Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,679
- 149,866
Mh.Kubenea,nakushauri swala hili lisiishie Bungeni tu bali uende pia kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuona kama kiwanja hicho kimeorodheshwa kama mali halali ya huyo unaemtuhumu.
Bila shaka ikithibitika kuwa ni mali yake na taarifa za umiliki wa kiwanja hicho hajaziwasilisha katika Tume hiyo,hilo linaweza kuwa ni kosa lingine na hapa sheria itambana zaidi tofauti na adhabu za kibunge.
Navyofahamu mimi sheria inaruhusu mwananchi yeyote kupewa taarifa juu ya mali za viongozi isipokuwa huruhusiwa kuzifanya taarifa hizo kuwa public.
Bila shaka ikithibitika kuwa ni mali yake na taarifa za umiliki wa kiwanja hicho hajaziwasilisha katika Tume hiyo,hilo linaweza kuwa ni kosa lingine na hapa sheria itambana zaidi tofauti na adhabu za kibunge.
Navyofahamu mimi sheria inaruhusu mwananchi yeyote kupewa taarifa juu ya mali za viongozi isipokuwa huruhusiwa kuzifanya taarifa hizo kuwa public.
Alichosema Mwinyi kuhusiana na hoja ya kubenea ni hiki;
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk Hussein Mwinyi, amesema yupo tayari kujiuzulu endapo mbunge wa Ubungo Saed Kubenea, atawasilisha ushahid i kuhusu tuhuma alizotoa bungeni dhidi yake.
Awali mbunge huyo akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/17 ya Wizara hiyo, alidai Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeingia mkataba na kampuni Hainang Construction kujenga nyumba za jeshi ambazo kampuni hiyo itazitumia kwa muda wa miaka 40.
Aidha mbunge huyo, pia alidai bungeni hapo kuwa anazo taarifa kuwa kampuni hiyo itaingia mkataba wa kumjengea nyumba Dk Mwinyi.
Akijibu tuhuma hizo Dk Mwinyi alisema tuhuma hizo hazina punje ya ukweli ndani yake. “Nasikitika kusema mbunge anaweza kuchukua maneno ya mitaani na kuyaleta kwenye chombo hiki muhimu tena bila ushahidi ni hatari sana,”
“...Nakuhakikishia mheshimiwa Niabu Spika tuhuma hizi hazina ukweli na endapo Kubenea atathibitisha nakuhakikishia nitajiuzulu,” alisisitiza.
Aidha alisema kuhusu hoja kwamba kampuni hiyo itamjengea nyumba Dk Mwinyi. “Naomba Bunge litumie utaratibu wa kikanuni, Kubenea akishindwa kuthibitsha maneno haya achukuliwe hatua stahili,”
Alisema ifike wakati wabunge ndani ya Bunge hilo wasitumie kinga ya Bunge na kufanya uchafuzi na udhalilishaji wa majina ya watu.
Knachotakiwa hapa ni kubenea kutuletea mikataba iliyoingiwa baina ya hiyo kampuni na JWTZ wakishirikiana na Mwinyi na ionyeshe vipengele vifuatavyo (1) Kujenga nyumba za jeshi na kuzitumia kwa miaka 40 kabla hawajazikabidhi kwa JWTZ (2) Kumjengea Mwinyi nyumba kama sehemu ya mkataba. Na si suala la umiliki wa kiwanja.