Nitaanza kwa kifupi kueleza makosa ya kijinga waliyofanya CHADEMA kabla ya kuelezea yale ya msingi;
1. TAMAA – Viongozi wakuu wa CHADEMA walipata UROHO wa ghafla wa kutaka kuingia ikulu kwa namna yeyote, wakasahau misingi, wakaivunja UAMINIFU (LOYALTY) kwa wananchi walioujenga kwa miaka mingi na kwa nguvu kubwa iliyojumuisha DAMU ya watanzania. Tamaa ikawafumba macho, ikatawala akili zao, ladha ya madaraka ikatawala mioyo yao.
2. JEURI – Viongozi wa CHADEMA walipatwa na jeuri, jeuri ambayo asili yake ni FEDHA aliyokuja nayo EDWARD LOWASSA, wakadharau ushauri, wakapingana na wataalamu wao waliokuwa wakiwaamini miaka yote. Wakawashushua na kuwaona sio lolote si chochote pale walipowaeleza hatari ya kumpokea EDWARD ndani ya CHADEMA.
3. KIBRI – M/kiti wa CHADEMA na genge lake wakapatwa na kibri, wakaacha Mbachao kwa msala upitao. Wakawashambulia wenzao Slaa, lipumba na kila aliyepingana nao katika wazo lao la kumuweka EDO kuwa nahodha wa chombo chao. Wakaamini katika Edo na Matajiri wenzake wanaomuunga mkono. Ujuaji ukawa mwingi na kujiona wao ni zaidi ya kila mtu.
Mwisho wa Kunukuu.
Sasa turejee hoja chache za Juliana... kupitia watu wafuatao.
1. Jecha s. Jecha(Kibri na Jeuri)
2. Dr. Shein (Tamaa)
3. Magufuli (JEURI)
Juliana wewe na Mbowe mna kitu mlinyimana/mlitofautiana. Maana ugomvi wako mkuu si wewe na CHADEMA, bali ni wewe na Mbowe.