MeinKempf
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 11,094
- 7,218
Miongoni mwa vyombo vya habari vyenye weledi usio na shaka katika habari zake ni BBC Swahili. Nami nimekuwa msikilizaji na msomaji wa chombo hiki kwa muda mrefu sasa hasa nyakati za asubuhi na jioni. Mimi si mwandishi mzuri hivyo usishangae namna ya mtiririko wangu ila kumbuka kuwa mimi ni "PRESCRIPTIVIST".
Siku za hivi karibuni kuna upungufu wa weledi ambao mimi kama mimi ninauona katika habari zao mbali mbali kama ifuatavyo.
1.Kuna makosa ya kiuandishi "TYPO" na baadhi ya sentensi zao kukosa upatanisho wa kisarufi "con-cordial relationship" katika makala na habari zao nyingi, kwa usahihi zaidi naomba ufatilie habari zao wanazorusha Facebook, na kwenye tovuti yao.
N.B: kwa chombo makini kama BBC wanajishushia heshima na credibility ya kuwa chombo cha
kuaminika katika habari zake kwani kinaonekana kuwa na wahariri wasio makini na habari wanazorusha
hewani. Mimi nawaomba walifanyie kazi jambo hilo ili kulinda heshima ya tasnina ya habari hasa ya
kimataifa (waige na kujifunza tokakwa wenzao BBC English) na kadhalika.
2.Kuhusu Kaka Salim Kikeke. Huyu ni mtangazaji mahiri na anayependwa na wadau wengi wa tasni ya habari ya ndani na ya kimataifa nikiwemo na mimi. Ila kuna baadhi ya mbo ninayaona kama hayaendani nae kama mtangazaji wa chombo kikubwa kama BBC. Huyu bwana Kikeke amekuwa akirusha "post" habari flani flani ambazo ninaona kama za "kitoto toto au udaku " katika ukurasa wake wa Facebook na Twitter, yaani habari nilizokuwa nikitegemea nizikute kwenye Global Publishers, Mpekuzi, Audiface, Mambo Mseto, Mambo ya Walimwengu, DJ Sek, na kadhalika ninaziona katika ukurasa wake kitu kinachofanya nione kuwa hatendei haki jina lake na hadhi yake.
N.B: Nimetoa ushauri tu, kama wakiona unafaa waufanyie kazi , kama wakishindwa wapotezee ila nimetoa dukuduku langu kwa nia ya kujenga na sio kushambulia au kuponda mtu flani au chombo flani.
Hivyo mchangiaji naomba awe ni mtu aliyesoma na kuuelewa uzi wangu na awe anayefatilia mambo niliyoainisha vinginevyo ukija kichwa kichwa utatoka kapa na kubaki.
ONYO: Changia hoja kwa adabu na heshima.