Juliana Shonza
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 2,009
- 1,607
Mwandishi maarufu wa Vitabu, Mmarekani mwenye asili ya Italia, anayeitwa MARIO PUZZO aliandika maneno yafuatayo katika moja ya vitabu vyake maarufu, kinachoitwa ‘’THE GODFATHER” ninamnukuu;
MWENYE - ENZI MUNGU alipomuumba mwanadamu alimpa MWONGOZO kisha akawatuma Mitume yake ije iufundishe muongozo huo kwa watu, kisha ikawekwa bayana kuwa atakayeufuata Muongozo huo ataongoka na atalipwa PEPO na atakayeuacha ataangamia na MOTONI yatakuwa ndio marejeo yake.
Katika Zaburi 51:6 inasema “Tazama wapendezwa na KWELI iliyo moyoni nawe utanijulisha hekima kwa siri” walio wakristo wenzangu wanafahamu mstari ukianza na neno ‘TAZAMA’ inamaanisha nini.
Baada ya utangulizi huo, kila mmoja wetu anajua kuwa LOWASSA kashindwa kwa aibu kwenye uchaguzi mkuu wa October 2015 na ni wazi kuwa MAGUFULI ndio rais wa AWAMU YA TANO wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA ambaye amekuwa ni MFANO WA KUIGWA duniani kote.
Naandika maneno haya, nikielezea kwa ufupi kabisa sababu zilizoipandisha na kuishusha CHADEMA hata kushindwa kwa aibu kabisa katika uchaguzi wa mwaka jana ili andiko hili liwe fursa ya kuamsha akili zao zilizolala.
Ikumbukwe kuwa CHADEMA ilipanda na kukubalika kwa watanzania wengi kutoka na IMAGE ‘taswira” yake ya kutetea wanyonge, kutetea haki, uzalendo na kupinga ufisadi. Waki-stress katika hoja ya RUSHWA kama kiini cha Umasikini wa WATANZANIA.
Katika uchaguzi uliopita hali ilikuwa tofauti, walifanya makosa yatakayogharimu ‘uwepo’ wao katika ulingo wa siasa za nchi hii, makosa hayo ni kama yafuatayo;
Nitaanza kwa kifupi kueleza makosa ya kijinga waliyofanya CHADEMA kabla ya kuelezea yale ya msingi;
1. TAMAA – Viongozi wakuu wa CHADEMA walipata UROHO wa ghafla wa kutaka kuingia ikulu kwa namna yeyote, wakasahau misingi, wakaivunja UAMINIFU (LOYALTY) kwa wananchi walioujenga kwa miaka mingi na kwa nguvu kubwa iliyojumuisha DAMU ya watanzania. Tamaa ikawafumba macho, ikatawala akili zao, ladha ya madaraka ikatawala mioyo yao.
2. JEURI – Viongozi wa CHADEMA walipatwa na jeuri, jeuri ambayo asili yake ni FEDHA aliyokuja nayo EDWARD LOWASSA, wakadharau ushauri, wakapingana na wataalamu wao waliokuwa wakiwaamini miaka yote. Wakawashushua na kuwaona sio lolote si chochote pale walipowaeleza hatari ya kumpokea EDWARD ndani ya CHADEMA.
3. KIBRI – M/kiti wa CHADEMA na genge lake wakapatwa na kibri, wakaacha Mbachao kwa msala upitao. Wakawashambulia wenzao Slaa, lipumba na kila aliyepingana nao katika wazo lao la kumuweka EDO kuwa nahodha wa chombo chao. Wakaamini katika Edo na Matajiri wenzake wanaomuunga mkono. Ujuaji ukawa mwingi na kujiona wao ni zaidi ya kila mtu.
Ukiacha makosa hayo ya kijinga, lipo kosa la msingi kabisa walilofanya CHADEMA, nalo si jingine isipokuwa ni kosa la KUACHA MISINGI yake. CHADEMA iliundwa ama kuasisiwa ikiwa na values na commitment zifutazo;
1. Image ya unyonge, u-nyerere na Uzalendo.
Watanzania masikini waliiona CHADEMA kuwa ni chama chao, wakakichangia kwa mali kidogo walizonazo, wakajitoa kwa hali na mali, wakawa tayari kufa ili kuinusuru CHADEMA wakiamini kuwa ni chama chao.
