Ushauri kwa serikali

Ushauri kwa serikali

machafuko jr

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2017
Posts
798
Reaction score
1,681
Selikali iongeze tsh 500 kwenye Kila bidhaa ili afya na matibabu yote yawe bure. Asante
 
IMG-20251125-WA0056.jpg
 
Usimamizi wa Rasimali zetu ukiwa mzuri siyo afya na matibabu bure Bali tutakuwa ni Donor Country

Nakumbuka enzi za JPM alipokamata makinikia wengi wetu hatukumuelewa ila Sasa tumeanza kumuelewa na alisema Kuna mikataba mingi sana ya hovyo Serikali za Awamu iliyopita zilisaini na akasema ni kichaa pekee ndiye anaweza kusaini hiyo mikataba.

Sasa turudi katika Awamu hii, badala ya Rasimali nchi zisimamiwe vizuri ili kuwezesha Ajira kupatikana kwa wingi na huduma za kijamii kuboreshwa na kuwa Bure tunaishia kuziuza kwa bei chee kwa waarabu na wachina.

Sasa utaamua mwenyewe, kwa Hali ya Sasa tulipofikia tunaweza KUSIMAMIA hizi Rasimali zetu vizuri kama Gadaffi alibyosimamia Rasimali mafuta na kuwapa Maisha Bora wananchi wake kwa Kila kitu kuwa Bure na kuifanya Libya kuwa donor country with zero debt.

The same apply to Arab Emirates na Asian Tiger countries walivyoweza KUSIMAMIA RASIMALI zao na watu wanakula maisha tu.

Selikali iongeze tsh 500 kwenye Kila bidhaa ili afya na matibabu yote yawe bure. Asante
 
Selikali iongeze tsh 500 kwenye Kila bidhaa ili afya na matibabu yote yawe bure. Asante
Mimi siyo muumini wa Tozo ni muumini wa KUSIMAMIA RASIMALI za nchi vizuri ili kupunguza ugumu wa Maisha kwa wananchi na kuondokana na mawazo ya tozo na KUKOPA na kuongeza deni la Taifa Kila Mwaka.

Uzalendo haipo tena watu wanakula kadri ya urefu wa Kamba zao.

Chao
 
Mmmh kwa kulinda rasilimali tutachelewa sana maana Kuna uvumi unasema watu watu wanamikataba Hadi ya miaka ishirini kwhy kuwatoa inakuwa changanamoto
 
Mmmh kwa kulinda rasilimali tutachelewa sana maana Kuna uvumi unasema watu watu wanamikataba Hadi ya miaka ishirini kwhy kuwatoa inakuwa changanamoto

Kaka hakuna Mkataba usiokuwa na kipengele cha kuvunja Mkataba.

Kila Mkataba lazima HICHO kipengele kiwepo, Mbona enzi za JPM wale Barrick walibanwa mpaka wakakubali kulipa fidia ya mamilioni ya Dola na Mkataba mpya ukaandaliwa na Sasa hivi Tanzania tuna hisa ya 16% kwa Barrick na tuna watu wetu ndani ya Barrick KUSIMAMIA hilo.

Na hiyo 16% ni ya kuanzia lakini Kila baada ya miaka 5 inaongezeka hiyo asilimia kwa asilimia 3% hadi 10% kadri Hali itakavyokuwa inaruhusu na bado Barrick walidhia hilo.

Ni kichaa pekee ndiye atashindwa KUSIMAMIA RASIMALI za nchi ili ziwanufaishe wananchi na kuondokana na umasikini tulionao na kupunguza ugumu wa maisha badala ya kukimbilia tozo.

Kwa kifupi Tozo yeyote itakayowekwa na Serikali itaongeza ugumu wa Maisha kwa Mwananchi masikini wa Tanzania.

Tafuta Blueprint document iliandaliwa enzi za JPM iliangazia sekta zote za uchumi na utitiri wa Kodi, ushuru, Tozo, n.k. ulikuwepo na ilivyomshauri JPM kuondoa hizo Tozo na Kodi zilizokuwepo enzi hizo JPM akiwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara nchini
 
Maniner Weeh! Umelipwa shingapi?
Sijalipwa na yeyote mimi ni job less hapa yenyewe nimeweka bando la jero 245mb na VPN inavopeleka moto sizani kama saa Tisa mbs zitatoboa. Nirudi kwako mbona matusi mkuu
 
Back
Top Bottom