Ushauri kwa mabinti: Usikubali kuamuliwa na mtu, maamzi ya maisha yako yategemee furaha yako

Kiti Chema

JF-Expert Member
Oct 18, 2017
1,793
1,941
Nawasalimu nyote wana Jf.

Niende moja kwa moja kwenye maada, Ilikuwa mwaka furani nilipata demu mtaani kwetu aliyekuja kuishi kwa shangazi yake akitokea mkoa fulani hivi, Nilipomtongoza alinisumbua kama wiki mbili hivi kukubali,mwishowe akakubari

Mahusiano yetu yalidumu kwa mda wa miezi 8, Tukaja kuachana kutokana na yeye kutaka tufunge ndoa me sikutaka hizo mambo, nikamuomba nitoe posa kwa wazazi wake harafu nimchukue akakataa akasema anataka ndoa ya kanisani pia akaniambia nitoe posa million 1.8, basi tukaachana

Nikachukua nafasi hiyo me kwenda kusoma chuo swala la kuoa nikaahirisha, basi akarudi kwao, ilipo pita miezi kama miwili akanitafta na kuniuliza nipo wapi mbona kanisani hauonekani wala mtaani sikuoni mimi nikamwambia nimesafiri kibiashara, akasema inamaana kweli huwezi tafta hiyo pesa tukafunga ndoa me nikamkatalia mwisho wa siku nilicho kifanya nikabadiri sim card, tukawa tumepotezana,

Baada ya kumaliza masomo yangu nikarudi nyumbani, alipo niona kananiambia ukweli kuwa aliyemshinikiza maswala ya ndoa ni shangazi yake lakini pia shangazi yake ananichukia mimi, Basi me nilicho mjibu kuwa endelea kuamuliwa maisha yako na mtu, Miezi iliyopita ametokea kijana bodaboda amemchumbia na akatoa posa,

Sasa mpaka sasa Demu yupo kama vile haelewi ni mtu wa kuwatangazia watu kuwa hampendi huyo boda boda alikuwa akinipenda sana mimi ni vile shangazi yake amemshinikiza.

Pia shangazi yake anasauti katika familia maana ndiye mwenye uwezo wa kifedha kwenye familia mme wake ni IT anafanya kazi office ya Waziri ila mke wake ni mwalimu wa primary school.

Juzi alinitafta bint kunielezea hisia zake, me nilimsihi amalize alicho kianzisha asije vunja ndoa yake kwa kutokuwa na msimamo, Ameshindwa kabisa kudhibiti hisia zake, amesema mwisho wa siku anaweza fanya maamzi ya kutoroka na kususia kufunga ndoa maana hajamkubali huyo jamaa wala hana hisia naye.

Ushauri kwa mabinti: Usikubari kuamuliwa na mtu, maamzi ya maisha yako yategemee furaha yako na sio mtu mwingine awe na nguvu juu ya maisha yako
 
Achana nae huyo. Mademu wanaovuta bangi iliyochanganywa na ugoro ukiwafuata unaweza sema umerogwa kumbe unadeal na mtu asiyejitambua.
 
Kilichopangwa na Mungu hakifeli hata nukta! Kama ni wako na itakuwa hivyo tu.

Hakuna kauli mbaya kama kusema "over my dead body"!. Huwa vinapinduka
 
Kilichopangwa na Mungu hakifeli hata nukta! Kama ni wako na itakuwa hivyo tu.

Hakuna kauli mbaya kama kusema "over my dead body"!. Huwa vinapinduka
Nakubali mkuu, heshima yako, mchango wako hapa Jf, ni mkubwa mno
 
Back
Top Bottom