Lakini CHADEMA ikaamua kuwasaliti Masikini wa Tanzania, wakaamua kuukataa U-nyerere [wakajivua image ya ukombozi] wakasikika wakimkosoa hadharani na kupayuka kuwa Nyerere hawezi kuwa Mungu. Wakajivua uzalendo, wakaacha kuchangisha na kutegemea ruzuku ya Edward na Rostam et al.
2. Kuzika HOJA ya UFISADI.
Chadema waliamua kuikataa, kuipinga na kujiweka mbali kabisa na HOJA ya kupinga UFISADI wakawa wako busy kuwasafisha mafisadi. Sidhani walifanya tathmini kiasi gani lakini confusion iliyozaliwa katika vichwa vya watanzania haikumithilika.
Hoja hii ndio iliyoijenga na kuitambulisha CHADEMA kwa watanzania, imani ya watanzania kwa CHADEMA ilitokana na hoja hii. CHADEMA wakaachana na hoja hii kimzaha mzaha kabisa. Hoja iliyobeba UHAI wao.
3. Kuunda AJENDA mpya ya MFUMO.
Baada ya kuzika hoja ya UFISADI wakaibua hoja mpya ya MFUMO, wakawaambia watanzania kuwa ajenda yao ni kuondoa mfumo, kwani wamegundua kuwa tatizo sio WEZI, wala rushwa bali ni mfumo ndio unatengeneza wezi na rushwa – hoja ya hovyo kabisa.
Hoja hii si tu kuwa HAIKUELEWEKA kwa Watanzania lakini imeendelea kuwa MAZINGAOMBWE hata kwa wasomi wenye ufahamu kujua kusudi na maana halisi ya MFUMO kama inavyotumiwa na CHADEMA.
4. MBOWE kuendelea kuwa M/kiti wa CHADEMA.
Miaka ya nyuma kidogo, nilieleza doubts zangu katika uwezo na maarifa ya MBOWE katika kuki-transform chama na kukiwezesha kushika dola, sikueleweka, labda sasa nitaeleweka. Lakini hata nikieleweka sasa, it’s too late, Chadema imeshapoteza watu muhimu, wasomi wenye maarifa, viongozi wenye uzalendo na kweli katika mioyo yao, wamepoteza waadilifu na sifa ya uadilifu, Chadema ya leo iko mikononi mwa wezi na mafisadi wa nchi hii, hakuna namna wanaweza kuondoka kirahisi, hata ikiwa MBOWE atajiuzulu sasa.
Mbowe betrayed principles and pillars of the family, amedanganywa akadanganyika, amepoteza legitimacy ya ku-lead the family, amekiuka misingi na commitment in the family – He must be disposed.
5. CHADEMA hawana utaratibu wa kujifanyia TATHMINI.
Chama makini hujifanyia tathmini kila jioni,kila mwezi, kila mwaka na kila baada ya tukio kubwa kama la uchaguzi. Chadema wanahitaji in-depth evaluation lakini najua kwa hakika hawatofanya kwani wao wanaamini kuwa wao ni intelligent kupindukia, hivyo hawakosei na hivyo hawana utaratibu wa kurudi mezani kujitathmini. Hili ni kosa la msingi kabisa, maana kama wangelikuwa wanafanya tathmini wasingelikubali LOWASSA kuwa mgombea wao wa milele (maana amejitangaza kuwa 2020 yumo).
Kwa makosa hayo, yote ya aina mbili yale ya msingi na hata yale ya kijinga CHADEMA imepoteza LOYALTY kwa watanzania, hawaaminiki tena, ndio maana wamepoteza uchaguzi uliopita na watapoteza zaidi.
Katika kitu kigumu ku-regain ni LOYALTY (UAMINIFU) kwani uaminifu ni kama roho, ikiachana na mwili haiwezi kurudi kwenye mwili huo. Once it’s gone, it is gone forever wenye akili mwili ukiachana na roho wanauchukua mwili huo na kuuzika haraka kabla haujaanza kuharibika na kutoa harufu mbaya, CHADEMA imeachana na ROHO yake, wenye akili wanajua kuwa MAITI mahala pake KABURINI.
“We are a family, and the LOYALTY of the family must come before anything and everyone else. For if we honor that commitment, we will never be vanquished – but if we falter in that loyalty, we will all be CONDEMNED”