Ushauri kwa Diamond Platnumz

perfect_rahym

Member
Mar 27, 2017
41
45
Na Saleh Ally

NARUDI nyuma kidogo, nataka kukumbusha namna ambavyo niliwahi kuandika kuhusiana na namna ambavyo mwanamuziki Nasibu Abdul, maarufu kama Diamond, kwamba ameanza kukosea vitu kadhaa, hasa kuiga video za wasanii wengine.

Nilieleza kwa mifano ya picha namna ambavyo Diamond aliiga karibu kila kitu kutoka katika video ya msanii mmoja, kuweka kwenye video yake. Halafu akarudia namna hiyo baadaye, jambo nililoliona ni la kustaajabisha kabisa kwa kuwa wimbo huo aliouiga haukuwa hata na miaka miwili sokoni!

Baada ya kuandika, nikaweka kila kitu kwa mifano. Kilichofuata ni baadhi ya watu walio na Diamond kuanza kulalama kwamba ninamsakama.

Mbaya zaidi, mwandishi mmoja wa Mwananchi ambaye ni kati ya watu niliowafundisha namna ya uandishi bora wa uandishi wa burudani alinifuata na kuhoji mbona “natumiwa”, kumsakama Diamond. Nilimuuliza maswali kupitia makala niliyoandika, hakuna alichojibu!

Baadaye niligundua ameingia kwenye mkumbo wa zile “Team”, jambo ambalo ni baya kabisa kwa mwandishi.

Lakini hivi karibuni, Diamond alikosolewa kwa nia njema kabisa kuwa vizuri akawa anafanya shoo za nyumbani kwa ajili ya watu wake ambao ndio wanaomfanya leo asikike kote duniani.

Mhamasishaji na mjasiriamali, Eric Shigongo alishauri hivyo akitaka Diamond na uongozi wake, kupunguza bei za shoo kwa mapromota ili nao watoze viingilio vya chini kwa Watanzania. Nalo hilo likawa kosa, Meneja wake Babu Tale, akacharuka kwamba kazi yake inaharibiwa akiamini eti, Diamond anashambuliwa!

Baada ya hapo akaanza vitisho eti atamuandika vibaya Shigongo mtandaoni, kwa madai yeye ni maarufu huko mtandaoni kwa kuwa ana watu milioni 1 wanaomfuatilia! Akafanya hivyo, hakukuwa na faida yoyote kwake, zaidi ya yeye kushambuliwa, watu wakiamini hakuelewa!

Tale hakuwa amejibu hoja hata kidogo kuhusiana na kilichoandikwa kama ilivyokuwa awali, zaidi ya kusema maneno mengi akitoa data za uongo huku akitengeneza filamu eti katishiwa kuuawa.

Hii inaonyesha kiasi gani Diamond amezungukwa na watu wanaoweza kumtengenezea mazingira ya kuwa hawezi kushauriwa, hawezi kuhojiwa, ni mtu anayejua sana na wao wanajua kila kitu cha muziki wakati rekodi zinaonyesha waliofaulu zaidi ni waliokubali kukosolewa.

Picha inayotengenezwa, kumueleza jambo Diamond kwa nia nzuri ni kumshambulia. Picha inayotangulizwa, chochote atakachofanya Diamond aachwe, “yeye ni yeye.” Mimi ninaamini hilo halitakuwa na nafasi na kwa kuwa ni msanii wa Tanzania, ataambiwa na mimi safari hii naendelea kumuambia bila ya hofu ya huo mtandao wa watu milioni moja wa Babu Tale na vizuri atakayetaka kuzungumza na mimi, twende kwa hoja ili tujenge.

Kutishiana mtandaoni eti watu watakutukana ni mambo ya kipuuzi ambayo wakati mwingine hupaswi kuyasikia yakizungumzwa na mtu unayeamini amefikia kiwango cha kuitwa kiongozi.

Diamond ametoa wimbo mpya uitwao “Acha Nikae Kimya”. Tayari mashabiki wengi wa muziki wameanza kumshambulia Diamond mitandaoni.

Nimeona wakishambulia katika hali ambayo inaonyesha wazi kuwa wamekerwa na uamuzi wake wa kutoa wimbo ambao ukiusikiliza kwa makini umelenga kumsafisha mkuu wa mkoa ambaye yuko katika sakata la vyeti.

Lengo ni kuona mkuu wa mkoa huyo anarejea katika heshima aliyopewa na wananchi hapo awali, lakini baadaye wakaichukua wananchi hao baada ya kuona hawastahili kumpa hasa baada ya kushindwa kulimaza suala walilohoji naye akashindwa kujibu na zaidi ikawa ni kutishiana tu.

