kila hii pesa uitumie kutunza wachezaji (camp cost) safari za timu kucheza mechi, ulipe mishahara kwa wachezaji na makocha plus gharama zingine kwa timu ..BADO mwenye timu hajajigawi na yeye gawio lake hapo..so unajikuta pesa yote hii hazitoshi hata ..
Timu za majeshi au mashirika kutofanya vzr ni changamoto kubwa ya kukosa uongozi sahihi kusimamia timu husika

Huwa inanifikirisha kiasi
 
Back
Top Bottom