Ndani ya wimbo huo unaoonyesha wazi unalenga kutengeneza mazingira ya kupoza hali iliyopo mfano, kama kile kipande anachosema: “Nyumbani nafungua geti, niende kwa Mangi kununua supageti, napewa za chini ya kapeti, kuna redio imevamiwa eti.”

Najua ukimuuliza atasema alikuwa anatafuta vina, lakini baada ya redio imevamiwa, neno eti, linamaanisha hakuna uhakika.

Hii yote ni kuonyesha kuwa hakuna redio iliyovamiwa kama ambavyo wengi wamekuwa wakifikiria. Kwa waliovamiwa na walio karibu yao au waliounganisha machungu katika hili ni sawa na kuwatonesha kidonda.

Najua ndani ya waandishi wenyewe wako walio tayari kugawanya machungu. Lakini ukweli mwenye akili timamu hakuna anayeweza kuunga mkono chombo cha habari kuvamiwa kwa visingizio visivyokuwa na msingi. Hata Diamond, amekuzwa kufikia alipo na vyombo vya habari hata anavyovidharau akaamini vinazidiwa na mtandao, ndiyo vilimpa nafasi watu wakamjua!

Kama hiyo haitoshi, kuna sehemu anaimba hivi;

“Napita kwenye magazeti, nakuta rundo la watu wameketi, badala ya kutafuta senti, wanabishana tu mambo ya vyeti. Acha nikae kimyaaa.”

Hii ni kuonyesha kwamba hakuna sababu ya watu kubishana mambo ya vyeti na yeye anawashangaa.

Lakini hakumshangaa kiongozi ambaye ameshindwa kuweka vyeti vyake hadharani baada ya kuonekana kuna walakini. Kiongozi ambaye ameshindwa kuonyesha ni kiongozi thabiti ambaye alipaswa kuwa wazi na kuwathibitishia wananchi wake wanachohoji.

Kama unataka watu wawe safi, unataka watu wafuate taratibu, kanuni na sheria. Vipi wewe umeshindwa kuthibitisha unavyo, uonyeshe? Vipi Diamond anakubali kujiangusha aonekane anafurahia visivyo sahihi? Uko wapi uongozi wake na unashindwa kuona hili? Kwa nini unaachia haya yapite na kunipa mimi nafasi ya kuandika ili kesho wadai ndiye nilimshusha Diamond?

Je, Diamond yuko tayari kuwakandamiza wananchi wote ambao ndiyo wamekuwa wakimsapoti yeye miaka yote kwa ajili ya kumfurahisha mtu mmoja?

Wale wanaomshambulia mitandaoni ni kuonyesha kuwa ni kosa kubwa kuamini una akili nyingi kuliko kila mtu.

Alichotakiwa Diamond ni kukemea vyanzo vya tatizo na si kuwakemea au kuwashangaa wale wanaotaka kuchukua chanzo cha tatizo.

Kama Diamond ameamua kuingia kwenye “siasa nyepesi”, vipi Babu Tale haoni kuwa anaharibu biashara yake? Vipi halalamiki au naye hayuko katika kampeni ya kushika taulo na kufanya usafi wa waliojichafua wenyewe?

Halafu jiulize, huu mjadala si ulifungwa? Sasa Diamond anapouamsha anataka nini? Naye anatumika?

Mimi nataka kuwa huru, nataka kuwa mwandishi ninayesema ukweli bila ya hofu ya kutekwa au kuwekwa ndani eti kwa kuwa nimemuambia mtu fulani ukweli.

Nataka kuwa huru na kusema ukweli kwa lengo la kuweka mambo sawa na kurekebisha taifa langu bila ya kuogopa eti mtu mzima mwenye akili zake atanitishia kuniweka nitukanwe mtandaoni.

Nasema sitaogopa kwa sababu viongozi wa mikoa waliopewa dhamana ya kutuongoza wanataka kututisha kwa kuwa wana uwezo wa kukuweka ndani mwandishi hasa wale wanaoonyesha si wapambe wao.

Diamond aachane na “siasa nyepesi”, anatakiwa kuusoma upepo na kuwa “intelligent” badala ya kukubali kutumiwa kusafisha mkono wa wenzake huku wa kwake ukijaa masizi.

Kuna ule msemo wa sanaa usemao hivi: “Music expresses that which cannot be said and on which it is impossible to be silent.”. Muziki unaweza kufafanua kile ambacho hakiwezi kuzungumzwa, tena katika kipindi ambacho haiwezekani kuwa kimya.

Huenda ulikuwa wakati mzuri kwake Diamond kuchagua kukaa kimya kweli, kuliko kusema yuko kimya huku akijaribu kuonyesha Watanzania hawawezi kuelewa.

Badala ya kukimbilia udhaifu ili kufurahisha nafsi ya mtu, kama angetaka kusema, angeonyesha ni imara kueleza kile ambacho hakielezeki katika kipindi ambacho watu wako kimya.

Wanaokasirika wanajua wanataka kufanywa wapuuzi. Waliolalamika wanakasirishwa na kuonyesha wanacholalamika wao ni kazi bure.

Mimi nashangazwa na Diamond anayetaka kubomoa matofali ya ukuta wa nyumba yake aliyoijenga kwa shida huku akitaka kujenga ukuta wa jirani aliyeubomoa wa kwake baada ya kulewa sifa.

Muziki kila mmoja ana mwisho wake, hakuna aliyewahi kutamba milele. Nimepata bahati ya kuwaona wanamuzi wengi maarufu nikiwa mwandishi chipukizi na mwandishi bora wa burudani wa nchi hii.

Nakumbuka ufalme wa Mr 2, wakati huo tukimuita 2Proud, usimsahau Profesa Jay. Nakumbuka ufalme wa miaka ya Juma Nature, baadaye makundi ya TMK na East Coast. Nakukumbusha umalkia wa Lady Jaydee. Najua hautakuwa umemsahau Mr Nice.

Ufalme unaweza kuwa wa muda mrefu au ukaporomoka haraka kulingana na mmiliki wa ufalme mwenyewe. Ninaamini siku moja atakuja mfalme mpya au kipenzi kipya cha Watanzania. Lakini ni vizuri Diamond akaepuka kuharibu kazi ya Babu Tale na ikiwezekana kuhakikisha anajenga misingi mizuri ili ukifika wakati wa kuondoka, aondoke kwa heshima. Wakati huo, Watanzania watakuwa wakiendelea na mfalme mwingine na hayo ndiyo maisha bora.
 
Tatizo analokumbwa nalo Diamond ni moja..
Hana Managers wala advisors.

Ana WAHUNI ambao ndio Managers wake..
Hao ni Tale na Salam..

Ana wasaka Tonge ambao ndio advisors..
Hao ni kina Le Mutuz na wengineo.
 
Kaongea ukwl simba bora akae kimya ana mama ana watoto yeye ndo kila kitu kwny familia yao ila ukwl unauma ishu ya vyeti ilikula mda wetu sana laiti baadhi yetu tu geutumia kufanya kaz !katuchana kwny kawimbo .. Hahaaa...ila k .ukwl simba asingenguruma angebakia neutral tu wala isingemcost sasa mrengo wake unajulikana kitu ambacho ni kibaya kwa team zetu bongo..ila namkubal simba asilimia elfu moja hata kitokee nn i will always be his loyal fan..long live simba na wew binadamu tu hakuna asiyekosea..
 
Saleh anatetea ugali wake tu.......kama unamfahamu usingetaraji kitu tofauti na hiki alichoandika!
Eric ni mnafiki na mzandiki,mwenye roho mbaya na mpenda sifa tu....Mashaka Matongo(Abiola) is one of his early vitims.
It was expected that his employees would jump to his defence.
 
Diamond hajui umuhimu wa vyeti ...sidhani kwenye ukoo wao kuna MTU msomi na kama yupo labda wa makopa
 
Tatizo analokumbwa nalo Diamond ni moja..
Hana Managers wala advisors.

Ana WAHUNI ambao ndio Managers wake..
Hao ni Tale na Salam..

Ana wasaka Tonge ambao ndio advisors..
Hao ni kina Le Mutuz na wengineo.
Managers wake na advisors ni bashite babu talent etcc so usitegemee jipya ni kikundi kipya cha.......[HASHTAG]#ney[/HASHTAG] aliweka fumbo##
 
Diamond hajui umuhimu wa vyeti ...sidhani kwenye ukoo wao kuna MTU msomi na kama yupo labda wa makopa
Wewe uliyesoma utamfikia diamond hata kwa chembe ya mchele? Kutwa na mabahasha kwny ofisi za watu ukipata chance ya kusoma soma hasa tena hasa lkn usimdharau pia ambaye hakusoma maana weng tu wanatoboa!tumeona tuna ushuhuda kusoma ni kitu kingine na kuaply elimu ktkt daily routine kitu kingine kabisa..
 
Wewe uliyesoma utamfikia diamond hata kwa chembe ya mchele? Kutwa na mabahasha kwny ofisi za watu ukipata chance ya kusoma soma hasa tena hasa lkn usimdharau pia ambaye hakusoma maana weng tu wanatoboa!tumeona tuna ushuhuda kusoma ni kitu kingine na kuaply elimu ktkt daily routine kitu kingine kabisa..
ushauuri wangu wekeni hash tag vyombo vyote vya habari visivyokubaliana na ushenzi wa Makonda viache kupiga nyimbo zake sawa na waliviyoacha kuandika habari za Bashite, pili, swala la kumuibia Saida Karoli wimbo wake lishughulikiwe kisheria tuanze kuheshimiana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom